LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
1. Usiniite mimi mpendwa.

2. Nakushauri ujifunze geopolitics.

3. Nimekueleza usidhani humu JF watu ni mbumbumbu kama mtaani kwako. Endelea kuwadanganya hapo mtaani kwako but not here.

4. Jifunze historia na upate kuijua Russia. Eneo la nchi ya russia ni kubwa kuzidi China, USA, India combine. But population yake ni ndogo ukilinganisha na USA. Sasa unadhani Russia wanauhitaji wa eneo!?.

5. Russia ni nchi inayoongoza duniani kote kwa kuwa na madini mengi. Unafikiria Russia anahitaji nini Ukraine.

Nakushauri: NENDA SHULE KAJIFUNZE KWANZA NDIO UJE KUJADILIANA NA MIMI.
 
Unaweza ukaifafanua zaidi?
Russia wana mtindo wa kushambulia miundombinu na majengo na kuyavunja yote kwa makombora.

Mfano ni mji wa Volnovakha ambao ni kama hakupo kutokana na majnego mengi kuwa tambarare.

Ndo maana naona Russia akiazimia kufanya hivyo Kyiv inagawa hataweza kuuvunja mji wote utokana n amji huo kuwa ni wa kihistoria.
 
He here mrussi wa Naliendele naona umetubalishia na la Avatar umeweka ka ZERO kenu eeeh?Zero Ni failure....mtafeli njooni kambi la ushindi
Ndio maana kuna hobby nyingi jamani msitupangie hobby zenu wengine mnapenda football, Music, Swimming wengine tunapenda kuona milipuko ya mabomu na uharibifu yaani hapo nafsi zinapata furaha tena ngoja niagize popcorn saa mbili imekaribia niwashe TV
 
Sema urusi mafala sana si wapige bomu Moja matata sana (hata la nyuklia ) sawa tu Ili marekani na washirika waingilie nao wapigwe mabomu ya masafa marefu (kwao) waonje joto la vita na wao kdg
Wakipiga Nyuklia hata Belarus ambao ni washirika wao hawatapona, nyuklia itaathiri Northern Hemisphere yote...yaani mpaka London, Milan na Paris wataathirika

Msemaji wa mambo ya nje ya Urusi amesema watashinda vita hii na hawajafikiria bado kutumia Nuclear weapons

Pia kumbuka wao ndio mwenye stock kubwa zaidi ya Nuclear kwa Ulaya yote.
 
Ila wadau kuna jambo natafakari sipati jibu. Ni nini hasa Russia anachokitaka maana hii yakutaka wananchi waondoke kwenye Miji/ nchi yao ndio nashuhudia kwa Mara ya kwanza kwenye hii Dunia.
Mkuu hii sio vita bali ni operation ya kijeshi, ndio maana anatoa hata muda wa raia kuondoka...

Ndio maana wataalamu wa vita wanasema Urusi hakuna hata silaha moja ya hatari aliyoitumia Ukrane..

Fikiria toka jana jeshi la Urussilipo kilomita 25 kuingia katikati ya jiji la Kiev linasubiri amri tu... Sasa kwa muda huo si adui anakuwa ameshajipanga tayari.

Lakini jamaa wala hawana wasiwasi.
 
Attack helicopter ya jeshi la Russia Ka-52 ilivyoangamiza magari ya kijeshi ya Ukraine

tuwe wakweli, haya mahelcopter ya hatari, madege ya hatari, mavifaru ya hatari ya russia, hatujaona kama yamefanya kile tulichotarajia. hata ukraine yenyewe haijaona hilo. kwa masilaha hayo tulitegemea hadi sasaivi biashara iwe imeisha, na wanajeshi wa urusi wasingekufa wengi namna ile. nimeamini vita mbali na silaha ni ujasiri na nia ya kuamua tu kupigana. ukiamua kupigana hata ukiumia lakini adui lazima naye aumie.
 
Wewe hapo mamzese kwa bi nyau unamiliki simu gani!?
 
Mpendwa (!!!), ninakuita jinsi ninavyopenda. Menginevyo: Uliuliza kuhusu Putin, ulipata jibu la Putin mwenyewe, nukuu ya Kirusi - unataka nini zaidi?
Ukisema Putina ana eneo la kutosha - TUKO PAMOJA! NAKUBALI!! Ila jibu hilo umwambie Putin, si mimi.
Jibu lake hujapenda, sawa. Na mimi sipendi. Huyu ana njaa. Hivyo ndivyo maisha jinsi yalivyo.
Angalau hapa mtaani kwangu watu hawana matata kuangalia mawazo mbalimbali. Karibu kwetu!
 
Teh...teh...teh....Picha za setiliti zaongea zaidi (picha zilizochukuliwa kabla ya mashambulizi June 2021, na za baada ya mashambulizi March 9, 2022)

Miji inasawazishwa na kuwa kifusi

A1/ Kabla ya shambulizi mji wavutia


A2/ Baada ya shambulizi.



B1/ Kabla ya shambulizi mji wavutia



B2/ Baada ya mashambulizi



C1/ Kabla ya mashambulizi




C2/ Baada ya mashambulizi



 
mwambie akatafute history two advance
 
Putin malengo yake kama ni kumkamata na kumuua si angetumia watu tu badala ya kutia hasara .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…