Mpole au anajua tafsfiri halisi ya vita? Hapa tu kwa anachokifanya dunia ipo katika hatari ya vita vya dunia. Kinachoendelea sasa sisi kwetu inaweza kuwa ushabiki ila hatari kwa nchi zetu hizi za kumtaka musk afungue kwanza ofisi ndo afunge mitambo ni kubwa sana. Hapa tuombe China asiingie front direct akamwaga petrol kwenye hii sigara iliyotupwa ndani ya nyumba ya nyasi. Busara za viongozi wa nchi kubwa zinaamua fate ya binadamu wengi duniani, lets hope hakuna red line itakayovukwa sababu Tanganyika hatuna hata reserve ya mafuta na petroli. Sijui vyakula vitasafirishwa vipi kutoka huko mashambani kuja mijini.
Nataka kujazia hapa, ni kuwa mrusi anaiangalia kesho yake Kwa jicho Kali kuliko Leo yetu,
Hivi umejiuliza baada ya vita na urusi akashinda nini kitafata???, Nani atakuwa kinara wa dunia??
Ukitazama Kwa haraka haraka unaweza sema mchina na uchumi wake Ila ninachokiona japo urusi Hana uchumi mkubwa lakini anaushawishi mkubwa kuliko uchina,
Taabu ya mchina ni mjanja mjanja Fulani hivi yaani ukijichanganya anakuibia tofauti na urusi,
Mrusi kwenye vita hii anajitengenezea CV kuanzia nguvu ya kijeshi, kuaminika Kwa watu na ushawishi wake
Putin anapigana Vita Ukraine na inaghalimu maisha ya Askari wake Sana Kwa kuwa yeye anapigana na adui huku akikwepa Kwa gharama yeyote kuua raia wasio na hatua,
Hivi umejiuliza kama mrusi angesema asiuze gas kabisa hapo ulaya watu wangapi wangekufa na baridi????, Na watu hao hawana hatia maana maandamano yanathibitisha kuwa maamuzi ya nchi za ulaya ni ya wanasiasa na Siyo raia, na kama angefunga gas wangekufa raia na Siyo walengwa ambao ni wanasiasa,
Hivi unafikiria kwanini urusi alikubali Nagano iliyopo Ukraine ikauzwe ulaya maana urusi alijua watakaoumia ni raia,
Na mpaka sasa kama urusi atashinda Vita atakubalika hadi kwenye nchi za ulaya na kumfanya awe kiongozi Bora wa dunia na akiongea kitu dunia itasikiliza
Lakini pata picha dunia iongozwe na uchina au Korea kaskazini 😂😂😂😂😂 sipati picha kitakachotokea maana mchina ni mwizi balaa,
Kwa hiyo lengo kuu la urusi kuendesha operation hii kibinadamu zaidi ni kujiandaa dunia kumpokea na kumkubali mrusi kama kiongozi wa dunia