1. Hoja yangu ni kwamba kama hizo media 'unazoziita huru' za magharibi zinaweza kupata idadi ya upotevu wa silaha za Urusi kwa nini wasipate taarifa hizohizo pia kwa upande wa ukraine!? Unasema "Ukraine inajitahidi kuficha" ina maana Urusi yeye hafichi!? Kwa hiyo tukubaliane Urusi yuko na uwazi zaidi kuliko ukraine!?
Unataka kutuambia West wanaweza kukosa taarifa zinazomhusu mshirika wao (Ukraine) badala yake wakawa na taarifa za hasimu wao Mrusi!? Hoja bado inabaki pale pale iko wapi taarifa ya Oryx inayoonesha idadi ya vifaru vya Ukraine vilivyoangamizwa vitani mpk sasa!! Wametupa kwa upande wa Urusi ni vifaru elf mia nane watupe na kwa upande wa ukraine. Kama hawatoi basi kuna kitu wanakificha kuhusu upande huo.
2. Sijaiona taarifa kamili ya IISS ila nimeona wamenukuliwa kwenye chapisho la WSJ. Yaani kwenye chapisho linalohusu upotevu wa vifaru vya Urusi WSJ wamenukuu data za Oryx na kuhusu vifaru vya Ukraine WSJ wamewanukuu IISS (vyanzo viwili tofauti).
Nukuu yenyewe hii hapa
"Ukrainian losses have been less well-documented. The IISS estimates between 450 and 700 Ukrainian tank losses, leaving about 950 operational, according to the report"
Isome article hiyo kwenye link hii kma unataka
Russia Likely Lost More Than Half of Its Tanks in Ukraine, Estimates Show.
Wanajitia aibu wanaposema Ukrainian losses have been less well documented. Hao wanaodocument losses za urusi inakuwaje hawadocument losses za Ukraine!? Kipi kinawashinda. Kwa hali ilivyo nilitegemea West wawe na access na taarifa za Ukraine kuliko urusi.
3. Kwa hiyo mashambulizi kutokea kila baada ya muda ndio dalili za kwamba makombora ya kisasa ni machache!? Shambulio la juzi ni majibu kwa ugaidi uliofanywa. Ina maana kama kusingekuwepo na tukio lile la ugaidi kusingekuwepo na shambulio lile la hypersonic.
4. Hujawaona wagner kwenye picha wamefika pale alipofika Zelensky mwaka jana Bakhmut. Hiyo ndio tafsiri ya vijiji baada ya vijiji baada ya miji baada ya majiji. Sio lazima tutaje majina