Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Naomba T14 Armata , HIMARS na kp kipanya44 mshirikiane kudadavua hii strategy mpya ya Russia. Kuhusu posho baada ya kazi, wala hata msijali. Mtapewa tanker 1 la mafuta na gesi kila mmoja.
Mkuu unfortunately sitoweza kushiriki kwenye uzi huu maana nikiandika replies zitakula muda wangu na nitahitajika kutoa mwendelezo wa kujibu. Kwa sasa niko mkoani ndani ndani huku mtandao unasumbua baadhi ya maeneo. Shughuli zangu zinanibana kupata muda wa kufuatilia vita inaendaje na tena nipate muda wa kuja hapa.
Vita haiishi hivi karibuni, mambo mengine yataendelea. Sitochangia kwa wiki kadhaa mpaka nirudi mjini.

NB: Kipindi hiki sitosoma notification yoyote inayohusiana na uzi huu. Mjadala mwema
 
Na wewe kwa akili zako umeamini??
 
The Security Service of Ukraine (SBU) reported on June 22 that it detained a Mykolaiv resident suspected of coordinating Russian fire and spying on the military.

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
[emoji298]President Volodymyr Zelensky said on June 22 that based on intelligence reports, Russia is considering a terrorist attack at the occupied Zaporizhzhia Nuclear Power Plant through radiation leakage[emoji298].

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 

Mkuu, mbona unachangia mijadala ambayo ipo kwenye majukwaa mengine.?

Au ukitaka kuchangia mjadala huu ndio network ya simu inakuwa inasumbua...?
 
Kwa upande wangu nilitegemea tu haya kutokea[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].



[emoji120] ila kila la kheri katika majukumu yako maana maisha inabidi yaendelee.umepata safari wakati mzuri sana maana wenzako wanapata tabu sana.

Tunakuombea urudi salama maana tuna maswali yetu mengi sana tumeandaa.ile misafara mirefu ya vifaa vilivyoteketezwa imeamia kwa wenzetu, sasa uje uchambue nayo maana ya Urusi ulikuwa unaichambua vizuri tu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe unavyofatilia vita unaona kuna hata dalili ya putin kurudi nyuma.achana kabisa na Warusi, hakuna nchi yoyote duniani iliyojiwekeza kijeshi kama Urusi.
Kinachoendelea Ukraine ni biashara tu mkuu, imekuwa mahala pa kila nchi kujaribu silaha zake, mwenye drones, tanks, missiles, war is about nothing, its a good way to launder dirty and bloody money, vita ya Afghan na USSR 1979 ilidumu miaka 10 na hakuna mshindi, US vita yake huko Afghan imedumu miaka zaidi ya 20,huku US ikipoteza Dolla billion zaidi ya 100 Kwa mwaka na maelfu ya askari, mwisho wake wameondoka.

Hii vita ya Ukraine itakaa muda mrefu, najaribu kutafakari tu, nimetafakari Kwa muda nikaacha ushabiki naona hii vita sivyo kama tunavyoichukulia.
 
Anayeumia ni Ukraine maana vita inapiganiwa Ukraine na sio Urusi wala sehemu nyingine.kwenye uwanja wa vita ndo uwa sehemu sahihi ya kutest silaha kama kweli inafanya kazi kwa usahihi.

Zelensk asipokubali kuwachia maeneo Warusi basi hali itakuwa mbaya zaidi huko mbeleni.
 
Mkuu izo data umezitoa wapi mbona umewapendelea sana USA.[emoji23][emoji23][emoji23]

Mpaka vita vya Afghanistan vinaisha USA alikuwa ametumia dollar trillion 2.(yani ni sawa na Tsh trillioni elfu 4000.

Bajeti ya Tanzania kwa miaka 200.

Ndo maana mizozo mingi siku izi Marekani anaogopa kujingiza kwa sababu anaona anazidi kuwa na madeni na uchumi wake kushuka chini.
 
Kuna MWANAJESHI wa Ukraine amechoma Bilblia kwakuw imeandikwa kirusi sasa wamepaniki hawa

Russia [emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji1218]
HADI KUFKa mwisho wa mwaka Ukraine itakuw imefutwa na kama vta kamili itaakuw imeanza au mrusi kuw mshinde


Zelekys must be eleminated[emoji88][emoji88]
 
Halafu kuna tajiri humo ndani ukisikia pesa makaratasi ndiyo hapo 😆😆😆😆😆😆
 
Russia pia inapoteza fedha na askari, huoni baada ya vita Ukraine inaweza kupewa support na misaada wakarudi vyema kiuchumi kwa Kasi? Kumbuka WWII West Germany na East Germany, West Germany walipata maendeleo na kufungua viwanda haraka kuliko East Germany iliyokuwa chini ya Russia kitu kilichopelekea wananchi toka East chini ya USSR kukimbilia West Germany chini ya US, UK na France, hapo ndipo USSR akatengeneza Berlin wall watu wasitoroke na kupunguza nguvu kazi.

Hizi nchi za magharibi zipo vizuri kiuchumi mkuu, unaweza shangaa baada ya vita kusimama wanarudi Kwa Kasi kiuchumi.
 
Mkuu rejea nimesema wamepigana zaidi ya miaka 20 na bajeti zaidi ya USD 100 Billion Kwa mwaka, rejea mkuu, sizungumzi kuipendelea US.
 
Hii vita ngumu sana, Russia anapewa upinzani mkali, mwisho kutabiri ni ngumu, nchi zaidi ya 40 ku support Ukraine si jambo rahisi.
 
hakuna nchi yoyote duniani iliyojiwekeza kijeshi kama Urusi.
Nina amplify to the maximum ili wasikie vizuri.
Russia is a real super power country in the world by real meaning of super power country.

NATO wanajua wazi kua Russia anawazidi kila kitu kwenye technology ya silaha za kivita na vita.
Hapo Ukraine ni uwanja wa majaribio zidi ya silaha za NATO VS Russia na hapo ukraine NATO washapeleka kila silaha yao ya hali ya juu kabisa na zote zimeishia kuharibiwa na Russia, hili hawataliweka wazi milele but wataishia kukimbia.
 
Russia haina uwezo wa kukabiliana na NATO, ukitoa silaha za nuclear.

NATO wapo vizuri, Russia inajitahidi sana kukabiliana nao.
Naikubali Russia kijeshi yupo vyema lakini si kuweza kukabiliana na nchi 31.
 
Hii vita ngumu sana, Russia anapewa upinzani mkali, mwisho kutabiri ni ngumu, nchi zaidi ya 40 ku support Ukraine si jambo rahisi.
Huijui vizuri Urusi wewe[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Izo nchi 40 mbona bado ndogo sana, inabidi ziongezeke nyingine 40 ndo hapo upinzani utakuwepo.

Mgogoro wa Syria ulikuwa kati ya (Assad, Putin- vs Nato, USA, Nchi za kiarabu).

Nafikiri jibu unalo ni nani aligeuka kuwa mshindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…