Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]...dharau hizi mkuu ngoja wafia dini inayoitwa uraya au nato au marekani wakukute humu watakuua
[emoji1784][emoji1784][emoji36][emoji36][emoji28][emoji28][emoji23][emoji23][emoji849][emoji849][emoji40][emoji40][emoji1784][emoji1784][emoji23][emoji23][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]View attachment 2636520
 
Si kama ilivyokimbia NATO tuuu
Uzuri hakuna siku niliwahi kua sijitambui labda siku ntayokufa
RUSSIA hakuna taifa lakuifananisha nalo kwa huu upekee linaouonyesha kwa Dunia
Urusi nchini Afghanistan ilikua kama hivi Sasa Ukraine.
USSR peke yake,wakati upande wa Afghanistan ukisaidiwa na USA,UK na NATO yake,China,Soud Arabia,Iran, Pakistan,na nchi nyine kadhaa.

While the mujahideen were backed by various countries and organizations, the majority of their support came from Pakistan, the United States (as part of Operation Cyclone), the United Kingdom, China, Iran, and the Arab states of the Persian Gulf. Combat took place throughout the 1980s, mostly in the Afghan countryside.

Ndio utajua kama Urusi ni Supa pawa au sio Supa pawa.

Pia napenda kuweka kumbukumbu sawa kuwa,ussr haikushindwa wala kukimbia Afghanistan,Bali iliamua kuondoka kama ilivyoamua kuondoa majeshi yake Dunia nzima kwa kufuata mpango mpya wa mageuzi ya kiuchumi na kisiasa "Perestroika na Glasnost."
Uondokaji wa majeshi ya ussr nchi Afghanistan haukua uondokaji wa kukimbia wala kushindwa vita kama uondokaji wa USA alivyoondoka Vietnam na Afghanistan.usa waliondoka kwa kukimbia na kuteketeza baadhi ya silaha na kuacha baadhi ya wanajeshi wao.

Asikusumbue mtu,
Mkuu Bwana Utamu.
Wanajaribu kupindisha ukweli lkn ukweli hua haujifichi.













Je uondokaji huo ni uondokaji wa kukimbia au kushindwa vita?
Inasemekana Kuna sehemu walipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari.


Picha za hapo chini ni ndege na helkopta za wamarekani wakizidumbukiza bahari wakati wakikimbia mapigano baada ya kuzidiwa na WA Vietnam.
Wakaona helkopta na silaha nyingine,nadhani waliogopa huenda anachokifanya Leo hii Iran angeweza kukifanya china, zinaweza kukamatwa na wavietnam,wakaona ni Bora wazidumbukize baharini.
Nadhani juzi pale Afghanistan hawakupata bahari ya kufanya hivyo











Soja wa USA akiburuzwa mitaani somalia.hii ni baada ya kushindwa.
Na ndipo USA akakimbia Somalia.
Picha nyingine sio nzuri kwa heshima ya binadamu.

U.S Soldier dragged through Mogadishu​

Posted on March 10, 2010by S.Za.


 
Naombeni Msaada Bila Ushabiki wa upande wowote Hivi Hiyo Counteroffensive ninayoisikia ina lengo lipi na lini walisema inakuja na itafanikiwa?? Lakini kingine naona Ukraine amepata uthubutu kuipiga Urusi kwenye ardhi ya Urusi hii manake nn?? uweke mahaba pembeni ujibu kama hujui kaa kimya.
 
sasa mkuu unaomba kufafanuliwa maswali yako alafu unaweka na mikwara kama yote duhh
 
Ahiitaji wakati Ujerumani ipo kwenye recession ya kiuchumi.

Kumbuka hili ni Taifa lenye uchumi mkubwa zaidi Ulaya.

Sasa yafikirie Mataifa masikini ya Southern Europe yatakuwa katika hali gani?
 
Je unaweza ukafananisha uondokaji huo na uondokaji wa ussr huko afghanistan.uondokaji wa USA ulikua ni kumkumbia
Je unaweza kufananisha uondokaji wa ussr huko afghanisatani
na uondokaji wa USA huko Vietnam?
Uondokaji huo wa Supapawa USA ulikua ni uondokaji wa kushindwa,kuzidiwa,na kuamua kuokoa roho zao TU,vifaa vyote tupa baharini,na Kuna vifaa vingi TU viko maonesho huko Vietnam.
Hivyo hivyo ndivyo Supapawa alivyowakimbia Watalaban kaacha silaha ambazo nchi kubwa kama Nigeria na Ghana kwa pamoja hawana.
Sasa fananisha na mwamba Urusi alivyokua akiondoka afghanistan.ameondoka kwa heshima na maua na kupungia watu mikono,hapo hakuna kukimbia wala kushindwa vita.
 
Zelensky alipopewa tu HIMARS mji wa Mariopol ukaondoka.. Akaomba Abrams & Leopard 2 na akatamba hizo zitakuwa game changer na kubadili mwelekeo wa SMO. Baada ya kupatiwa alichokiomba zimeondoka na Bakhmut.

Kwa sasa anaomba ndege vita F-16 na makombora ya masafa marefu, na wafadhili wake wameahidi kumpatia kile alichoomba.. Kwa upande mwingine Russia wanazisubiri zitue tu ili KYIV wakaichukue na kuigawanya Ukraine vipande viwili.

Kila silaha na msaada anaopatiwa ZELENSKY unakuwa baraka kwa upande wa RUSSIA.
 
Ni comment nzuri,shida ni Kiswahili:usuruishi,mfururizo,hisijiunge,taaruki nk.
 
Inahitaji Gesi na Mafuta kutoka wapi?. Au havihitajiki tena, Kwa maana hawana matumizi navyo?.
 
Counteroffensive imefanyika mara kibao tu na wala hakuna jipya kwa sababu Warusi wapo macho na kila kitu Ukraine wakitaka kufanya wao wanakuwa washajua.

Bakhmut ilifanyika counteroffensive ila matokeo yake ikawa kuanguka kabisa kwa mji maana ubaya wa counteroffensive ikiferi basi mnakuwa mmepoteana kabisa.

Kuhusu kushambuliwa Urusi kwake ilo ni swala la kawaida sana maana hata magaidi wa Chechnia walikuwa wanafanya kama ivyo ila mwisho wa siku imebaki story.Urusi ni kubwa sana ndugu kwa iyo watu kujipenyeza kwenye mpaka na kufanya mashambulizi ya kuvizia ilo ni jambo la kawaida tu.
 
Ukikwepa gesi na mafuta ya Urusi basi jua muda wowote ule utatolea kwa maandamano.Nchi zote ya ulaya zilizoamua kuachana na mafuta ya Urusi kiukweli zinapitia kipindi kigumu sana.

Unawanunulisha wananchi wako mara 2 ya gharama ya mwanzo alafu unategemea nini zaidi ya watu kuandamana.
 
Inahitaji Gesi na Mafuta kutoka wapi?. Au havihitajiki tena, Kwa maana hawana matumizi navyo?.
Mkuu nchi zote za umoja wa Ulaya ziliamua kitambo (kabla ya Putin kuvamia 2022) kwamba wanataka kuachana na gesi na mafuta shauri ya hatari kwa tabianchi kutokana na kuchoma kabohidrati (=makaa, mafuta, gesi). Zote zilichelewa kuchukua hatua za lazima kuhamia nishati mbadala kama vile umemejua, umemeupepo, umememaji, uzalishaji wa hidrojeni. Mwaka 2021 nchi hizo zilifikia asilimia 20 nishati mbadala. Wengine waliendelea zaidi. Mfano nchi kama Uswidi (yenye tasnia kubwa ya feleji na mashine) tayari imefikia asilimia zaidi ya 60%.
Putin aliwasaidia sana kuchukua hatua za lazima kuendelea haraka zaidi.
Pamoja na hayo, nchi kama Hispania na Ureno hazikutumia gesi au mafuta ya Urusi kabisa kwa sababu zilitumia vyanzo vingine. Ujerumani ilikuwa ngumu sana kabla ya vita kwa sababu ilipata gesi ya Urusi kwa bei nafuu kidogo ilikosa pia mabandari kwa ajili ya gesi miminika kutoka Uarabuni au Marekani. lakini walijenga mabandari hayo haraka sana.
Hitimisho: nchi mbalimbali hazihitaji tena gesi ya Putin leo hii.
 
...dharau hizi mkuu ngoja wafia dini inayoitwa uraya au nato au marekani wakukute humu watakuua
Hakuna atakayemwua ila atasababisha watu wengi kushangaa jinsi gani ushamba wa aina hii inawezekana katika nchi inayofurahia kuvuka mapato ya USD 1000 kila mkazi kwa mwaka (=Tanzania) akijadili nchi yenye mapato ya USD 5000 kila mkazi kwa mwaka (=Moldova)
 
Wanaendesha viwanda vyao kutumia Nini?.

Na vipi uchumi wa German unaonekana kusinyaa ni sababu ya nini?.
 
Ahiitaji wakati Ujerumani ipo kwenye recession ya kiuchumi.

Kumbuka hili ni Taifa lenye uchumi mkubwa zaidi Ulaya.

Sasa yafikirie Mataifa masikini ya Southern Europe yatakuwa katika hali gani?
Mkuu si vizuri kuamini propaganda. Kwa mfano propaganda kwamba serikali za Ulaya zinapaswa kufuata maagizo kutoka US katika swali la Ukraine.
Serikali za Ulaya zilifuata matakwa ya wanachi wao wanaoona siasa ya Urusi inayolenga kubadilisha mipaka kwa mabavu ni hatari kwa kila nchi ya Ulaya.
Hapo ni sababu watu wa Ulaya (karibu kila nchi) wanasimama upande wa
  • misaada ya kiuchumi kwa Ukraine
  • misaada ya kijeshi kwa Ukraine
  • misaada kwa milioni za wakimbizi kutoka Ukraine
  • vikwazo dhidi ya Urusi na makampuni ya Urusi
Angalia kura za maoni zinazoendeshwa katika nchi za Ulaya, jibu ni hilohilo.
Wako wachache wasiokubali, wana uhuru wa kuandamana na kusema wanachotaka. Hapa unapata picha hizo zinazoonyeshwa hapa mara kwa mara na marafiki wa Putin.
 
Propaganda ndio hizi unazoleta wewe
Je, Uchumi wa Ujerumani unakuwa?
Je, haupo kwenye recession?
Sababu ni nini ilio ufanya ufike hapo?
Kama hili ndilo Taifa linaloongoza kwa Uchumi Ulaya, vipi Yale Mataifa masikini?

Kwa nini huamini Ujerumani ni Taifa huru?
Kama huru elezea kwa nini liweke vikwazo vinavyoliumiza lenyewe?
 
Mkuu jaribu kwa dakika 1 kusahau propaganda uliyolishwa halafu jiulize:
kwa nini asilimia kubwa sana ya watu wa Ulaya inasimama upande wa kutetea Ukraine na kuweka vizuizi dhidi ya Urusi - hata kama gharama zao zimepanda kutokana na vita hiyo??
Si vile kwamba USA inalazimisha serikali dhaifi. Ni kinyume kwamba serikali (ambazo zote zinachaguliwa kwa kura huru ambazo wala Urusi wala watu wa TZ wamewahi kuona) haziwezi kusimama dhidi ya matakwa ya raia. Wote wanaona Urusi kama hatari kwa Ulaya kwa sababu inatumia nguvu kwa kubadilisha mipaka na imevunja mikataba.
Jisomee hapa:

Utaona kuna tofauti katika msimamo. Mfano Wapoland na Wadenmark ambao wengo wanaona lazima Urusi inapaswa kushindwa. Tofauti Ujerumani ambako wengi wanasema "Urusi haiwezi kuruhusiwa kushinda, lakini kwa ajili ya amani labda maeneo kadhaa kama Krimea zibaki upande wa Urusi kama wakazi wake wanakubali".
 
Kwani mkuu Abrams zimeshaanza kutumika kwenye battle field?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…