Hiyo iliyokuwa grounded ni batch fulani ya F-35B. Wameziground ili wafanye uchunguzi, kila ndege ya Marekani ikipata hitilafu huwa wanazipiga chini aina fulani au batch fulani ili kujiridhisha.
Marekani ina maelfu ya ndegevita, F-35 pekee zipo zaidi ya 800 duniani kote hivyo rate ya ajari ni kubwa kuliko hizo Su-57 zenu ambazo hata 20 hamna. Nyinyi ndege zenu mnatumia kwenye gwaride kuliko mnavyotumia vitani, hamuwezi pigana na Ukraine inayoombaomba air defence systems sijui hizo ndege zitaweza nchi gani ya NATO.
Kwanza Su-57 haina injini, inatumia injini ya Su-35. Wazo la kuwa na stealth jet walianza during Cold War kama response ya F-22, project ikacheleweshwa mpaka Marekani ikaanza stealth nyingine F-35. Urusi wamefufua project miaka kumi na ngapi uko hadi leo ndege haina injini yake. Subiri Su-57 iondolewe injini za AL-41F1 ipewe Izdeliye 30 ndio uwaze mass production na hela yenyewe hamna. Kwanza Saturn hizo injini sijui watazifanikisha lini na hizi sanctions zilizopo.
Ile ndege yenu ya kwenye maonyesho Su-75 Checkmate imefikia wapi? Na ile PAK DA stealth bomber imefika wapi? Nayo mmemjibu Mmarekani na B-2 Spirit ila kashazindua B-21 Raider na bado hamna matumaini. Kwanza mambo ya stealth sio level zenu kwa sasa, vipi kuhusu Mig-35 mnazo hata za kutosha squadron mbili? Na mbona haziuziki hizo ndege wateja wakitia nia mazungumzo yakianza wanakimbia sijui wanagundua nini.
Air force nzima ya superpower haiwezi fanya hata SEAD mission sasa utamuuzia nani hizo ndege. Si bora wateja wanunue China, si bora wachukue Saab za Sweden. Uzuri mnauza bei ndogo na hakuna masharti. Iran akinunua hizo Su-35 za deal la sasa naamini mtatumia miaka mingi bila kupata mteja wa hivyo