Rafiki yangu Proved ,kabla ya mgogoro huu nilikua nakuona kama mtu unaelewa mambo kwa haraka sana.
Ila kwa michango Yako humu unaonekana ni mtu tofauti kabisa.
Rafiki Iko hivi?
Nilishakueleza vizuri huko juu,hata hivyo Sasa hivi ntaeleza kwa mtindo mwingine.
NATO sio umoja wa kutoa michango ya silaha kwa nchi wanayotaka kuisaidia,bali NATO huingia vitani kamili kwa kuingiza wanajeshi wake ambao wengi wako west Europe na wengine huongezwa kutoka nchi wanachama pale inapohitajika.
Sasa kwa kuangalia body language TU ya NATO ni kwamba wameipenda sana Ukraine na hata kufanya Kila mbinu ili ijiunge na NATO sema Urusi imekua ikitibua.
Sasa nchi wanayoipenda kwa kiwango hicho Leo hii imevamiwa na inapigwa Hadi kumegwa ardhi yake.
Tena inapigwa na nchi adui ambae ndiyo aliepelekea kuundwa kwa NATO.
Kumbuka NATO haikuumdwa kwa ajili ya kujihami dhidi ya Africa,Asia, South Amerika wala middle east.
NATO iliundwa kwa ajili ya Urusi.
Leo hii Kwa mapenzi waliyonayo NATO kwa Ukraine kwa mara ya kwanza NATO safari hii hawajatumia jeshi lake kamili Bali wanachangishana silaha,Tena kwa masharti ya silaha zisizoweza kufika ndani kabisa ya Urusi. Umeona hiyo?
NATO wan jeshi kamili la askari wa miguu,wakiwa na silaha zote,wan jeshi la anga na Majini.
Kwa huruma walioonesha juu ya Ukraine ilikua ndio muda Sasa wa kuingia jeshi lote la NATO na kumsaidia Ukraine. Zaidi ya hapo wanamuogopa Urusi kubali kataa.
Rais wa USA kaka mkubwa wa NATO aliiambia Dunia safari hii hatutapeleka jeshi Ukraine kwa sababu safari hii tunadili na moja kati ya jeshi kubwa sana hapa ulimwenguni.
Urusi sio mtandao wa kigaidi.
Hapa ni kama kusema sisi USA tumezoea kudili na vijitaasisi vidogo kama Al-qaida,Isis na nk.
Kwa hiyo kupeleka silaha kwa mtindo wa kuchangishana,NATO wanashiriki vita hii kwa uoga na kujifichaficha.
Sio utamaduni wa NATO na sio kawaida ya NATO.
Ukisema Ukraine sio mwanachama wa NATO majibu unayo kua NATO walishazipigania nchi ambazo sio hata wanachama wa NATO.