Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 1,535
- 5,332
Naomba kutofautiana na wewe Kwa facts.Binafsi naona Russia kuizuia Ukraine isijiunge NATO Kisa issue za usalama si kweli maana Majirani wengi tu wa Russia ni NATO members. Issue kubwa ni bandari na Mali zilizoko kwenye hayo majimbo yaliyotekwa na Russia. Hata US na Rafiki zake wanaitaka Ukraine ili wapate hizo rasilimali ili wapunguze kama siyo kuachana Rasilimali za Urusi maana wakifanikiwa kiuchumi Urusi itapoteana Kwenye Export trade
Vita vya Ukraine kwa upande wa Urusi ni suala la ulinzi na usalama dhidi ya NATO.
Kabla ya vita (SMO) Miaka mingi nyuma Urusi waliisihi USA na NATO wasijitanue Eastward.
Lkn wakajitanua,Urusi ikawa na uvumilivu.
2014 kwa hila za NATO wakafanya mapinduzi nchini Ukraine Kwa kivuli Cha maandamano na kumtoa Yanukovic.
Urusi uvumilivu ukaanza kupungua wakaiteka Crimea.
Majimbo yenye raia wenye asili ya Urusi yakaona hayatendewi haki wakaanza harakati za kujitenga.
Ukraine Kwa kusaidiwa na NATO wakawa wanawapiga,Urusi ikaendelea kua mvumilivu.
Ukraine wakaingiza kwenye katiba Yao kusudio la kujiunga na NATO bila kujali hisia za Urusi kuhusu kuwepo NATO mipakani kwake.
Russia iligundua mipango ovu ya Ukraine na NATO iliyokua ikiendelea Kwa Siri nchini Ukraine,kama ujenzi wa makambi ya Siri ya mafunzo ya kijeshi,miundombinu ya kijeshi,ujasusi na silaha za sumu.
Kutokutekelezwa kwa makubaliano ya Minsk.
Mojawapo ni kuitaka Ukraine iwe nyutro.
Urusi ikaona heri nusu Shari kuliko Shari kamili.
Ukiangalia sababu zangu zote hapo juu hutaona kama uchumi unahusika na mzozo huu.