Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Vita ipo kwenye mji mdogo wa Inanivske.wakitoka hapo wanaelekea mji wa chasov.

Wagner wamepewa kazi ya kwenda kuchukua mji wa Seversk
 
Mkuu unachekesha. Unaleta tena ramani ambayo huelewi ukidai sehemu ya buluu ni "Poland".
Hapana, sehemu hiyo haionyeshi Poland.
Poland ni eneo la dola lililoanzishwa na kupanushwa na mtemi Mieszko I.
Miji yote (nukta kubwa nyeusi) ni miji na ngome zake, kuanzia Przemysl na Krakow kwenye kusini hadi Wolin na Gdansk kwenye kazkazini.
Mtoto wake Boleslaw alichuua cheo cha mfalme.
Unajaribu ubishi kuhusu mada ambayo huelewi, tena mada ambayo haisaidii chochote kuhusu maswali tunayojadili hapa.
Inaonekana unasikia haja ya kuonyesha "ukuu wa Urusi" tangu milele - ambayo kwanza si muhimu pili haiwezekani kwa sababu Urusi kama taifa ilitokea karne baada ya Poland. Nitajibu chini kwa nini "Rus" si "Urusi".
 
Mkuu kwanza sina maeneo yanayochukuliwa na mtu yeyote. Ukimaanisha Ukraine na Urusi, nimeona kwamba Jeshi la Urusi imefaulu tena kuchukua sentimita kadhaa huko Bakhmut baada ya kupoteza askari maelfu kwa miezi mingi.
Kasi ya ajabu.
 
yani kweli wewe ni chizi sasa kama unajua vita vinaendelea mariinka alafu unasema vimesimama si upunguwani huo
kifupi umeshindwa kutaja wapo sehem gani hapo bakhmut upinde wenzio
Wewe ndiye unaonekana tahahila,na sidhani kama itatokea huo upumbavu ukutoke kwa staili hii

Kuanzia Sasa nakupuuza maana nimekuona hamnazo kabisa [emoji1787]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
[emoji298]Russian forces have committed 88,517 war crimes and crimes of aggression in Ukraine since the start of Russia’s all-out war, Ukraine’s Prosecutor General’s Office reported on May 21.

Ukrainian law enforcement agencies also said that Russia’s war against Ukraine has killed at least 482 children and wounded at least 981 since Feb. 24, 2022.

Learn more: Prosecutor General’s Office records over 88,500 Russian war crimes, crimes of aggression in Ukraine

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Unaposema Rus na urusi ni tofauti unanishangaza sana.
Yaani ungesoma kidogo expansion ya Mongols na uhusiano na Rus hapo ungenielewa vizuri.
Mkuu ni vizuri sana ukishangaa ukiwa tayari kujifunza. Ndiyo, "Rus ya Kyiv" (Kievan Rus) na "Urusi" (Russia) ni vitu viwili tofauti katika historia.
Rus ni hao watu kutoka Uswidi waliofanya biashara na kuanzisha utawala kati ya Bahari Baltiki na Bahari Nyeusi. Walianzisha dola la Kyiv wakati mtemi wao aliamua kujiunga na Ukristo wa Kiorthodoksi akiamua kushikamana na Milki ya Bizanti (Roma ya Mashariki). Hii ilitokea mnamo mwaka 998 BK.
Soma: "One of the earliest written sources mentioning the people called Rus' (as Rhos) dates to 839 in the Annales Bertiniani. This chronicle identifies them as a Germanic tribe called the Swedes. According to the Kievan Rus' Primary Chronicle, compiled in about 1113, the Rus' were a group of Varangians, Norsemen who had relocated somewhere from the Baltic region (literally "from beyond the sea"), first to Northeastern Europe, then to the south where they created the medieval Kievan state" (Names of Rus', Russia and Ruthenia)

Urusi (Russia) ilitokea baada ya kuporomoka na kkugwiwa kwa Rus ya Kyiv. Kutoka sehemu mojawapo iliyoitwa Utemi wa Vladimir-Suzdal, ilitokea tena sehemu ndogo ambayo ilikuwa Utemi wa Moscow. Utemi huo uliendelea kuwa chanzo cha Urusi (Rossiya)
The modern name of Russia (Rossija) came into use in the 15th century
 
Mkuu kwanza sina maeneo yanayochukuliwa na mtu yeyote. Ukimaanisha Ukraine na Urusi, nimeona kwamba Jeshi la Urusi imefaulu tena kuchukua sentimita kadhaa huko Bakhmut baada ya kupoteza askari maelfu kwa miezi mingi.
Kasi ya ajabu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] maelfu wamepotea lakini eneo limechukuliwa sasa naomba nikuulize warusi wamekufa wengi sana hayo maeneo yamechukuliwa na mizimu au?
 
Mzee unaikuza sana Poland. Kati ya tawala zilizokuwa weak huko Ulaya kwa wakati wote ni Poland.

Unapomuongelea mtemi huyo wa kwanza kwanini unaruka kuongelea wake zake wawili:-

Doubravka of Bohemia - Czech
Oda of Haldensleben - German

Hawa wanawake ndio walimfanya akawa mkristo. Na hawa ndio walianzisha utawala huo. Maana yake hao Piast wapo chini ya utumwa miaka yote.

Kwahiyo niambie sasa huyo mtemi Mieszko I wazazi wake walikuwa kabila gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…