LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mimi Maoni Huru ambae ni Lee Van Cliff zamani nasema wote mnaomlaumu Putin mtakuja kumsifu baadae na wote mnaodhani kushindwa mtakuja kumlaumu baadae.
Kwa kufuatilia habari nimesoma mahali Putin Yuko kwenye vikao na Viongozi wa ulinzi na usalama na wataalamu.
Nafuatilia vyombo vingine vya habari hapa.
 
Wakati huko urusi kwenyewe kukiendelea kuchakazwa

Huko pia kwenye battle field wanazidi kuchinjwa
 
Duh! Jamaa umekomaa kweli 🏃🏃🏃🏃
 
Atakaa vikao sana, lakini kuingia kwenye vita ya muda mrefu namna hii kwa kutegemea wingi wa askari, Putin alichemsha sana.
1. Amesababisha vifo vya warusi wengi sana.
2. Amesababisha vifo vya wa ukraine wengi sana.
3. Na sasa more than 100,000 North Koreans wameingizwa kwenye conveyor belt.
 
Kila mmoja Anamaoni yake
Lakin Lazima Mjue Vita ya Sasa Sio Kukurupuka kama Mnavyo Fikiria
Na sio lazima Ukipigwa lazima Ujibu Muda huo huo ili ionekane ww ni mwamba hapana.
Lazima mipango Ipangwe
Na Kwa karne ya sasa Nuklia Sio Rahisi kutumika Kwa Haraka Hivyo.
Ukrein Atapigwa tena Vibaya sana
Na Marekani Uk nao watapata Majibu yakuumizwa inaweza isiwe Urusi moja kwa moja
Bali wanaweza wakawa Huthi au Wengineo
Meli yeyote ya Us , Uk zikapewa moto na Silaha za Mrusi kupitia Hao Huthi
 
una tungo zuri unafaa kuwa mwalimu wa tungo
 
Mzee Baba kuwa mpole Putin ni zaid y mtu upande wa ujasusi wazungu wa Ulaya wameundiwa michuma chuma wakapewa maelezo ya uwongo mifano ipo wazi uko Telaviv kunawako moto bahari nyekundi tumeona yale matenga ya nyanya yalivyo fanywa. Kwaiyo Putin anawavuta waje kaawacha kwanza wajitutumu ili ulimwengu ujue mchokozi nani kisha haaaaa atawafuraisha na watacheka kweli kwenye mashimo ya foot6 tuupe muda heshima.
 
Mr. Lee Van Cliff, habari zs miaka ndugu yangu!

Unajua Russia anapigana proxy war against the USA directly.

Sababu kuu na maalumu ya SMO ilikuwa ni kuepuka kwa Russia kushambuliwa na western missile moja kwa moja kwenye ardhi yao. Lakini kwa sasa wanapiga moja kwa moja kwenye ardhi ya Russia.

Haya ni mawazo yetu tu tunachangia: Russia inabidi ifikirie tena upya au history will be written for them.
 
Putin kaishajichanganya kwa kuanza kufikiria kama USA & CO. Na nadhani wamempandikizia hizo fikra bila yeye kuelewa kwamba anacheza mziki wao.

Toka walipoanza kumsaidia Eukraine, USA & CO wamekuwa wakijifanya kumzuia EUKRAINE asipige ndani ya Rusia sababu hiyo itakuwa ni escalation, lakini pia wamekuwa wakidai wao sio washiriki wa hivyo vita hivyo hawatapeleka majeshi yao Ukraine.

Matokeo yake, Putin akashindwa kushambulia Misafara ya siraha ndani ya Poland, au iliyobebwa na vyombo vya usafiri vya USA & Co.

Sasa wanadai Kaescalate kwa kukodisha majeshi ya North Korea, hivyo na wao wanaruhusu apigwe nyumbani kwake.

Na yeye anaamini kaescalate yeye. of course yeye ndio mwanzilishi na yeye ndiye atayeamua vita iishe au isiishe.
 
Naona watu walitegemea kuwa na majibu usiku wa leo, but inawezekana hadi hii week inaisha kusiwe na retaliation, sababu huwezi kurupuka na kurusha missile hovyohovyo.
Russia watakuwa wanakusanya data na movement ya command center zinazo coordinate hizi attacks, lauching center, ammo concentration depot, Deployment and rotation point, radar and signal, Logistic and supply and vital energy zinazo support millitary operation.
Issue zio kujibu, ila ni hasara kwa kiwango gani unapeleka kwa adui ili kukata pumzi na uwezo wa kupambana frontline.

Ukraine na west wanategemea majibu within 4 days, ndio maana balozi nyingi zimefungwa hadi wiki ijayo, hii maana yake Ukraine na west wako on guard, radar and tracking pia ziko kwenye high alaert, sambamba na hayo pia watakuwa wamefanya relocation ya silaha muhimu na kuzificha. Nadhani mrusi anakusanya data ya silaha na makombora Ukraine waliyopkea, Expert waliotumika, lauching equipment, joint intelligency centers, depot na njia za usafirishaji ndio ajibu.
Usisahau ni gharama kubwa sana unatumia kuanzia equipment, resource, money na mind kuwa kwenye high alert
 
Unatuzingizia sisi tu Wahadzabe. Wahdazabe sisi tuna amisha yetu ya kijadi kabisa wala hatujishughulishi na yanayoendelea duniani na wala hatujui yanayoendelea nje ya maeneo tunayoyaona kwa macho yetu. Wanaojifanya kuijua dunia ni nyie Waswahili wa mijini.
 
Nonsense
 
Russia anauwezo wa kuifuta Marekani kwenye uso wa dunia kwa hiyo usiwaze Russia kupoteza hivi vita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…