Kwanini asijiondoe tu hapo Bakhmut aliache jeshi la Urusi pekee kuliko kuweka rehani maisha ya mamluki wake ?
Prigozhin alikuwa mfungwa hivyo haya mambo hayamtishi. Alafu Wagner ni njia yake ya kupata hela na lazima afuate serikali yake imemuagiza nini. Mambo ya vifo hata jeshi linapata.
Prigozhin ni kama Hemedti, Wagner ni kama Janjaweed na Putin ni kama al Bashir. Unatengeneza kundi lenye silaha ili liwe buffer kati yako na jeshi usijepinduliwa. Vilevile unatumia kundi hilo kufanyia vitu vitakuharibia CV au morale ya jeshi. Hili ufanikiwe lazima jeshi na hilo kundi visielewane hata makamanda wake wasipendane kiasi kwamba hawawezi shirikiana. Na wanakuwa na hofu kwa mpinzani hivyo akitaka kuchukua nchi wanakupigania maana akiwepo madarakani atawakomesha. Hata Interahamwe pale Rwanda waliua kwa sababu hizo hizo.
Tukirudi nyuma baada ya Black October constitutional crisis serikali ya Rais Boris Yeltsin iliamua kuipa silaha wizara ya dharura ili iwe buffer endapo jeshi litataka kuiondoa serikali maana bunge lilibaki kidogo tu. Kwanza wabunge walifungwa wakapigwa njaa. Picha ni mwaka 1993 kifaru kimepiga jengo la bunge, wanajeshi wa kuzuia ugaidi wakaingia. Bunge lilimuondoa Rais Yeltsin na kumchagua Makamu wake ndio awe Rais wa mpito. Ndio maana hadi leo Urusi haina cheo cha Makamu, Yeltsin alibadili katiba na ndio mwanzo wa kifo cha demokrasia ya Urusi
Baadae sana Putin akiwa Rais alimtoa Civil Engineer Sergei Shoigu atoke wizara ya dharura awe waziri wa ulinzi. Prigozhin alikuwa mpishi wa Putin miaka ya zamani ila akafungwa, baadae alitoka sasa sijui kama alimaliza kifungo. Ni mwaminifu kwa Putin hawajakutana njiani, picha ni Putin na Prigozhin mwaka 2011
Putin anawachezesha ngoma yeye anawaangalia tu wabishane wakimpigania boss. Kila mmoja anatetea nafasi yake ila ikitokea Putin anadondoka ghafla yasije yakajitokeza yaleyale ya Valentiy Beria wa NKVD dhidi ya kina Nikita walipomaliza mazishi ya Stalin. Beria alipewa summary execution wakiwa kwenye kikao tena akiwa anawafokea, kesi siku hiyohiyo na akawa executed palepale. Na waliosaidia hivyo ni Nikita pamoja na mkuu wa majeshi Marshall Zukhov ambaye jeshi lilikuwa na chuki sana na Beria