Mkuu naona unaongea kipropaganda mno...yaani nakuangalia unavyoandika mada hapa hauna tofauti na wanyonyaji wa kizungu wenye siasa za kuzunguka mbuyu wakati nia yake ni akupige tukio huku unajiona na unakubali kupigika.
Zimbabwe ilichapisha banknote nyingi kwakua ilipata vikwazo kutokana na kufukuza wakulima wa kizungu, uganda ilichapisha banknote nyingi kwasababu ilipoingia mgogoro na Tz kpnd cha Idd Amin basi nchi zilizokua zinaidhamin misaada zilikatisha misaada, Tz iligoma kuchapisha banknote nyingi ndio ponapona yake fedha haikuporomoka sana, ukilinganisha na sarafu ya Kenya(baada ya vita ya Ug ndio kipindi kenya inaiacha nyuma Tz kiuchumi)..hadi leo hii vita ile imesababisha shida katika chumi za nchi hizo mbili,
N.korea baada ya kuwekewa vikwazo uchumi uliyumba fedha yao haukuweza kujitosheleza S.korea iliwekizwa kuiangusha N.korea, raia walitegemea zaidi kilimo cha ndani ya nchi, kama mazao hayakutosha basi baadhi walikufa njaa na wengi waliugua utapiamlo, na aliejaribu kutoroka nchi alipatikana na madhara makubwa ikiwemo kifo pindi akikamatwa anatoroka,serikali iliendeshwa kwa njia zisizo halali km black market na hacking kwny mitandao, je wajua ilipokosekana sababu ya kuiangusha fedha ya libya ni nini kilitokea? Je Iraq? Je misri? Unakijua kinachoitesa sudani na akiba yao kubwa ya mafuta? Somalia? Je Nigeria?
Cuba ilipowekewa vikwazo raia wengi walikufa njaa, wengi walitorokea Miami..fedha ya nchi ilidorora..unajua kwanini Cuba inajulikana kwa kuwa na madaktari bingwa wanaotibu maeneo mengi duniani tena burebure....? Kama hujui sababu muache basi propaganda za kizungu humu..mtaelewa kwanini US ana vituo vya kijeshi karibu 65% ya nchi zote duniani hadi nchini kwako, lkn huyo urusi tunaeambiwa ni mbaya na hatari kwa dunia hana hata kituo cha kugawa kondom nchini kwako.