Kaka samahani, history book yako kutoka wapi??
1) Ukraine haina silaha za kushambulia nchi kama Urusi, kinyume walikabidhi kwa hiari yao silaha za nyuklia kwa Urusi (iliyoahidi kuheshimu na kutunza mipaka ya Ukraine daima)
2. Je kati ya mipaka ya Urusi ni nchi ngapi za NATO? Mipaka ya Rusi inagusana kwenye 6 % za urefu wake na nchi za NATO. (kama Urusi isingechukua ardhi ya Finland na Ujerumani, ingekuwa sehemu ndogo zaidi; ni hapa tu KArelia inagusana kidogo na Norwei na Kaliningrag inapogusana na Poland na Lithuania, tzoite mbili hazikuw maeneo ya Kirusi kabla ya 1945
3. Vita za Urusi dhidi ya nchi nyingine:
a) Urusi imepanuka na kujenga milki ya koloni ambazo ziko nyingi hadi leo (ila ajabu Waafrika wengi hawaelewi): Siberia yoote ilivamiwa na kuchukuliwa kama makoloni ya Urusi katika karne zilizopita;
Nchi zote za Asia ya Kati (ambazo zimepata uhuru mwaka 1991) zilikuwa koloni za Urusi tangu karne ya 19; nchi za Kaukazi (Azerbaijan, Georgia, Chechnia, Armenia, Cherkesia) zilivamiwa katika karne ya 19 kwa damu nyingi;
1939 Urusi ilivamia Poland (pamoja na Ujerumani) na Finland;
1940 ilivamia Estonia, Latvia na Lithuania
1953 ilituma majeshi kukandamiza mapinduzi katika Ujerumani Mashariki
1956 ilituma jeshi kukandamiza uhuru wa Hungaria
1968 ilituma jeshi kukandamiza uhurui wa Chekoslovakia
1994/96 na 1999/2009 ilipiga vita kukomesha uhuru wa Chechnya
Si ajabu majirani wengi wana mashaka kuhusu Urusi na ahadi zake.