LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Naamini putin anachukua ushauri toka kwa watu wa usalama. Makamanda wakuu wa kijeshi na watu wengine, haswa wa nje ya russia. Kama china india na iran pia na ututuki.
 
Safari hii hadi Putin aombe poo
 
Hawatokuelewa ila ukweli ndio huo russia kuanguka ni LAZIMA na ni miaka michache kutokea sasa kwa wanaofuatilia kitu inaitwa eschatology wanaelewa. Russia itaanguka pamoja na Iran, Turkey, Libya, na nchi nyingi tu ambazo zipo upande wa russia.
Siku Russia ikianguka niite mbwa niko paleeeee nimekaa.
 
Hivi wewe unadhani marekani hana mbinu zakutosha katika hili.
Wewe unaamini kuwa amefanya tu maamuzi ya ghafla bila kushirikisha,
Izo ni mind games na zimeanza mda sanaa.
Hatutapeleka kitu flan na wanapeleka,hawatafanya kitu fulan na wanafanya.
Huo mpango ulikuwepo kitambo sana.
Ukiona marekani anaongelea jambonjua ameshalifanya
Kweli hazitawamaliza Russia ila lazima zifanye damage ,lazima askari watakufa na miundombinu.

Ishu kubwa zaidi ni raisi kusimama kusema jambo na halitimizi.
 
British naye karuhusu Ukraine atumie silaha zake za long range missiles kwenda Russia. Jana zimetumika za US
Hapo wanamlazimisha Putin afanye chochote halafu watasema Putin anaescalate.

Ni kama west wamedhamiria WW3 na wanamlazimisha Putin. Ikitokea hii watakaobaki watasimulia manake nusu ya dunia tunaweza kwenda na maji..
 
Alafu hata USA hawawazi, yani USA imeshavuka redline zote zilizowekwa na Putin na hakuna lolote alilofanya zaidi ya mikwara,
Sio mikwara,unaona nguvu aliyoipata Iran kwa siku za hivi karibuni ni matokeo ya kukiuka Red line za Putin.Defence capability ya IRAN imekuwa boosted sana kwa kupewa S400 na ndio maana uliona Israel ilibidi arushie makombora akiwa km 100 ndani ya IRAQ kwa kuhofia usalama wa ndege zake.Hata madhara ya shambulio yalikuwa madogo kwani asilimia kubwa ya makombora yalipanguliwa.Pia anampelekea Iran SU35 multi role stealth combat plane akimuongezea uwezo IRAN wa kuzichallenge F35 za Israel ambazo zimekuwa mwiba mchungu kwa nchi jirani.
 
Sio nyie mlisema hawataki vita na wanaogopa mno kifo, Leo imekuwaje mnasema wanalazimisha WW3
 
Inauma sana kiukweli sisi ambao tupo upande wake
Kitu gani kina kuuma?? Russia anazidi kuchukua maeneo huko Ukraine kwa kifupi anafanya vzuri..mimi sina wasiwasi kabisa na Putin,

,sababu ya nchi za west kuruhusu Ukraine atumie makombora ya masafa marefu kwenda Russia nahisi wataka kumlazimisha Russia abadilike aina yake na strategy zake upiganaji,they are testing something
 
Huyo jamaa kajaa ushabiki wa kipuuzi sana, anawaza miji ya ulaya na marekani kuchakazwa, lakini ubongo wake hauwazi kuwa miji ya Urusi pia ipo uchi, yaani ni vichekesho vitupu
Hivi wewe unaongea Nini.?
Unajua unachokiongea lkn?
Busara ya Putin sio udhaifu,najua kua unajua lkn hutaki kukubali kua Urusi inazo silaha na inaweza kuzifikisha katika nchi yoyote hapa duniani hasa nchi zote za NATO,je unafikiri ni Kwa Nini wanasita kufanya hivyo?
Unachokisema kuwa hata west wanaweza kupiga miji ya Urusi hiyo ndio sisi tunaiita WWIii kitu ambacho wengi hatutaki na hata wamarekani wenye akili safi kama akina Trump hawataki.
Wewe unadhani nchi kama Urusi inashindwa kuvurumisha makombora kwa west kwa sababu ya kuogopa?
Kuogopa Nini Sasa?
Watu wanaangalia na utu,lkn kama unafikiri ni burudani kama mlivyozoea sinema za akina Rambo wewe subiri waendelee kurusha makombora Yao ndani ya Urusi halafu unakuja kuona Nini matokeo yake.
Busara za Putin msizichukulie kama udhaifu.
 
Mimi sichambui kimahaba kama nyie. Tatizo lenu hamtaki mawazo yanayoshusha upande mnaoupenda.
Elewa tu kuwa Russia inaanguka
Sjui una Elimu gani but unaonyesha uko mtupu sana kichwani kuhusu hii vita,mtupu kichwani kuhusu Russia na historia yake,mtupu kichwani kuhusu NATO,yaani wewe ambae uko Tanzania unajua Russia ina anguka lakini marekani na washirika wake wasijue?

Yaani Putin na warussia wameshindwa kuliona hilo ila wewe kutoka nchi ambayo hata technolojia yakuokoa watu wake hawana unaona Russia inanguuka,VERY FUNNY
 
Safari hii hadi Putin aombe poo
Kwa sentensi hii naweza kujua uwezo wako wa kiakili na uwezo wako wa kufikiri.

Hivi tufanye wameshapiga mara mbili ndani ya Urusi,je wamefanikiwa kwa kiasi Gani kurudisha majimbo,wilaya,miji au vijiji vilivyochukuliwa na Urusi,ama majeshi ya Urusi huko Dombass yamerudiahwa nyuma kiasi Gani?
Je unafikiri mashambulio hayo yatapita bila majibu?
Jamani msiwe mnaandika vitu bila kushirikisha ubongo zenu.
Hii ni vita na vita ni piga nikupige.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…