Nadhani ishu ya south korea ilikuwa designated kutia pressure kwa North Korea asipeleke askari kujifunza modern warfare Urusi na Artillery shells. Ila katika kui stage walifanya miscalculation au hawakutegemea backlash ya bunge na wananchi
Hii ni intelligence failure kwa South Korea na backers
Naomba nitofautiane nawe kwenye hili mkuu.
Kinotokea Korea Kusini ni jaribio la mapinduzi linofanywa na wapinzani wa serikali dhalimu ya kidikteta.
Hizi serikali (ikiwemo ya Ufaransana Ujerumani) zataka kuleta sheria kali za kubana bajeti za nchi zao (Austerity) na kulazimisha kwamba vita ya Ukraine ni lazima Korea Kusini ishiriki kwa kupeleka silaha na vifaa mbalimbali vya kivita kule na hata kwa Israeli kule Gaza.
Pia Korea Kusini yashirikiana na Marekani pamoja na Japan ili kuikabili China kwa pande ile hivyo ni kama jicho la Marekani kule.
Kwa sheria na katiba ya Korea Kusini nchi hairuhusiwi kupeleka silaha kwenye maeneo yenye migogoro.
Kwa kuwa Korea Kusini na Japan kwa upande ule wa mashariki ya mbali wamejiunga na NATO ni lazima nao wachangie shughuli za kiharamia. Kama wakumbuka kule Japan nako kulitokea zogo juzijuzi tu linohuhusiana na mambo kama haya.
Kwahiyo chama cha upinzani kinapojaribu kupinga huo ujinga wa serikali kuweka sheria kadha wa kadha kandamizi ikiwemo ya kuzuia watu kutohoji, serikali ya raisi Yoon yaja na kuweka matumizi ya nguvu za kijeshi (Martial Law) na kusema walo wanopinga agenda ya serikali ni washirika wa Korea Kaskazini.
Ukae ukifahamu serikali ya Korea Kaskazini kiufundi ni serikali inoongozwa na jeshi na ndo maana ilipotokea vurugu bungeni jeshi mara moja likaingia bungeni badala ya polisi.
Ukiweka Martial Law wazuia shughuli za kisiasa, watu kuhoji, kuchungulia matumizi ya mitandao, kukamata watu hovyo bila warrant na kuwalazimisha wale wanogoma warudi kaziniau la waende jela huo niudiketeta wa hali ya juu.
Hio nimeeleza kwa kifupi sana la sivyo ningeandika ungeona ni gazeti, lakini kinoendelea Korea Kusini ni jaribio la wale wenye kujitambua kupambana na serikali dhalimu inotaka kuingia utaratibu mpya wa kimataifa (international process)ambao saa hii wakabiliana na kuanguka kwa ubepari, utafutwaji vita, na ubanaji matumizi ya fedha za umma kwenye mahitaji ya kijamii, kitu kinopelekea upinzani wa wananchi wanojitambua ambao wapo tayari kuingia barabarani kwa namna yoyote ile.