Ginner
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 1,576
- 2,227
Hongera chief...you seem to be very informed kwenye hii field..uko vizuri tuendelee na mjadala. Nitajibu hoja chache na kukaa pembeni kabla wadau hawaja tuattack kwa kutoka nje ya dhima kuu ya huu uzi.. kujua mkong'oto unaoendelea kule Ukraine.Typo ni kawaida wasio na hoja ndio huikomalia, nimekukosoa hapo naona kama autocorrect yako umeikaririsha kimakosa inarudia hivohivo.
Hakuna sehemu nimesema Urusi ilimtapeli Mhindi, ni kwamba Mhindi aliona capabilities zilizotajwa kwenye makaratasi sio hizo zinazojitokeza kwenye development. Mpaka leo Su-57 haina injini yake ya Izdeliye 30 inatumia AL-41F1 injini ya Flanker. Sasa injini hamna kisha mnaleta mbwembwe humu mnasema ndege ni superior. Hamjui stealth jet inahitaji injini yake maalum?
Na kwenye tukio la pale airbase umeongea vizuri sana, tatizo sio kuona ndege tatizo ni kuifanyia engagement. Russia inazo radars zinazoweza ona F-35 ikiwa almost 60km (data rasmi ni za siri ila kwa muda mrefu nimekuwa nikisoma hii claim). Hapo ni kulingana na radar cross section ya F-35 ambayo inasemekana ni kubwa kidogo kuliko F-22 ila ndogo maradufu kuliko Su-57.
Umemsema kunguru ila bado mkubwa huyo, ujue kuna radar zina uwezo wa kutambua matone ya maji angani. Tatizo searching radar na engagement radar ni tofauti kwenye wavelength na frequency. Kwahiyo unaiona F-35 na ground based radar ikiwa within 60km wakati yenyewe ina stand off missiles za range ya 100km+ sasa utaifanyaje?
F-35 kwa ukubwa wake kwenye radar inakuwa inazidiwa na kimpira cha tennis, ukirusha kile kimpira angani na F-35 ikapita hapo kitaonekana kuliko yenyewe. Uwezo wa radar unakuja kwenye processing hapo ni kompyuta ambazo Russia huwa yuko nyuma siku zote.
Unaiona ni target angani ila huna engagement radar ya kutoa guide accurately matokeo yake unafyatua missiles ovyo zinalipuka mita nyingi mbali na target, unatumia mbinu ya Urusi ya siku zote ya kutuma salvo unakuwa depleted with interceptors.
Kwanza hayo yote ya nini wakati AEW za Marekani zinasimama hundreds of km away zinascan radar emissions kisha 4th gen. fighters zinakuja na HARM missiles zinaondoa AD systems. Na bado kuna successor wa HARM ni AARGM yenye range kubwa zaidi na software nzuri. Kazi ya HARM si umeiona Ukraine? Sasa hao hawana ndege za kuitumia ipasavyo na wamepewa vikombora kidogo waringishie.
The indians withdrawal from the program Was made pre maturely. Ofcourse na demands zao zilikuwa nyingi sana as we know the Indians. Wangesubiri mpka prototype itoke na iwe tested ndipo wafanye maamuzi.
Kwa technology ya sasa ambayo dunia inapunguza manned aircrafts, wao the indians wanataka kuwa na two seaters version, mbali na iyo wanataka the aircraft iwe capable kutumia indian made missiles na kucommunicate na other indian made aircrafts ambazo in reality zinatumia architect tofauti kabisa kimuundo hata na kimfumo.
Mrusi ni heri amliamua kuachana nao, maana bila hivyo hii project ingekuwa na delays nyingi ambazo hazina maana mradi tu kumfurahisha mhindi. Atengeneze yake itakayoendana na mahitaji yake.
Issue ya engine iko very challenging. Ni lazma uchague moja, kati ya manuvability au stealthy.
Hapa mmrekani kwa f22 aliamua kuchagua stealthy ..akaunda f22 ambayo kujigeuza angani ni kizungumkuti kwa vile engine nozzles zake can only flip up and down.
Mrusi hesabu zake ziko tofauti, anahitaji stealthy ngoma ikiwa inakuja kwa mbele, ikisha kutungua hata ukiona signature kupitia engine hana shida, so ame balance stealthy kwa namna moja na manuvability kwa upande mwingine.
Hii engine ya flaker aliotupia humo ina 3D vectoring. Nozzles zake zinayumbishwa kuelekea nyuzi zote 360. Imeipa hii chuma manuvability isiyo ya kawaida. Inaweza hata kwepa missile ikija ovyo ovyo. So far inafanya kazi vizuri sana tu, mean while sasa akiwa jikoni kuunga engine ambayo itaachieve both, manuvability pamoja stealth at the same time.
This takes time, muhindi hakuwa na subira. Mwache aende.
Umezungumzia AEW za mmarekani kukusanya radar signals na kutuma anti radiation kuzimaliza. Chief, ujue tu kwamba in missiles technology Mrusi yuko mbali sana. Uwezo wa kuzishusha izi AEW za mmarekani hata zikiwa kwenye base zake pale florida anao, wala hata subiri mpaka zisogee karibu na mpaka wake kukusanya izo data. Na hiyo ndio sababu kwanini marekani hataki kuingia face to face na huyu jamaa.