Ni ile personality ya Kiongozi aliyepo Madarakani Korea kaskazini ambayo sio rafiki kwa michezo ya kisiasa. Ni sawa na kutaka mchezo wa kurushiana mawe ilhali unaishi kwenye nyumba ya Vioo.
Mara zote viongozi ambao huchokozwa sana ni wale wenye "think twice before acting" kwenye mind zao, wale ambao hukubal kujishusha inapobidi na kupuuza inapohitajika kama kupuuza uko kuna faida kuliko kutenda. Viongozi mithili ya akina Putin na Xi ila sio Kim.
Historia pia inachagiza hilo, NKorea ni taifa ambalo hadi kufika hapo walipo wamepitia mengi ambayo huwa hawataki kabisa yajirudie. Wamepitia kila aina ya unyonge na hawajapoa. Zaidi hawapendi kuonekana wanyonge, wana personality ambazo si rafiki kwa michezo ya kisiasa.
Tunaweza sema Kim ni Aina ya akina Medvedev, Kwa taarifa za nyuma ya Pazia yasemekana hata ile Maiden Revolution iliyofanyika 2014 Ukraine ilicheleweshwa hadi mwaka huo kwani ilitakiwa ifanyike kabla ila ikasubiriwa Rais aliyekuepo kati ya 2008 hadi 2012 atoke madarakani.
Ni nani aliyekua madarakani akati huo? hope unamjua, Je Kwanini ilikua hivyo? Nadhani Obama ana siri hiyo kwani anajua mwenyewe alicho kiona kwa Rais huyo enzi hizo alipokua madarakani.
Hivyo maelezo yanaweza kua mengi ila kwa ufupi tu Kiongozi aliye Madarakani hapo North Korea ana Personality ambayo sio Rafiki kwa Michezo ya kisiasa.