Asante, kuhusu GDP pekee unasema kweli, hapa Urusi ni nafasi ya 11 duniani (kwa sasa, tuone mwaka ujao baada ya vikwazo walivyojipatia). Ila hii ni pamoja na biashara ya gesi na mafuta, inayoweza kucheza sana (nimeona ni asilimia 60% ya GDP).
Upande wa Pato la Taifa GDP kwa kila raia unasema kweli pia, nchi ndogo ziko juu. lakini linganisha
chanzo hiki (inaunganisha data za IMF, Benki ya Dunia na UM) utaona Urusi kati ya nafasi 80-85 (nilikosea kuhusu 92, ilikuwa ya zamani), Marekani nafasi ya 6-10, Ufaransa 24-29. Pato kwa raia inasema kidogo kuhusu utajiri halisi ukiangalia ugawaji wa mali ndani ya nchi, ambayo huko Urusi ni kati ya nchi zenye tofauti kubwa sana kati ya matajiri wachache na maskini wengi (ni vibaya kote duniani, lakini hapa vibaya zaidi).
Ukiangalia si mapato bali mali, ninakuta hiyo: Wealth inequality is even more drastic, with the richest 10 percent of Russians owning 87 percent of the country's wealth, making it the most unequal of the world's major economies.
Yah ngoja tuone itakuaje...
Af kwanza em mpongeze kabla ya 24th Feb. 2022... Yani hajaingia Ukraine tear alikuwa na vikwazo zaidi ya 2700 mgongoni... Yani nafasi y pili nyuma ya Iran kwa vikwazo en still bado akaweza kua wa 11 kwa GDP.
Kingine kuhs gap la wenye nacho na waso kua nacho dah hilo tatizo kwenye dunia yetu bado majanga na sijui litaja pona lini mzee...
Hyo list Ukizichukua top three countries with highest wealth inequality Baada ya Russia ni number 2 ni USA kisha 3 ni China. Ila kabla ya 2018 aliyekua anaongoza ni Mmarekani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]...
Sasa ukiangalia wanapima vp hcho kitu n kupitia Market Values ya kampuni wahusika wanazomiliki ndani ya Stocks Markets kisha utajiri huo kulinganisha na watu wengine.
Sasa me na ww twajua fluctuations za Stocks market leo hii unaitwa billionaire kesho soko likiyumba unaitwa millionaire...
Je ni kipimo sahihi cha kumtambua mwenye nacho na asiekua nacho...?
Tanzania nzima ina Billionaire mmoja tu. Ambae kwa taarifa za uko nyuma kuna mahala nliwah kusoma ati anachukua takriban asilimia 3 ya GDP... (Ka n kweli au si kweli sina hakika sana)
Af mwisho kwenye vikwazo bado me nawasi wasi wa kitu kimoja... Naona kama USA anawaingiza chaka wenzie. Kuna picha ntakuwekea apo chini utaiona.
Apa nahisi anawaingiza chaka wenzie kwa mfano kama hivi... Kuna familia 4 huwa zinakula gengeni. Familia ya kwanza anakula gengeni ila ndani ana hazina ya chakula... Familia zingine zinakula gengeni ila hawana hazina ya chakula nyumbani.
Siku moja mwenye hazina ya chakula nyumbani akagombana na mwenye genge kisha akaanza kuwashawish na wenzie wasiende kula pale...
Hapo kama wakiacha kwenda kula pale gengeni mwenye genge ambae nae pia an hazina nyingi tu ya chakula ataathirika kwa kukosa mapato ya nje so atapunguza tu idadi ya chakula cha alichokuwa anapika but hatolala njaa...
Ile familia kati ya hizo nne mwenye hazina ya chakula ataanza kujipikia kwake kisha anakula... Yule aso kua na hazina ndo anabaki anatanga tanga...
Angalia kwe hyo 4to USA ni number 2 kwa kua natural resources nyingi... Hao wengine wako wapi? Maana ake ni wazee wa ku'import. Haraka haraka watatoboa?