mohamedidrisa789
JF-Expert Member
- Jun 20, 2015
- 5,615
- 23,751
Kwanza unatakiwa kujua kifaa kikifanyiwa Upgrade basi uwa kinakuwa na ubora mwingine.Mkuu bila shaka wewe u jenerali mkubwa na sisi sote tunasubiri kitabu chako unapoeleza siri za uongozi. Mfano siri ya kutuma vifaaa vingi visivyo na uwezo uwanjani kwanza ili viharibike. Na pia askari wenye mafunzo na utaalamu wa kuendesha vifaru kwanza wafe, ila baada kuharibika kwa vifaru 1000, 2000, elfu ngapi?) utatoa silaha zako nzuri zitakazofyeka maadui.
Utaeleza pia kwa nini unaleta T90 chache tu (bila shaka una akiba kubwa ianyofichwa bado) na badala yake unatafuta T62 zako zisizoliwa na kutu bado na kuzituma uwanjani.
Ilhali sisi tulio wengi hatujaelewa genius hiyo bado, tafadhali utuelimishe!!!
Marekani wanatumia Abram tank.je ! unajua Abram tank ilitengenezwa mwaka gani.ni tank ya toka miaka ya 70 ila Marekani kaifanyia Upgrade.kwa iyo kama unadharau Upgrade ya T-72, T-80 na T-64 basi unatakiwa udharau n a Abram tank.
Kwa iyo futa kauli yako ya kusema Urusi anapeleka tank chakafu na zisizo na ubora