LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
🤣🤣🤣🤣

Umejua kunichekesha.
 
Alibakia baada ya waziri mkuu wa Israel kuongea na Putin akamuomba Putin amhakikishie kwamba hatomuua Zelensky, baada ya Putin kutoa hiyo commitment ndio Zelensky akaanza kiburi kwasababu anajua Putin ni mtu wa kuheshimu kauli.
Huu ni mwendelezo wa propaganda,mithili ya zile zinazodai urusi aliondoka Kiev Ili kuonesha Nia njema.., kumbe alipewa kipondo akakimbia 🏃🏃
 
Hakuna huruma kwenye vita, Urusi hata yeye anahofia "retaliation" itakayofanywa kwake its either akubali moja apige Ukraine apoteze sehemu kubwa ya uchumi wake
 

Ajabu ni kuwa na nyinyi Leo mnaendeleza huo ujinga kwa kufurahishwa na trump😍🤩

Mnaweza kuona miaka 4 mingi lakini mambo yanaweza kwenda hivihivi mpaka muhula wa Trump ukaisha kisha akaja kiongozi mwingine pro-kyiv haswa,nani alitegemea Biden ataondoka Whitehouse na kuacha vita hii ikiendelea!?., nadhani hakuna binadam wa kawaida alitegemea hili!
 
 
Dah andiko hili Lina ubunifu mkubwa. Sana,maneno machache TU lkn mazitoo mno.
 
Trump amekua ni Kwa faida ya zelensky na Ukraine yake.
Wala Trump Hana msaada wowote kwa Urusi.
Urusi haisumbuliwi na binadamu yoyote wa USA atakae kua Rais wa USA.
Urusi imeweza kuwafanyia ujeuri Marais wote wa USA tokea Putin akiwa madarakani.

Tuachane na habari za zamani USSR ilipozivamia chekoslovakia na Afghanistan.
Tuangalie Putin TU alivyowatesa Marais wanne wa USA.

Urusi iliipiga Georgia na kukomboa majimbo ya Southern Ossetia na Abkhazia bush akiwa Rais.

Urusi ilichukua Crimea Obama akiwa Rais.

Urusi inaipiga Ukraine na imechukua Donbas Biden akiwa Rais.

Urusi inaendelea kuipiga Ukraine na kuchukua maeneo zaidi Trump akiwa Rais.

Tumsubiri nani aje kua Rais wa USA ndio ataidhibiti Urusi labda.?
Tuambie.
 
Ndoto ya Putin ilikuwa ni kuiteka Ukraine ndani ya siku 3..,kama ulingalia mkutano kati ya zelensinky na trump wote wakikubaliana katika hili,Tena Trump alienda mbele zaidi na kusema huenda hata siku 3 zisingefika😁😁

Hivyo mpaka hapa Putin kafeli.., kutoka kuiteka Ukraine ndani ya siku 3 mpaka mwaka wa 4 Sasa🏃🏃
 
Uzuri pamoja na Trump kuwakingia kifua wanazidi kuchinjwa tu 🥱 🥱 🥱
 
Zelensinky ni jasiri haswa,kwa Jinsi anavomvimbia Putin..,na kwa Jinsi alivowavimbia Trump na makamu wake hapo Jana inaonesha kabisa jamaa Hana chochote Cha kumtisha chini ya jua🏃🏃
Nakupa miezi kadhaa asipochutama yatamkuta ya Sadam H
 
Oia Philippines wasome upepo vyema, wauelewe
 
Kwenye hii vita Zelensky amefaulu sana kwa kupoteza zaidi ya 20% ya nchi yake na amefaulu sana kwa kupoteza rasilimali zilizoko Donbas na soon anaenda kufaulu kwa kupoteza madini yaliko kwenye maeneo ya Ukraine yaliyobaki chini ya Ukraine
 
Kumbe wewe ni msomaji wa ndoto.
Basi na Mimi nasoma ndoto ya NATO kua walidhani wataishinda Urusi kupitia Ukraine Kwa kushirikiana Mataifa 59 kijeshi na kivikwazo lakini matokeo yake wamameamua kuungana na Urusi.
Sasa kama Ukraine ni mwamba apigane peke yake bila USA.
Hata Trump Jana kasema Ukraine bila USA Putin angeshaichukua Kiev mapema TU.
Lakini Sasa Urusi ni ya nne kiuchumi.
Haya leta ndoto nyingine nami nije na nyingine.
 
Kwenye hii vita Zelensky amefaulu sana kwa kupoteza zaidi ya 20% ya nchi yake na amefaulu sana kwa kupoteza rasilimali zilizoko Donbas na soon anaenda kufaulu kwa kupoteza madini yaliko kwenye maeneo ya Ukraine yaliyobaki chini ya Ukraine

Umemjibu vizuri sana ,wajinga kama hao ndio wanatakiwa kujibiwa namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…