Ni mapema sana kusema counteroffensive imefeli.., lakini binafsi nilishindwa kuwaelewa Ukraine Pamoja na west kwa kutangaza ujio wa counteroffensive as if watatumia maroboti na mashine kuyafagia na kuwafukuza majeshi ya vamizi
Urusi pamoja na confidence na miguvu na milundo ya silaha aliyokuwa nayo mwanzoni mwa uvamizi ,bado hakudhubutu kuweka hadharani kwamba ataivamia Ukraine, badala yake alikana kabisa kwamba huo mpango Hana..,bila shaka alifanya hivi Ili kazi iwe rahis kwake, yahani amshtukze adui bila kujiandaa, ingawaje mwishowe malengo yake yaligonga mwamba,
Staki kuamini kwamba Ukraine na west Wana akili finyu kiasi Cha kutangaza ujio wa counteroffensive kama matangazo ya vifo, huenda pengine walikuwa na lengo lao nyuma ya pazia mbali na ukombozi wa ardhi iliyotwaliwa na wavamizi
Ninachoribu kukiona kwa mtazamo wangu ni kwamba,kwa kuwa hii vita Kuna watu hawataki iishe,basi walifanya Hivyo Ili urusi awekeze properties nyingi Ili kuzuia counteroffensive..,yahani urusi azidi kujikaanga kwa mafta yake kama kitimoto, lakini tusisahau kwamba Kuna watu wametenga bajeti ya kuendesha hii vita kwa takribani miaka mitano..,hii bajeti ingekuwa Haina maana kama Ukrainian counteroffensive ingeenda kwa spidi tuliyotarajia
Vinginevyo kama hayo mambo ni tofauti na mtazamo wangu hapo juu.., naweza kuwaona wote waliokuwa wakitangaza counteroffensive mithili ya matangazo ya vifo kama vilaza.., maana wamezidiwa hata akili na
kp kipanya44 kutoka nanjilinji,
Sent from my Infinix X660B using
JamiiForums mobile app