Leo ilikua siku mbaya sana kwa Ukraine na Ulaya baada ya waziri wa ulinzi Pete Hegseth kuwapa za uso;
-Ukraine watakua wanajiliwaza kama wanadhani wataweza ku reclaim maeneo yao pre-2014
-Ukraine kuwa mwanachama wa NATO haitokua sehemu ya mazungumzo ya amani na kusitisha vita na Urusi
-Marekani haitakua kabisa sehemu ya walinda amani alio propose Zelensky wakae kwenye DMZ, Ulaya wameachiwa hilo jukumu kama watajihisi wana msuli huo ila amewaambia kabisa article 5 haitohusika Urusi akiwashambulia, ila hata hivyo Zelensky alishasema kama Marekani hayumo kwa hao walinda amani basi mpango mzima hauna maana.
-Jukumu la kuisaidia Ukraine, Marekani wanawaachia Ulaya ili a focus zaidi na kupambana na China ambao kwao wanaona ndo project ya muhimu zaidi kuliko Ukraine.
-Zelensky amesema yupo tayari kubadilishana eneo wanalokalia kwa muda huko Kursk kwa maeneo ya Ukraine anayokalia Urusi, sasa ukitaka kujua huyu rais wa Ukraine ameshakua chizi chukua ramani, tena usichukue hata ramani ya Urusi yote, chukua ramani ya Kursk uone hiko ki eneo ni % ya Kursk nzima, halafu angalia maeneo ya Ukraine anayoshikilia Urusi.
-Na Urusi wameshamwambia hilo eneo yeye aendelee tu kukaa nalo watalichukua kwa muda wao.
-Hata deal ya $500b ya rare earth minerals kumbe sio kwa ajili ya future defense ya Ukraine, kumbe lengo ni Marekani warudishe walau gharama ya silaha na misaada waliyotoa kwa Ukraine in the past.
-Hii maana yake ni;
..Ukraine amepoteza nguvukazi kubwa sana kupitia vifo vya vitani na wengine kukimbia nchi ambayo hatoweza kuirudisha mpaka mwisho wa dunia.
..Nchi imeharibiwa vibaya mnoo haiwezi kujengeka tena.
..Hana jeshi tena.
..Ameshapoteza tayari zaidi ya asilimia 20 ya eneo lake na wataalamu wanasema Urusi akifika tu kwenye mto Dniper (Huu kimsingi ndio unaigawa Ukraine pande mbili) ndo utakua mwisho wa Ukraine kama "nchi", hili hata Budanov alilisema.
..Wanaenda kupoteza tena madini adimu ya zaidi ya dola bilioni mia tano.
-Sasa ukitazama yote hayo, kwanza kibinadamu unajisikia kuwahurumia sana waukraine wa kawaida ambao hawana say kwenye maamuzi ya nchi, katokea mpumbavu mmoja alikua anafanya comedy akagombea wakampa nchi, kaja kuharibu kila walichojenga kwa miaka kibao, na ameharibu ndani ya muda usiofika hata miaka mitatu.
-Huyu Zelensky ukimfikiria, hata adhabu ya kifo unaona ni ndogo haimstahili.
-Alitaka ku achieve nini wakati wazungu wana offer kum evacuate yeye akawa anawaambia "give me weapons, I don't want a ride"??!!
-Hata baada ya vita kuanza alikua na nafasi kubwa sana ya kuokoa mengi katika hayo ambayo kwa sasa keshayapoteza ila sijui kwa kichaa cha namna gani akaamua kumsikiliza mwehu mwenzake Boris Johnson akaendeleza mapambano wakati wenye akili walishamwambia mapema hakuna namna nchi ambayo haina nyuklia inaweza ikaishinda kivita nchi ambayo ni nuclear super power. Na alijua kabisa hakuna namna Marekani ange risk vita ya nyuklia ipelekee mwisho wa dunia kwajili ya Ukraine!!
-Wengine waliokua wanaona mbali walishasema ni hatari zaidi kuwa rafiki wa Marekani kuliko kuwa adui yake.
-Wakubwa wamezozana miaka mitatu halafu leo wameelewana, Trump kaanza kupiga simu kwa Putin kabla yake katika maandalizi rasmi ya kumuacha kwenye mataa!!
-What was he thinking??? Alihisi mwisho wa hii vita ulikua upi??