Mkuu kweli hali imekuwa vibaya hadi unamkimbilia Trump? Mwongo, mbakaji, mwizi na mlaghai aliyethibitishwa mara nyingi?? Pole.Oh, is it?? Hivi mwaka juzi raia wa Merikani walio fanya maandamano makubwa na baadhi yao kuvamia Bunge wakidai kwamba Biden hakushinda uchaguzi kihalali i.e waliiba kura za Trump vurugu zilikuwa kubwa sana kuna baadhi ya waadamanaji walipoteza maisha kwa kutetea demokrasia ya kweli, je, kama Urusi nayo ingejiingiza kwa ku-support maandamanaji kwa silaha na professional snippers na fedha kama US ilivyo fanya huko Ukraine kwa kuwa-support colour revolution nchini Merikani unafikiri kungetokea nini? au mnafikiri Warusi hawana uwezo wa ku-support makundi ya kuivuruga Merikani yenyewe.
Ndiyo naamini Putin ana uwezo wa kusaidia wapinzani anasemekana amejitahidi mara kadhaa kwa kuingilia chaguzi.
Sasa ni nani aliyepoteza uhai MArekani akitetea "demokrasia a kweli"?
Hakika Marekani hawahitaji silaha wala masnaipa waana wana vichaa wa aina hii wa kutosha.
Hao makundi ya Kirusi walioshambuliaBelgorod sijui vema. Nina picha kuhusu Wachechen walioko upande wa Ukraine. Ni wazalendo wanaotafuta njia za kumwondoa wakala wa Putin huko Grozny. Baada ya Chechnya kupata uhuru mnamo 1995, Putin alirudisha vita akaua bila huruma na kuharibu nchi ile ndogo na kumweka kadikteta huko...
Sipendi mauaji lakini siwezi kukana haki yao ya kujitetea.