Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Akirudi tena kwa Trump kumpigia magoti (something to be expected), basi naamini hao jamaa wanacheza na script kwenye movie iliyokwishaandaliwa.Watamsisitizia Zele arudi kwa Trump kichwa chini na asikilize kile atachoambiwa na kusaini mkataba wa madini.
Mengine yote ni changa la macho, kutupumbaza, kupitisha muda na kupima joto la wakereketwa kama akina kp kipanya44 .
Zelenskyy yumo kwenye mfumo na ndiye asset namba moja wa CIA huko Ukreni - anafuata anachoambiwa na mabwanyenye zake.
Njia pekee ya kutamatisha vita vya Ukreni ni kumpatia Urusi anachotaka, huku Marekani na NATO wakipata kifuta-jasho cha sehemu ya mgao wa madini ya Ukreni.
Kama Ukreni hatojiunga na NATO kamwe, Putin atake nini kingine wakati zaidi ya 25% ya ardhi na mali ya Ukreni iko mikononi mwake?
Trump anamkomalia Ukreni kwenye madini ili kujiliwaza kutokana na Marekani kushindwa vita hivyo.
Hii ina maana kwamba kama Ukreni angeshinda, basi Marekani angepakalia hapo Ukreni kama bosi mpya!
So far, kila kitu kinaenda kulingana na mpango wao. Russia is overjoyed, Trump is happy, NATO is relatively okay, Ukraine cool and is about to be snatched from complete extermination, and the world safer once again!