Mkuu je umeishia matusi makali zaidi?
Unaendelea kuamini stori ambazo ni uwongo dhahiri???
Hakuna jenerali wa Kanada aliyekamatwa huko Mariupol.
Hujajaribu kufuatilia habari zake?
1) Trevor John Cadieu alikuwa luteni jenerali kwenye jeshi la Kanada hadi 2022. Mwezi wa Oktoba 2021 alishtakiwa kuhusika katika kashfa fulani
2) Alijiuzulu kwenye jeshi la Kanada tarehe 5 Aprili 2022 baada ya kunyimwa kupanda cheo
3) Mwezi ule wa Aprili 2022 aliondoka Kanada akaelekea Ukraine alipotaka kujitolea dhidi ya uvamizi wa Kirusi.
Sasa pamoja na propaganda yote uliyosambaza kuhusu Mariupol na Azovstal - hukumbuki kwamba wakati ule Mariupol imeshatekwa na Azovstal imeshaviringishwa pande zote na Warusi?
Lakini mgeni kutoka Kanada aliweza kutembea tu akipita mstari wa mapambano na kuingia kwenye mahandaki wa Azovstal??? Jamani, utoto gani hiyo?
Na ajabu - kama amekamatwa hakuna aliyemwonyesha, kuleta picha zake, . . . .
Kinyume chake amerudi Kanada anapoendelea kujitetea dhidi ya mashtaki ona
The Canadian military’s senior leadership was advised the sexual misconduct crisis was a battle for public opinion and those who raised concerns were ...
www.saltwire.com
Uwongo unaojulikana kitambo - kwa nini unaendelea kuusambaa (pia kuamini???)?