Kwa sasa Mrusi ndiye yupo kwenye offensive, maana kwamba yeye ndiye anashambulia, Ukraine wao wanaendelea kupambana kuhimili mashambulizi yake.
Kihistoria Urusi wakifanya mashambulizi wao hupigana kizalendo na wapo radhi hata kufa mamilioni lakini wafanikishe lengo, ndicho walikifanya kwenye vita vya pili vya dunia, waliuawa mamilioni lakini walisonga mbele kwa mbele mpaka wakaingia Berlin kwa Hittler.
Lakini kwanza huwa mwanzo uwaaminishe kwanini wapigane, kwanini wajitolee kufa, uwachochee na kuwapa mzuka, ila kwenye huu ugomvi Putin kawakanganya kwa kukurupuka, amewatumbukiza kwenye ugomvi ambao hawauhitaji na hawautaki, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii kama Quora utaona namna gani Warusi wanapinga hivi vita.
Pia kwao kule wanakamatwa wengi wanaothubutu kufanya maandamano ya kupinga hivi vita vya Putin.