LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Naomba kutofautiana na wewe Kwa facts.
Vita vya Ukraine kwa upande wa Urusi ni suala la ulinzi na usalama dhidi ya NATO.
Kabla ya vita (SMO) Miaka mingi nyuma Urusi waliisihi USA na NATO wasijitanue Eastward.
Lkn wakajitanua,Urusi ikawa na uvumilivu.

2014 kwa hila za NATO wakafanya mapinduzi nchini Ukraine Kwa kivuli Cha maandamano na kumtoa Yanukovic.
Urusi uvumilivu ukaanza kupungua wakaiteka Crimea.

Majimbo yenye raia wenye asili ya Urusi yakaona hayatendewi haki wakaanza harakati za kujitenga.
Ukraine Kwa kusaidiwa na NATO wakawa wanawapiga,Urusi ikaendelea kua mvumilivu.

Ukraine wakaingiza kwenye katiba Yao kusudio la kujiunga na NATO bila kujali hisia za Urusi kuhusu kuwepo NATO mipakani kwake.

Russia iligundua mipango ovu ya Ukraine na NATO iliyokua ikiendelea Kwa Siri nchini Ukraine,kama ujenzi wa makambi ya Siri ya mafunzo ya kijeshi,miundombinu ya kijeshi,ujasusi na silaha za sumu.

Kutokutekelezwa kwa makubaliano ya Minsk.
Mojawapo ni kuitaka Ukraine iwe nyutro.

Urusi ikaona heri nusu Shari kuliko Shari kamili.

Ukiangalia sababu zangu zote hapo juu hutaona kama uchumi unahusika na mzozo huu.
 
Huko Kursk ni kiama!Sikia kauli za askari!

Ukraine’s exhausted troops in Russia told to cling on and wait for Trump​

“The situation is getting worse every day.”

“We don’t see the goal. Our land is not here.”

They speak of dire weather conditions and a chronic lack of sleep caused by Russia’s constant bombardment, which includes the use of terrifying, 3,000kg glide bombs.

They’re also in retreat
, with Russian forces gradually retaking territory.

“This trend will continue,” Pavlo wrote on 26 November. “It’s only a matter of time.”

Wanazidi kubadilika!

'Significant shift' from the PM as he talks about putting Ukraine in 'strongest position for negotiations'​

Sir Keir Starmer has now for the first time tonight said it was British policy to "put Ukraine in the strongest possible position for negotiations".

He wants Ukraine to be in a position of strength "so they can secure a just and lasting peace on their terms that guarantees their security, independence - and right to choose their own future" .

But make no mistake. This is a significant shift.

Usichokijua pengine ni kuwa ukraine ilikuwa inaandaliwa kuwa ngome ya nato ktk kuivuruga russia, hivyo ilipewa mafunzo na vifaa kabambe
Wengi hawafahamu kuwa mwaka 2021 Marekani / NATO walifanya mazoezi ya kijeshi pamoja na hilo Russia walikuwa wakiwaangalia tu.

Lakini tarehe 24 mwezi Februari Russia wakaamua waanze hii SMO ambayo malengo yake ni kuvunja uwezo wa kijeshi wa Ukraine na pia kuondoa "ideology" ya unazi.
 
Katika majirani wote wa Russia ni Ukraine tu ambaye akijiunga NATO atahatarisha usalama wa Russia? Mbona majirani zake wengine wamejiunga na hana habari nao?
 
Katika majirani wote wa Russia ni Ukraine tu ambaye akijiunga NATO atahatarisha usalama wa Russia? Mbona majirani zake wengine wamejiunga na hana habari nao?
Jitahidi sana kutafuta maarifa. Pia jiulize kwa nchi majirani zinazoizunguka nchi yako ya Tz ni ipi ina muhimu zaidi kwa Tz Kiusalama au hata Kiuchumi.
Pia jiulize ni kwanini Muungano wa Tanganyika na Znz una faida zaidi kwa Tanganyika.
 
Mnapenda sana ushabiki usio na tija mkuu

Ukraine ni taifa huru lililojimega kutoka muungano wa SSR na likapewa uhuru wake na kutambulika kimataifa, na tena halikuwa taifa hilo pekee katika kujimega kutoka muungano huo na yote yalitambuliwa

Linapokuja suala la namna ipi Ukraine ijiendeshe, taifa lolote halina mamlaka ya kuliamlia kwa wananchi wake

Russia ni mhuni tu na hii lana haitawaacha mkuu,hata wakishinda leo, lakini miaka mingi ijayo, hiyo laana itawarudia
 
Kuna sababu zngine kabisa sio NATO kuikaribia Russia kwani mpaka sasa NATO inapakana na Russia ktk nchi za
Estonia
Latvia
Lithuania
Norway
Sweden
Hivyo vita vipo kugombani Mali nguvu kazi na utaalamu
Russia alitumia advantage ya mukataba wa Minsk ambazo katika masharti yake ni kufanya Ukraine sehemu salama isiwe na siraha za maangamizi
Kwa hila hizo Ukraine alisalimisha siraha zake Kwa Russia
Hilo gap ndilo alitumia Russia kuivamia Ukraine
Kama Ukraine asinge salimisha siraha zake ingekua Kati ya nchi zenye siraha za nyukiria duniani
Na isngekua na haja ya kuombaomba siraha
 
Wewe ni mpuuzi inapaswa upuuzwe.
Kama Cuba ni nchi huru kwann hairuhusiw kuruhusu urusi waweke silaha zake pale??
 
Jitahidi sana kutafuta maarifa. Pia jiulize kwa nchi majirani zinazoizunguka nchi yako ya Tz ni ipi ina muhimu zaidi kwa Tz Kiusalama au hata Kiuchumi.
Pia jiulize ni kwanini Muungano wa Tanganyika na Znz una faida zaidi kwa Tanganyika.
Jirani yetu muhimu ni Kenya kibiashara akifatiwa na Uganda.

Kiusalama macho yetu yapo zaidi Rwanda Burundi na Mozambique na Congo

Hawa wengine Zambia na malawi sio kivilee
 
Munapenda sana kujisahaulisha hata Cuba 🇨🇺 Mexico 🇲🇽 Venezuela 🇻🇪 pia ni mataifa huru hizi laana pia zitamtesa marekani mpaka qiama wala sio Russia 🇷🇺 tuuuu
 
Wewe unaongelea mkataba wa Budapest wakati wa ussr lile lilikua kosa kubwa sana ambalo Ukraine walilifanya maana kwa dunia tulokua nayo kama ukiwa na nyuklia hata uwe unachinja watu hadharani hakuna taifa litakalo Kuja kukuvamia labda itokee mtifuano wa ndani kama Pakistan au vishambulizi vidogo vidogo vya mpakani na dunia ya leo hata ukimiliki silaha za sumu uweze kuzirusha tu bara moja kwenda jengine lazima uheshimike ila mkataba alokiuka Ukraine ulikua ni mkataba walousaini pale minsk
 
Katika majirani wote wa Russia ni Ukraine tu ambaye akijiunga NATO atahatarisha usalama wa Russia? Mbona majirani zake wengine wamejiunga na hana habari nao?
Unaonaje ukarudi kwenye vitabu mbalimbali ,ili upate uelewa wa hii zana ya usalama kwa Russia? Sababu nakuona huna taarifa za kutosha kuhusu NATO na Russia kuhusu makubariano yao yakiusalama waliyoingia baada ya vita baridi(cold war) kuisha..mkataba wa Ukraine na Russia..angalau ungesoma ungeelewa vzuri hii zana ya usalam .

Hapa utapewa elimu hutaelewa,nenda kwanza kasome
 
Cuba pia ni nchi huru inayotakiwa kuamua mambo yake bila kuingiliwa na mtu yeyote, nini kilisababisha Cuban missile crisis?

Kwanini uwepo wa makombora ya nyuklia Cuba ilibaki kidogo kusababisha vita ya tatu ya dunia?

Ukielewa hilo utaelewa kwanini Urusi aliivamia Ukraine.

Na pia kama unaelewa jiografia ya Urusi, sio rahisi kuvamiwa na Nato kupitia Finland, eneo pekee ambako Urusi yupo vulnerable kwa Nato na ni karibu sana na Moscow ni kupitia Ukraine ndio maana hakuna namna Urusi anaweza ruhusu Ukraine ijiunge Nato au kuwa koloni la Marekani.

Tukirudi kwenye hiyo Cuban missile crisis, kwanini Marekani walikubali kuondoa makombora yao ya nyuklia Italia na Uturuki ndio Urusi nae akakubali kuondoa ya kwake Cuba?

Au wewe hii ishu unaiangalia kuanzia 2022??!!

The Cuban Missile Crisis, also known as the October Crisis (Spanish: Crisis de Octubre) in Cuba, or the Caribbean Crisis (Russian: Карибский кризис, romanized: Karibskiy krizis), was a 13-day confrontation between the governments of the United States and the Soviet Union, when American deployments of nuclear missiles in Italy and Turkey were matched by Soviet deployments of nuclear missiles in Cuba. The crisis lasted from 16 to 28 October 1962. The confrontation is widely considered the closest the Cold War came to escalating into full-scale nuclear war.[1]
 
Ngoja tuone pengine leo mbuzi atacheza baada ya kupigiwa gitaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…