Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Waukraine wanataja vifaru 3200 hivi walioharibu au kukamata. Inawezekana hii ni namba ya juu. Waingereza hawakubali kadirio hilo. Tovuti ya Oryx inaonyesha picha za vifaru 1800 vya Kirusi ambavyo viliharibika au kukamatwa na jeshi la Ukraine.
Ubora wa vifaru tunaweza kujadiliana, tofauti ziko hasa kiwango cha usalama kwa ajili ya askari ndani yake, vifaa vya darubini vya kulenga gizani na kwa umbali mkubwa, uwezo wa kifaru kupiga wakati wa mwendo na uwezo wa kutumia grened tofauti na kasi ya moto.
Hii ni upande mmoja tu. Upande mwingine ni ubora wa mafunzo wa askari ndani ya kifaru, na uwezo wa uongozi unaotuma kifaru pamoja na au bila ulinzi wa askari miguu. Leopard za Uturuki zilipotea huko Syria kwa sababu Waturuki hawakufuata utaratibu . . .
Menginevyo: kimsingi inawezekana kuharibu kila kifaru.
 
The transition into a multipolar, fragmented and contested world has happened more quickly and definitively than anticipated. - UK Goverment
 
Hahahah waendelee kukaza ubongo, walete hizo Leopard na Abrahm Tanks tunazisubiria kwa hamu ili kuwaonesha mfano kuwa Russia is number 1 in Missile Technology!
 
Mapema sana ila WANATO WA BUZA wataendelea kukaza ubongo 🤣🤣🤣
 
Muajemi .....yeye ni kuingia maabara na kutoa copy za leopard tanks, juvelin mpaka kieleweke


Hapa NATO wamekamatwa .....walipeleka silaha ....zinakamatwa na kutolewa photocopy wasipopeleka ..... zelensky anapoteza then atawalipua Kwa kumuacha idle
 
Lete iyo picha ya vifaru 1800 vya Urusi unavyosema sijui vimepigwa picha ili nasiso tuvione[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu tatizo watu wengi wao huamini kila habari inayotolewa na vyombo vya habari vya west.Hii uliyoielezea ndiyo hasa ilivyokuwa kwenye CUBA MISSILE CRISIS.Hautosikia western media yeyote ikielezea ya Kwamba USA walishurutishwa na wakakubaliana na masharti karibia yote.
 
Wamebaki mapumbu wazi ndio akili zimeanza kuwarudia. Kwa taarifa yake tu China hawezi kubali Russia adondoshwe na hata silaha atapewa akihitaji ili kusudi dunia iendelee kuwa salama. Hamna nchi inaweza mkoromea Marekani isipokuwa Urusi tu
 
German ilkuaga ile ya Hitler

Hii ya sahv ni mdebwedo sana
Zile kelele za kuteketeza silaha zao za maangamizi na kupunguza silaha mkakati za Hitler baada ya ww2 kwa maelekezo ya USA kupitia kivuli cha UN imewaacha weupe kabisa na waoga mno.

sahv german hawana ushawishi na hawezi kumvimbia yeyote pale EU,west au duniani.
Kwa uaoga wamegeuka chawa wa USA.

Kusingekua kuanguka kwa Hitler
German ingekua vzur sn kuliko hata China,

Maana kipind Cha Hitler walkua na silaha za hatari, na kipind Cha Ww2 baada ya kuwatwanga France, Poland na anakinukisha ile mbaya kule Russia uku England ya Churchill ikiwa hoi Sana kijeshi wanabweka TU.

Akatangaza hadharani kabisa Vita na USA baada ya USA kumzingua mshirika wake wa karibu JAPAN.

Hitler alisema wazi kua kituo kinachofata baada ya kumalizana na Russia Ni USA na akawaambia kabisa kikosi Cha nyuklia na icbm kijiandae.

Isingekua winter na ubora wa jeshi la urusi,
Ile German ya Hitler sahv tungekua tunaiongea german tofauti kabisa kijeshi.
 
Lete iyo picha ya vifaru 1800 vya Urusi unavyosema sijui vimepigwa picha ili nasiso tuvione[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu hujui kutafuta habari kwenye intaneti?? Hata kutumia google??
BAsi ona hapa: Attack On Europe: Documenting Russian Equipment Losses During The 2022 Russian Invasion Of Ukraine
HAo wa Oryx wanaorodhesha pekee vifaa (vifaru, ndege...) vilivyothibitishwa kwa picha. Kila kitu kina picha yake, bofya tu!

kwa jumla wamehesabu vifaa vya Kirusi vilivyoharibika, au kukamatwa na Ukraine :

Tanks (1831, of which destroyed: 1086, damaged: 92, abandoned: 103, captured: 550) MFANO:​


Armoured Fighting Vehicles (805, of which destroyed: 501, damaged: 13, abandoned: 28, captured: 263) MFANO:

Infantry Fighting Vehicles (2192, of which destroyed: 1405, damaged: 65, abandoned: 117, captured: 605) MFANO:

Armoured Personnel Carriers (304, of which destroyed: 189, damaged: 6, abandoned: 12, captured: 97) MFANO:


Jisomee mwenyewe jinsi wanavyotambua picha hizi na kuzitofautisha, maelezo yanapatikana kwenye tovuti.
 
Mkuu kama Hitler angeshinda, ukoloni ya Ujerumani ungerudi Tanganyika (na sehemu nyingine za Afrika). Wewe ungetembea na kitambulisho kinachosema ama "nusu mtu" au "nusu sokwe"; maana hii ni jinsi Hitler na wenzake walivyoona Waafrika. Labda ungepata nafasi kufanya kazi ya kufagia barabara za Ujerumani (ingawa hapo walikuwa na mipango kutumia zaidi Warusi), ila kwa masharti uhasiwe kwanza....
 

Russia alilenga kuparamia kainchi kajirani yakamkuta, amepokea za uso hadi aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…