Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ukraine haiwezi tuma vidrone vidogo kama haka kapae kutoka uko kavuke mpaka mpaka Kremlin, hakana hiyo range. Either ni false flag au ni wahuni ndani ya Urusi.
Hicho kidrone hakina explosives za kuleta maafa hivyo ni kujisumbua kukituma kushambulia critical area, shambulizi kama la Kherson bridge ndio lilikuwa linamaanisha. Au hata la Moskva.

Putin halali Kremlin akiwa Moscow makazi yake ni Nova Ogaryovo
Hao wanataka wamuue Boss wao afu lawama ziende Ukraine.
 
lcimg-915ae325-0d72-44f9-a5b5-74884c8b71c6.png


Putin yupo leo kapewa picha nzima.

Hapo akipata "brief" yote kutoka kwa gavana wa mji wa Nizhny ambao upo katika jimbo la Novgorov.
 
Televisheni ya Poland imetoa Taarifa kuwa Zelensky Ataendelea kuwepo Poland kwa muda Mrefu zaidi ya Ilivyo Pangwa
Naona Wamechokoza Moto na wanajua kufuatacho
IMG_20230503_163705.jpg


Finnish TV: "Vladimir Zelensky will stay in Finland longer than planned."

What's wrong? After today's events, security guarantees cease to operate?
 
Na wamesema, majibu ya mapigo ya tukio hili kwa walioamua kufanya jambo hili wataamua ni wakati gani wayatoe. Nadhani wanataka wafanye Uchunguzi kwanza wamjue hasa aliyeamrisha ugaidi huu washughulikie yeye kama yeye !!!
====
Nadhani majibu yatakuwa tofauti sana na Yale yaliyotolewa baada ya kulipuliwa Daraja la Crimea.
Mimi Kwa mtazamo wangu Ninahisi kwenye tukio hili mrusi anahusika kivipi ni hivi,

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kuongezeka Kwa vitendo vya kichokozi kutoka marekani na ulaya dhidi ya uchina, na pia majirani wa uchina kuanza kuzalisha silaha huku wakijitangaza wanataka kujilinda dhidi ya uchina, kwanini uchina??

Katika mipango ya west Taifa lililokuwa tishio zaidi kwao ni urusi, ndiyo maana waliwekeza nguvu kubwa na mipango mkakati ili kuimaliza urusi halafu waje wamalizane na mchina, sasa walichokutana nacho ni tofauti na matarajio Yao lile anguko la kiuchumi la urusi walilolitegemea imekuwa kinyume chake, lakini ukiangalia uimara wa uchumi wa urusi mchina anaplay nafasi kubwa Sana, sasa baada ya kuona wameshindwa urusi wamehamia Kwa mchina maana wanajua kama mchina ataanguka basi litakuwa pigo Kwa ulimwengu Wote BRICS ambayo kila siku inapata nguvu na huku west wakiporomoka,

Sasa mrusi ili ndoto yake itimie anamuhitaji mchina ambaye ana Amani na uchumi mkubwa na wenye nguvu duniani, sasa Kwa namna yeyote Ile na Kwa gharama yeyote Ile mrusi ni lazima amlinde mchina ili kupata muungano wenye nguvu dhidi ya west na marekani,

Kwa hiyo mrusi anatakiwa amalizane na Ukraine ili akili yake itulie kwenye kujilinda uchina na nchi zote zenye nguvu za kiuchumi dhidi ya chokochoko za marekani, usishangae kampuni ya ulinzi ya Wagner wakapewa kazi ya ulinzi bila jeshi la uchina kuhusika, sasa ili Wagner waingie hapo basi wanahitaji vita ya Ukraine imalizike Kwanza,

Siku za karibu mrusi alionekana anapeleka silaha nzito na watu wakatabiri kuna mashambulizi makubwa mrusi amepanga kuyafanya baada ya muda kidogo hifadhi yake ya mafuta imepigwa akaanza kushusha kipondo Leo ikulu maana yake Yale matayarisho ndiyo yanaenda kufanyiwa kazi
 
Inawezekana basi ni false flag kwa malengo fulani ila sio mara ya kwanza kwa drone za Ukraine kushambulia ndani ya Urusi.
Sio mara ya kwanza ila hawatumii drone ndogo hizo FPV, wanatumia zile kubwakubwa kama moja ya Tupolev ni Soviet era. Mara zile walikuwa wanashambulia vyanzo vya nishati kama majibu baada ya wao kushambuliwa.
Hizi za jana FPV hata mtoto mdogo anainyanyua sasa range ya mamia ya km inatoa wapi na ikibeba explosives ndio inaenda umbali mfupi zaidi.

Watasema walikuwa ndani ya Russia na walitumwa, na watatoa ushahidi fake wa waliokamatwa. Ila hata kichaa hawezi panga kumshambulia mwenyekiti akashambulia ofisi usiku wakati mhusika ana nyumba ya kulala. Sembuse jeshi la nchi lipange shambulizi kwa kiongozi wa adui.

Putin anakolala kunajulikana sasa mjinga gani atake kumshambulia ofisini usiku. Kwani analala ofisini
 
Kwa kuwa wamemkosa Sasa ni zamu ya Zelle na hata akiwa Chini ya handaki atapandiwa huko huko kama walivyofanywa majemedari wake.
Hizi ni propaganda ambazo kuna wakakti inabidi uzichambue.

Kwa muda kama wiki mbili au tatui hivi Russia imetoa tahadhari kwamba huko angani kuna UAV zimezagaa.

Ni kweli Ukraine nao wana "saboteurs" ambao moja ya kazi zao ni hizo za kufanya uharibifu.

Jamaa wa FSB leo wamesema wamewakamata hao saboteurs na wanawashikilia kupata info zaidi.

Lakini kiukweli Ukraine haiwezi kumlenga raisi wa Russia moja kwa moja kwa malengo ya kumuua.

Na Russia nao hawawezi kumlenga raisi wa Ukraine Zelenski.

Ndo maana ya "rules of engagement" kwenye vita na hakuna kuvuka mstari mwekundu.

Ila kama taarifa hizi (Ukraine kutumia saboteurs kutumia UAV) ni za kweli basi sasa hivi twaweza kusema vita imefikia "tipping point".

Vinginevyo tuwe makini na propaganda war na information war.
 
Back
Top Bottom