MKUU NITAJARIBU KUKUJIBU KAMA IFUATAVYO;
USA na allies wake wanamuzidi vitu vingi sana NK tena kwa gepu kubwa sana iwe kijeshi, kiuchumi na kisiasa. Kitu pekee kinachomfanya NK kuwa mubabe wao ni umiliki wa nukes na mabomu ya masafa marefu (ICBM) halafu kuwa na kiongozi ambae haogopi kuyatumia hayo madude wenyewe wanamuita Don't care leader au crazy leader, haeleweki kama ukimkorofisha anaweza akayatumia au asiyatumie. Nisawa nawewe uanzishe ugomvi na mwehu alieshika mawe na rungu unadhani kipi kitatokea hata kama nawewe una mawe na rungu kama yeye [emoji23][emoji23]
IKUMBUKWE: huyu huyu dogo Kim Jong Un kiongozi wa ka nchi kadogo, 2018 alimtoa rais wa US (Trump) pale white house mpaka Singapore kwajili ya kwenda kumaliza tofauti zao baada ya dogo kumpiga biti trump kuwa atabonyeza kitufe cha bomu lakufika New york kilichopo mezani kwake[emoji23][emoji23]
KINGINE, tofauti ya North korea na nchi nyingine zinazo miliki madude hatari kama hayo i.e USA, Russia China, India, Israel, UK, France n.k ni moja tu nchi hizo zina viongozi wenye busara na smart wanaojua kutofautisha matumizi ya silaha, wanajua niwakati gani wa kutumia silaha za miaka 50 iliyopita na wakati gani wa kutumia silaha za kisasa pia wanajua wanachokupoteza tofauti na NK ambae anajua hana cha kupoteza sana.
Kama marais wangekuwa wanasajiliwa kama makocha, ukamchukua Putin ukampeleka kwenda kuongoza N.k halafu Kim akaenda Russia hii yenye kila aina ya silaha na mabomu hatari kuliko nchi yeyote ile duniani basi nakuhakikishia kuwa USA&NATO watamuamuru mpambe wao Ukraine asitishe hiyo Vita mara moja kabla Mr mashavu hajaanza kubonyeza batani za mabomu moja baada ya nyingine maana wanajua chizi kakabidhiwa rungu sasa kimachofuata nikichapo cha mbwa mtu bila kujali madhara ya hicho kichapo[emoji23][emoji23].
Mkuu kiufupi hata sisi na umasikini wetu huu siku tukiweza kutengeneza mabomu ya nukes yenye uwezo wa kutoka kambi ya jeshi ya Bulombola-kigoma hadi new york city au ulaya ndani ya dakika kadhaa halafu tukawa na kiongozi aliejizima data kama Kim Jong Un huyo USA na mashoga wake wataishia kubweka wakiwa mbali mno hata tukikamata mabalozi wao tukawachapa bakora na hata majirani wetu wataogopa kuzichapa nasisi.
HIZO NDO SABABU ZA KWANINI DOGO KIM NA N.KOREA YAKE WANAOGOPWA NA USA+MAJIRANI ZAO LICHA VURUGU ZAO ZA MABOMU UKANDA HUO.