The time will tell!
USA ANAWEZA TANGAZA VITA DIRECT NA RUSSIA. AU ZELENSKY ATAPINDULIWA KUEPUSHA AIBU YA KARNE.
USA atangaze vita direct na Urusi kwa ajili ya Ukraine na zelensky?
Maweee!
Hivi mnawachukuliaje wamarekani?
Kwamba ni vilaza sana?
Kwamba wako tayari miji Yao iangamie zaidi ya zilivyoangamia Hiroshima na Nagasaki?
Kwa sababu ya zelensky?
Zelensky wala hatapinduliwa na USA ,Bali USA itamuambia zelensky ajiuzulu TU na kwenda kuishi Marekani.
Nakuambia hivi kwa Karne hii hakuna vita kati ya USA NATO dhidi ya Urusi hakuna.
Labda Mkuu wangu nikupe tathmini ndogo TU.
USA akiingia maana yake NATO wameingia .
Kwa sababu sioni ujasiri wowote wa USA kuingia vitani na li nchi likubwa kama Li Urusi akiwa peke yake,ikiwa vita nyepesi TU kama Afghanistan,Syria,Libya Iraq USA alienda na washirika ,Leo li vita likubwa namna hii atapata wapi ujasiri huo?
NATO akiingia fahamu fika Uchina,Korea Kaskazini,Iran na baadhi ya nchi za kiarabu kama Syria zitakua upande wa Urusi,
Sasa jiulize ka china peke yake ikiamua kua upande wa Urusi Hali itakuaje?
na USA NATO wanafahamu fika Hali hii.
Hoja ni kwamba uchina,Iran na Noko zinajua fika kua Urusi ikipigwa wao ndio kituo kinachofuata.
Unajua vurugu yake,je yote hii ni sababu ya zelensky?
Sioni vita kubwa hapa mazee.