Yeah ni sahihi, kuna kitu kwenye uchumi kinaitwa arbitrage, ambayo inahusisha currency tatu kwenye market mbili tofauti.
You buy dollar kwenye market ambayo demand ya dolla iko chini, unaenda kuuza kwenye market ambayo demand ya dolla iko juu.
Ukifanikiwa kununua dola kwa rate ya 2500tshs hapa Tz, ukauza Kenya kwa rate ya 150Kshs na ukaja kuibadili ile Kshs hapa bongo kwa rate ya 1kshs to 22 Tshs...ile difference ndo faida.
Changamoto iliopo hapa ni kwenye upande bank charges. Ukitumia bank charges zilizopo, faida yote unawaachia banks. Ukisema uvushe pesa kwenye bag, uwe makini kutopewa kesi ya utakatishaji wa pesa