Mkuu suala la kuliangusha taifa la marekani na ulaya ni process ya muda mrefu si jambo la kukurupuka tu
China anaweza akafanya hivyo wakishirikiana na urusi, India na nchi za kiarabu swali la kujiuliza baada ya kufanya hivyo nini kitafata
Wao kutokana na mipango Yao kiuchumi wanaweza wakayumba kidogo wakakaa sawa, je baada ya kufanya hivyo nchi washirika kama nchi za kiafrika zitaweza kuendana namageuzi hayo????, Ukumbuke baada ya USA na Europe kuanguka super power atakuwa mchina na mrusi, je nchi ambazo anatakiwa kuziongoza zitakuwa katika Hali gani???
Hapa ndipo linapokuja hili suala la kuiondoa dola linahitajika lifanyike taratibu ili wale wateja wakubwa ambao ni serikali lazima ziwe na uwezo wa kujiendesha, yaani ni sawa na dukani kwako kuna jambazi kajichanganya na wateja inabidi ufanye juu chini umalize jambazi bila kuua wateja maana wakifa biashara itakufa maana mnunuzi alishafariki,
Kwa hiyo marekani na ulaya wanatakiwa kuanguka kiuchumi na kiushawishi bila kuleta madhara Kwa mataifa mengine duniani,
Hiyo hoja ndiyo sababu hii SMO kuendelea hadi Leo maana kupitia hii operation ndiyo njia ya kuizuangamiza west
Hebu jiulize kama hii operation mrusi angeimaliza ndani ya miezi mitatu ya mwanzoni Leo hii ufaransa kungekuwa na maandamano?, Mabenki marekani yangefirisika???, Leo hii mmarekani Angelia kumpigia mchina simu???, Saudi Arabia angeweza kumjibu shit marekani????, Tungeweza kuujua na kuifanyia kazi mfumo wa ulipaji kupitia mfumo wa urusi na uchina????
Hii yote imesababishwa na hii operation na jinsi muda unavyokwenda ndiyo urusi anaongeza ushawishi na marekani wanaloose, na dunia inafatilia kila hatua inayopiga hapo Ukraine, ni Kwa jinsi gani mrusi alivyo na huruma Kwa Ukraine na raia, ni Kwa kiwango gani anamdhalilisha mmarekani na kumfanya aonekane kinyago mbele ya jamii
Kuna mengi ya kuelezea kuhusu hii SMO kuchelewa kwake, kitendo cha mchina kukwepa ugomvi baada ya pelosi kwenda Taiwan, na marekani akaingia kichwa kichwa bila kujua athari zake baadae sasa hivi ndiyo kajua kumbe alikosea Ila anakomaa maana mkubwa hutakiwi kulia 😆😆😆😆
Kuna mengi Ila sina muda wa kuandika kutokana na pilika za kutafuta tonge