Yalishatumika yakapiga satellite ipi??? Yaani watengeneze wao, wajaribu wao na taarifa ya mafanikio waitoe wao wenyewe HALAFU MNAKUJA KUAMINI. Mimi kuhusu suala la kutengeneza sikatai ila ninachohoji ni EFFICIENCY YAKE.
Tuliaminishwa sana kuhusu defence systems za Urusi kuwa zinaona hadi nzi na mbu lakini leo hii tunashuhudia jinsi Ukraine anavyotuma Drones hadi Moscow na kupiga.
Sio kwa Russia tu lakini pia tuliaminishwa kuwa Israel ana defence system matata sana lakini mbona Hamas, Hizbullah na Iran wameweza kutuma makombora na mengi yakafika tena ya speed ya kawaida tu tofauti na yale ya hypersonic kama ya Mrusi. Ni kama tulivyoaminishwa kuhusu mfumo wa ulinzi wa USA pamoja na ndege zake za F16, F22rapter na F35 kuwa haviwezekaniki.
Hawa wakubwa wote wa dunia wana mambo mawili .1. Vitisho 2. Biashara
MIMI NITAAMINI SIKU NIKISIKIA SATELLITE IMEPIGWA NA KUHARIBIWA. NA NINAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA AKILI KUBWA YA KUCHANGANUA MAMBO. SIDANGANYWI kama wengi wenu humu. Halafu hii vita ya Ukraine IMEWAUMBUA WENGI SANA NA BADO HAMBADILIKI.
Tuliozaliwa zamani tunakumbuka mengi kwenye vita ya Iraq ambapo kama kawaida yetu wabongo ni kulipa sifa zisizostahili kombora la Scud
1.Mashine yeyote anayotengeneza mwanadamu in degree fulani ta inefficiency.
2.Utambue technologia inakua kwa kasi na warfare imebadirika sana. Ndo maana unaona hizo iefficiency unazoziona either kwa Israel au Urusi hata Marekani wenyewe.
3.Kama kweli unajisifia una -akili kubwa- ulipaswa kuwa umeishaona utofauti na jinsi technogia ilivyobadilika ghafla kwenye mambo ya kijeshi.
4.Kama kweli una akili ya kuchambua ilibidi uwe umeishajua kuwa wakati vita vya zamani infantry ndo ilikuwa kila kitu - Vita vya Ukraine vimeonesha umuhimu wa matumizi ya unmanned vehicles - drones pia na pinpoint strikes.
5.Inabidi ungekuwa umeishaona hayo mabadiriko ya ghafla na jinsi wazungu walivyoanza kuadapt - kwa kuanza kuwekeza instantlly kwenye drone technology - killer drones
6.Pia kama kweli akili yako ni kubwa ulipaswa ujue kuwa kuna ugumu sana wa kuzuia drones kulingana na size - vidogo..hata kwa risasi unavikosa - vingine vinapita chinichini - air defenses zinshindwa kuvidetect
7.Ulipaswa kuwa umeisha- appteciate njia za dharula ambazo nchi kubwa zimeanza kuchukua kujilinda na uvamizi wa drones - wengine wana - ant drones guns, wengine wanaweka nyavu n.k
8.Ulipaswa pia uelewe traditional airdefenses zilikua zidi ya much bigger threats and they cant jusy update kama vile wanakunywa maji, in 5 years to come watu watakuwa wameishapata walau airdefenses ambazo ziko effective kwa drones ndogo ambazo pia ni very deadly.
Ndo maana umeona drones zinatoka YEMEN mpaka Israel bila kuwa detected - sasa kwa akili yako hicho kitu kisikufanye ukadharau air defenses za Israel - utakuwa unacheza na kifo. The same kisa et drones zinatoboa zinapiga Urusi au Ukraine - Usithubutu kukaza fuvu et zile partriots za US na yale ma - pantsir, S- ...n.k za Warusi hayafanyi kazi - utakuwa bado akili yako sio kubwa...unapaswa uangalia zinatumwa drones ngapi na ngapi zinafanikiwa.
9.Kuhusu scud.Usifanye masihara na kitu chochote kinaitwa kombora..hata hako kabomu ka mkono tu - ni deadly - hata risasi moja tu ikifyatuliwa sio mchezo. Hivyo basi wewe akili yako kubwa ina - assess uwezo wa scud kwa kulinganisha vita ya 2003 kati ya US/NATO versus Iraq ambapo nguvu kubwa ilitumika kuharibu mitambo yote ya kurushia, kutengeneza, kuhifadhi, na wanayaoperate.- NENDA KAFUATILIE VITA KATI YA IRAQ NA IRAN ndo utaelewa how deadly they were na namna yalivoua maelfu ya watu.
10.Akili yako kubwa ni kama ya Tomaso.mpaka uguse uungue ndo utaamini kuwa kitu ni hatari ama la. Wazungu hawako hivyo - wanakuchunguza wanafichua uwezo wako kabla ili waangalie namna ya kukudhibiti - always wana mipango ya muda mrefu - Urusi haijawahi kutamka kuwa inauwezo wa kuzitungua setellites lkn nchi za magharibi ndo zimekuwa zikionya kuwa hao watu wanauwezo huo - hii ni kulingana na data wanazopata kuhusu majaribio ya siri wanayofanya n.k wakati wewe mwenye akili kubwa unasubiri mpaka satellite ishuke ndo uamini - wenye akili kubwa iriginal wameishaanza kuangalia alternative ya kufanya iwapo satellites zitatunguliwa n.k
Ukimya wa Israel na kukanusha kuwa hawana bomu la nyuklia kusiifanye akili yako kubwa ikaamini hivyo....na usisubiri mpaka siku walitumie ndo et ukubali