Hizo silaha zimetumika hapo kabla wakumbuka daraja la Kerch lililipuliwa na bomu la Storm Shadow na hizo ATACMS zimetumika kupiga Crimea zikaharibu meli za kivita pale Sevastopol kiasi cha kuifanya Russia kuhamisha mali zote za kijeshi.
Hizo silaha ni ghali mno (ATCMS ni dola milioni 1.5 kwa kombora na Storm Shadow ni pauni milioni 2 kwa kila kombora soma hapa:
Atacms: What we know about missile system Ukraine could use to strike Russia ) ndo maana waliziweka akiba na zikiisha hizo hakutakuwa na zingine.
Isitoshe Russia ataendelea kuzidungua na huku akiendelea na SMO kama kawaida maana wamesema matumizi ya silaha hizo hayatabadili mwelekeo wa vita yaani Russia kuchukua maeneo zaidi.