LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
NATO wanataka rushia apigane na ukrein mpaka pumzi imwiishie alafu ndio waje kumchakaza kabisa kijeshi
 
Umechanganya MAHARAGE NA BAMIA MZEE. umeandika UPUPU.
 
Suluhisho sidhani kama litapatikana
Maana matakwa ya Putin ni kama hayatekelezeki na yeye kashikilia hapo hapo
Apo apo huwa najiuliza kwanini wanayapuuza ilhali kuna uwezekano aa kukaa chini wakayuzungumza kuliko kuacha raia waendelee kuumia...

Kingine nachojiuliza zaidi, hasa hasa likija swala la taarifa kwa ujumla.

Naona vinafungiwa vyombo vya habari vua kirusi, ila hili linaonekana ni kawaida na inatakiwa. Papo hapo vikifungiwa vya nje ndani ya Urusi tunaambiwa wanaminya uhuru wa habari.

Sasa hii double standard kwanini inakuepo kwenye dunia ya "Free of Speech"... Ni nini kinachojaribu kufichwa. Kwanini wastuache huru tusikilize hoja pande zote mbili ili tupate kuamua kwa ufasaha.
 
Sio amekosa ni kwamba Hujui,.....
Hata hiyo corona hujui pia.
 
Mbona hoja za pande zote zinafika hapa kwetu? Hoja za Urusi zinatagazwa kote, maana kwa inataneti isiyozuiliwa kila mtu anapata yote.
Ninavyoelewa ndani ya Urusi wanabana sana habari. Walitangaza sheria eti ni marufuku kusema "vita" - kuna "operesheni maalumu ya kijeshi".
Kukaa chini - labda vigumu kidogo wakati unafyatuliwa risasi??

Je tuko pamoja ni nani aliyeanza kuvuka mpaka na kufyatulia risasi?
 
pole MKUU
 
Ok sawa em twende polepole, nachotaka mie ni kuchuja hoja za pande mbili bila kuweka mahaba.

Kusema kwamba "Internet" ndo source ya taarifa sizan kama kila taarifa inayowekwa apo ni sahihi.

Mfano mdogo ingia YouTube af kisha angalia wanachokipost watoto zetu juu ya mambo yanayoendelea apo nchini. Kisha jiulize wanachokipost na uhalisia uliopo ka unaendana.

Najarib kua na 'Cautious' kwa kila taarifa inayopenya kwenye masikio yangu kwasababu tuliopo hivi sasa. Unaeza ukaaminishwa kumpenda mtu mwenye asiye na salama na wewe kisha ukaaminishwa kumchukia mtu aliye na salama na wewe.

Kuhusu kama ni Vita au si Vita huwa najiuliza swali, hivi inawezekana ukatokea uvamizi apo nchini Tz. Wavamizi waue Raia ndani ya Week mbili zote waishie Raia wasio fika ata 500...?
 
Kukaa mbona wanakaa sana na kinaelekea kikao cha tatu ila viwili vyote vimeshindikana
 
Kukaa mbona wanakaa sana na kinaelekea kikao cha tatu ila viwili vyote vimeshindikana
Hapo sasa ndo huwa nawashangaa sana "Politicians".... Wako vzuri kutoa hint ya hiki na kile kifanyikaje kwa interest zao binafs chini ya mwamvuli wa "National Interest".

Wakati wengine wanaangamia wao wanashinda kwenye ma'office wakitoa maagizo.

Huwa naendelea kuwaza nje ya box ka ni kweli "Democracy" power inatoka kwa watu (Raia) kwa ajili ya watu (Raia)... Zaidi huwa naona kama Raia huwa ana maamuzi wakati wa uchaguzi tu baada ya apo ni matakwa na mapendeleo (Interest) za mtawala ndo zitakazoendelea.

Kwasababu kikawaida nadhania ka ikipigwa kura kwa wananchi wa pande zote hizo mbili yani Russia na Ukraine kati ya mapigano au kukaa chini wazungumze... Naamini watachagua cha pili.

Hakuna wanaopenda Vita, hakuna wanaopenda uhasama, ila hakuna pia anaependa kukaa kwa mashaka kwasababu ukaidi wa jirani yake.
 
Kifupi hii vita kujua nani anampiga mwenzake angali mashirika ya Wakimbizi, Haki zq binadamu wanasema nini? Utakuwa ni ujinga kusema Russia imeziwa sana huku wananchi wanakimbia nchi na kuwa wakimbizi nchi za jirani.
Ni kweli kuwa hata Russia kuna vifaa vinaharibiwa lkn Ukweli ni kuwa Ukraine imezidiwa mnoo.
Ikumbukwe si tu kuzidiwa pamoja na misaada ya kivita anayopatiwa na nchi za USA, na washirika wake amefanya ku slowlkn wanapigika tu

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Taarifa za pande zote mbili zinapatikana kupitia intaneti. Sahau Youtube. Sahau Facebook. Twita - ukijua ni nani anayeandika, menginevyo sahau. Intaneti ni chombo cha habari. Lazima uweza kutofautisha chanzo kinachoeleweka na kurasa ambazo huwezi kutambua ni nani.

Unaweza kuangalia https://tass.com/ unapata kila propaganda kutoka Urusi (wakati mwingine hata habari - hapo na pale).
Fungua kurasa za habari kama Aljazeera, BBC (MArekani sipendi sana kugusa) maana unapata hapa habari zinazoandaliwa na watu wanaojua kazi. Pia na watu wanaotoa masahihisho kama wamaandika kimakosa.

Sielewi kwa nini unarudia swali la wahanga 500?? Usipoteze wakati youtube, angalia habari za wanahabari. Leo nasoma Aljazeera: "Ukraine said at least 1,170 civilians had been killed in Mariupol since the start of the invasion, and 47 were buried in a mass grave on Wednesday. It was not possible to verify the figures."
Mariupol ni mji mmoja tu.
Idadi ya wanajeshi Waukraine waliouawa hawatangazi (hii ni sawa pia Warusi hawataji namba halisi). Ukraine wanasema waliondoa warusi 12,000; Marekani wanahisi 3000-4000 ya hao waliuawa, wengine walijeruhiwa au kukamatwa.
 
Ungeandika tu Ukraine ikubali matakwa ya Urusi vita iishe kuliko kupendekeza wakae wakati una mlengo wako[emoji16]
 
Ungeandika tu Ukraine ikubali matakwa ya Urusi vita iishe kuliko kupendekeza wakae wakati una mlengo wako[emoji16]
Uko umeenda mbali... Haijalishi nini watakubaliana ila Raia kufa kwasababu ya Interest za kisiasa me sizan kama zina mashiko.

Haya basi tuseme wasikae chini kuzungumza. Nini hatma ya kupigana uko adi leo hii Raia takriban zaidi ya Mil. 2 sa hivi wana status ya "Ukimbizi"...
 

China blames NATO for pushing Russia-Ukraine tension to 'breaking point'

Moves by U.S.-led NATO have pushed tension between Russia and Ukraine to a "breaking point",
Chinese foreign ministry spokesman Zhao Lijian said on Wednesday
 
Mwisho nachojarib kukisema kwa makundi yote mawili... Wale wa Marekani wa Tandahimba na Warusi wa Tandale. Tuacheni ushabiki kwenye kupoteza uhai.

Hao wanaotapa tapa na kugeuka kua wakimbizi kwenye nchi jiran hawazifurahii hali hizo.

Sie tuliopo ndani mpaka tunapata mda wa kuchekelea nyuma ya Keyboard flani kafa au flan kapigwa vikwazo si jambo la maana ka tuna mawazo na akili za ubinadam.

Wanaoshabikia Ukraine kupigwa, tukumbuke wanaoathirika zaidi ni Raia na sio Viongozi wanaoshinda maofisini... Miundo mbinu ikiharibika wana athirika kwa kiasi kikubwa Raia wa kawaida ambae naamini angekuwa amepewa chaguzi ya kupigana au kutafuta suluhu angachagua suluhu.

Na kwa wale wanaoshabikia Urusi kupigwa vikwazo, tukumbuke anayeumia sio Putin anayeshinda Ofisin kutoa Amri. Wanaoathirika zaidi ni Raia wa kirusi ambao nahisi ata wao ungewauliza kati ya kuipiga ukraine au kutafuta suluhu ya mazungumzo wangechagua suluhu ya mazungumzo.

Kinachoumiza au kuniumiza binafs ni kwanini Raia wa kawaida ndo anakuwa wa kupokea "Consequences" zinazozalishwa na maamuzo ya watu wachache tunaowaita viongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…