Mzee Putin angechutama tu, hii fedheha aliyoipata imempora hata ushawishi mkubwa kimataifa aliokuwa nao kabla ya Vita.
Mkuu huo ni mtazamo wako tu lakini kiuhalisia ni tofauti.
Vita ya Ukraine imewafumbua macho watu wengi na kujikuta wanatambua mengine yaliyo kuwa yameficha.
(1) kwanza watu wengi wamejua ya kuwa mataifa ya Magharibi yameshapoteza udhibiti wa kiuchumi duniani hasa baada ya kushindwa kuusambaratisha uchumi wa Urusi.
(2) pia ime isaidia Urusi kutafuta washirika wengine wa kibiashara hivyo kujikuta ana jitoa kwenye makucha ya nchi za Magharibi kiuchumi , kwa hiyo siku za usoni hata ile hofu aliyo kuwa nayo dhidi ya nchi za Magharibi inaenda kuisha hivyo kufanya chochote anacho taka,kwa sababu mara nyingi Urusi ilikuwa na hofu juu ya wamagharibi kwa sababu ya kuhofia uchumi wake lakini sasa tiyari ishajua kuwa kumbe uchumi wake unaweza kuendelea bila ya wagharibi.
(3) vita ya Ukraine imetusaidia kujua ya kuwa silaha za kimagharibi sio bora pamoja na kuwa ni za gharama kubwa kwa sababu kipindi cha mwanzo wa vita kipindi jeshi la Ukraine linatumia silaha za kirusi lilionekana kuwa na pafomans nzuri ,lakini jeshi hilo tangu lianze kutumia silaha za kimagharibi limekuwa na pafomans mbovu kabisa kwenye uwanja wa vita na Offensive inayo endelea ni ushahidi tosha kabisa sina haja ya kuelezea.
(5)Pia ilitufanya tukajua nguvu na umuhimu wa Urusi ndani ya dunia hii hasa baada ya dunia kuingia kwenye mtikisiko wa kiuchumi kwa sababu ya yy kuingia vitani.
(6)kumbuka Urusi ndo sababu ya Ufaransa kufurushwa Africa Magharibi na kwa sasa nchi hizo ziko chini ya ushawishi wa Urusi kitu ambacho kilikuwa hakifikiliwi kabla ya vita.
Hayo nimeeleza kwa ufupi tu, kuhusu yanayo endelea kwenye uwanja wa vita bila shaka umeuona ugumu wa vita kupitia Hamas na Israel.
Mlikuwa mnaiponda Urusi ya kuwa hajui kupigana badala yake anaharibu majengo lakini cha kushangaza Israel mpaka sasa hajatuonesha huo utaalamu wa kupigana bila kuvunja majengo zaidi ya kuuwa watu hovyo.
Mlikuwa mna taka Urusi aiteke Ukraine ndani ya siku 3 lakini leo ni siku ya 10 ya vita Israel bado inajishauri iwapo ipeleke au isipeleke wanajeshi ili kuidhibiti gaza ambayo haifiki hata robo ya Dar.
Vita sio lele mama.