Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ajabu ni kuwa na nyinyi Leo mnaendeleza huo ujinga kwa kufurahishwa na trump😍🤩

Mnaweza kuona miaka 4 mingi lakini mambo yanaweza kwenda hivihivi mpaka muhula wa Trump ukaisha kisha akaja kiongozi mwingine pro-kyiv haswa,nani alitegemea Biden ataondoka Whitehouse na kuacha vita hii ikiendelea!?., nadhani hakuna binadam wa kawaida alitegemea hili!
Kipanya naona umeandika kwa hisia kabisa,, pole sana, afu naona unaandika leo comment zako kwa hisia zako kabisa,, sio kama siku za nyuma kukopi na kupest habari kwenye vyanzo uchwara na kutupostia humu,, leo hata kile kiposta chako cha wamekufa wangapi urusi ujatupostia.
 
Kipanya naona umeandika kwa hisia kabisa,, pole sana, afu naona unaandika leo comment zako kwa hisia zako kabisa,, sio kama siku za nyuma kukopi na kupest habari kwenye vyanzo uchwara na kutupostia humu,, leo hata kile kiposta chako cha wamekufa wangapi urusi ujatupostia.
Mkuu, mwacheni tu huyu jamaa asee. NATO hawajamlipa hela yake ya posho tangu Novemba mwaka jana, wakati tayari kafanikiwa kuwachinja askari kibao wa Urusi.
 
🇩🇪 Diplomacy fails when negotiating partners are humiliated in front of the whole world, German President Frank-Walter Steinmeier harshly criticized US President Donald Trump

➡️"The scene in the White House took my breath away. I would never have thought that we would ever have to defend Ukraine from the United States," Steinmeier said in an interview with the German news agency dpa.

➡️"We must not allow Ukraine to have to accept submission," Steinmeier added.

➡️He also expressed his belief that Germany, after holding snap elections a week ago, "urgently needs a strong government" to overcome the crisis.
 
Up to 150 Ukrainian militants eliminated in Russian strike on testing ground
Russian forces used an Iskander missile system, the Russian Defense Ministry said
MOSCOW, March 1. /TASS/. Russian forces, using an Iskander missile system, have carried out a strike on a testing ground of the Ukrainian armed forces in the Dnepropetrovsk Region, eliminating up to 150 militants, including up to 30 foreign instructors, the Russian Defense Ministry said.

"The crew of an Iskander-M missile system has delivered a strike on the Novomoskovsky military testing ground in the Dnepropetrovsk Region where servicemen from the Ukrainian 157th mechanized brigade were being trained. As a result of the strike, up to 150 Ukrainian nationalists, including up to 30 foreign instructors, were eliminated," the ministry said.
 
1 Mar,
Trump wants to stop ‘meat grinder, ’ Zelensky needs money to continue — Musk

WASHINGTON, March 1. /TASS/. US President Donald Trump during a meeting with Vladimir Zelensky in the White House insisted on halting the Ukraine conflict while Zelensky wanted money for it to continue, American entrepreneur Elon Musk who is in charge of the US Department of Government Efficiency (DOGE) said.

"Trump pushed for a ceasefire that would have stopped the meat grinder. Zelensky wanted it to continue with the money," he said in a commentary on the X social network.

On February 28, Zelensky arrived at the White House for a meeting with Trump. Their televised exchange, with reporters present, unraveled into a shouting match, with Trump scolding Zelensky for being disrespectful to the US, and Vice President JD Vance noting that Zelensky had not ever said a "thank you" for all the support provided to Kiev. A news conference scheduled to follow the meeting was canceled, and Trump posted a statement on the Truth Social media platform saying that Zelensky was disrespectful and not ready for peace.
 
Lile bomu nililogeuza kiwanda cha silaha majivu, niliwaambia liliwaogopesha sana US na washirika wake. Ndiyo maana Trump hataki kufanya Ujinga wa kutunishiana msuli na Russia!
Screenshot_20250302-104517~2.png
Screenshot_20250302-104634~2.png
Angela Merkel's words about Russia.
 
Zelensky ni mpumbavu full stop. Unapigana vita ambayo huwezi kushinda, umeua raia wa Ukraine wengi, umepoteza madini pamoja na ardhi yenye rutuba, una mdharau mfadhili wako mbele ya camera ukiwa ofisini kwake. Huyu mchekeshaji kuna Nati zimelegea sio bure😂
Halafu kuna wapuuzi wanamsifu huyo comedian wakimuona ni shujaa eti kwa kile alichokifanya...

Yaan unaomba msaada halafu unanipangia mimi nikusaidie vipi na hauna mpango wowote wa mimi kunufaika kivyovyote vile baada ya kukusaidia wewe? Ni raisi kichaa tu ambaye hana huruma na kodi za raia wake ndio atatoa misaada ya aina hiyo.
 
Zelensky’s presidency is over – Scott Ritter

The White House meeting with Donald Trump was “a setup” to discredit and remove the Ukrainian leader, the former US Marine Corps intelligence officer has told RT

Ukrainian leader Vladimir Zelensky’s presidency is over, former US Marine Corps intelligence officer Scott Ritter has told RT. Zelensky’s five-year term in office concluded in May 2024, but he has refused to hold new elections, citing martial law. According to Ritter, Washington is “fed up” with Zelensky, who US President Donald Trump recently labeled a “dictator without elections,” and is moving to unseat him.

***************************


Vladimir Zelensky is done as the leader of Ukraine

journalist and former CIA analyst John Kiriakou told RT, commenting on the verbal spat between Zelensky and US President Donald Trump at the White House on Friday.

The meeting became heated when Zelensky resisted Trump’s demand to negotiate peace with Russia, leading the latter to accuse him of ingratitude and an unwillingness to end the conflict. Consequently, Zelensky left the White House prematurely, without signing an agreement that would have granted the US rights to Ukraine’s natural resources. The planned joint press conference was canceled.

“For all intents and purposes, Zelensky is done. I wouldn’t be surprised if in three months Zelensky is living in London or some such place,” Kiriakou said on Friday. He noted that Zelensky
 
Nadhani Sasa na kuanzia Leo hakutatokea wajingawajinga wengine kama Viongozi wa Nchi kuichokoza Urusi kwa kutengemea ulinzi kutoa kwa USA.
Ni kwamba USA haiko tayari Leo wala kesho kuingia vitani kwa sababu ya viji nchi vingine mfano ki Ukraine.
Vita ya USA na Russia ikitokea ni Kwa sababu wao kwa wao watakua wamechokozana wenyewe kwa wenyewe.
Na tayari Trump keshaweka msimamo kua kama nchi za Ulaya zitaamua kuisaidia Ukraine Kwa kupeleka majeshi yao kujifanya kulinda amani basi USA haitahusika na Sheria ya NATO haitafqnya kazi hapo.
 
Lile genge la akina Joe Biden na NATO lao jambo ni moja - kujifanya wanaisaidia Ukreni kuidhoofisha Russia, huku wao wakitafuta mwanya wa kuichuna rasilimali zake.

Trump na swahiba wake Putin nao wana lao jambo - kuidhibiti Ukraine na NATO ili wamgawane jamaa na rasilimali zake.

Kwa hiyo kimsingi kila anayejifanya kuitetea Ukreni, anafanya hivyo kwa sababu tayari pua yake imenusa utajiri wa nchi hiyo.
Watamsisitizia Zele arudi kwa Trump kichwa chini na asikilize kile atachoambiwa na kusaini mkataba wa madini.
 

Trump adviser describes how Zelensky was kicked out of White House​


The Ukrainian leader’s team was “stunned” when they were told to leave, according to Mike Waltz

1 Mar, 2025 22:32

 
Nafikiri kuna mahala nimesema huko juu kwamba Zele hana uzoefu wa hii michezo ya kidiplomasia, na sasa yazidi kudhihirika.

Alotakiwa kukifanya juzi ni kusaini mkataba na si longolongo.
kabisa, kaleta longo longo, halafu sasa anaanza kuandika magazeti ya appreciation huko twitter, nadhani it's either yeye ama washauri wake walimdanganya, sahivi anataka kurudi Washington kusign, it's too late.

sasa Trump atakachofanya, ni kuongeza vipengele vya kumbana zaidi kwenye mkataba, then he will be kicked out of presidency
 
Watamsisitizia Zele arudi kwa Trump kichwa chini na asikilize kile atachoambiwa na kusaini mkataba wa madini.
Akirudi tena kwa Trump kumpigia magoti (something to be expected), basi naamini hao jamaa wanacheza na script kwenye movie iliyokwishaandaliwa.

Mengine yote ni changa la macho, kutupumbaza, kupitisha muda na kupima joto la wakereketwa kama akina kp kipanya44 .

Zelenskyy yumo kwenye mfumo na ndiye asset namba moja wa CIA huko Ukreni - anafuata anachoambiwa na mabwanyenye zake.

Njia pekee ya kutamatisha vita vya Ukreni ni kumpatia Urusi anachotaka, huku Marekani na NATO wakipata kifuta-jasho cha sehemu ya mgao wa madini ya Ukreni.

Kama Ukreni hatojiunga na NATO kamwe, Putin atake nini kingine wakati zaidi ya 25% ya ardhi na mali ya Ukreni iko mikononi mwake?

Trump anamkomalia Ukreni kwenye madini ili kujiliwaza kutokana na Marekani kushindwa vita hivyo.

Hii ina maana kwamba kama Ukreni angeshinda, basi Marekani angepakalia hapo Ukreni kama bosi mpya!

So far, kila kitu kinaenda kulingana na mpango wao. Russia is overjoyed, Trump is happy, NATO is relatively okay, Ukraine cool and is about to be snatched from complete extermination, and the world safer once again!
 
Akirudi tena kwa Trump kumpigia magoti (something to be expected), naamini hao jamaa wanacheza na script kwenye movie iliyokwishaandaliwa.

Mengine yote ni changa la macho, kutupumbaza, kupitisha muda na kupima joto la wakereketwa kama akina kp kipanya44 .

Zelenskyy yumo kwenye mfumo na ndiye asset namba moja wa CIA huko Ukreni - anafuata anachoambiwa na mabwanyenye zake.

Njia pekee ya kutamatisha vita vya Ukreni ni kumpatia Urusi anachotaka, huku Marekani na NATO wakipata kifuta-jasho cha sehemu ya mgao wa madini ya Ukreni.

Kama Ukreni hatojiunga na NATO kamwe, Putin atake nini kingine wakati zaidi ya 25% ya ardhi na mali ya Ukreni iko mikononi mwake?

Trump anamkomalia Ukreni kwenye madini ili kujiliwaza kutokana na Marekani kushindwa vita hivyo.

Hii ina maana kwamba kama Ukreni angeshinda, basi Marekani angepakalia hapo Ukreni kama bosi mpya!

So far, kila kitu kinaenda kulingana na mpango wao. Russia is overjoyed, Trump is happy, NATO is relatively okay, Ukraine is cool and saved from complete extermination and the world is safe once again!
Upo sahihi 100% ni script iliandikwa miaka mingi tangu 1991 USSR ivunjwe na kisha Russia nayo imalizwe kabisa.

Huu mpango waendelea kufeli na Marekani khasa lengo lao ni kuitawala Dunia nzima ili kuizuia China kufanya hivyo na si Russia.

Kuna mengi ya kujifunza hapo kwa wale wanozungumzia huu mgogoro wa Ukraine na si kushabikia bila kuchambua kwa makini maana wahusu Dunia nzima ambayo yaathirika na mgogoro huu.

Ukikumbuka mazungumzo kati ya Trump na Macron wiki ilopita Trump alisema nanukuu "We must have an agreement with Ukraine on critical minerals and rare earths,". Yaani lazima tuwe na makubaliano juu ya madini muhimu ya Ukraine. Macron nae akasema nchi kubwa za Ulaya yaani European Superpowers wameipatia Ukraine msaada ambao uko katika mfumo wa ufadhili, mkopo, na mkopo wenye dhamana, ambao namnukuu Macron akisema, "which are likewise to be recouped—one way or another" yaani itarudishwa kwa njia moja au ingine.

Hapo kwenye mkopo wenye dhamana ni mabadilishano ya "security guarantees" na "natural resources" ambazo nimezitaja hapo juu nilioongelea madini wanoyahitaji hawa "EU superpowers".

Hii ni aina ingine ya "Scramble for Africa" kugombania rasilimali lakini ni jambo linofanyikia kwenye bara lao wenyewe la Ulaya.

Hivyo Zele jana jinsi ni kutafuta "balance" ya kusaini mkataba na Trump na kusuluhisha mgogoro na Russia au kuwasikiliza NATO ambao usalama wao kiuchumi na kirasilimali uko mashakani endapo vita itaisha na Russia atakuwa mshindi kwa kuchukua asilimia karibu 25 ya Ukraine yenye rasilimali zote muhimu kupatikana Duniani.

Kwa watu kama sie ambae tumekuwa tukiungalia huu mgogoro na kuelewa "inner insights" bila kueleza sana twatambua kuwa hapo mlengwa ni bara la Ulaya na uchumi wake na kwamba Russia kwa kipindi chote cha mgogoro uchumi wake umeimarika na haujatetereka sana ukizingatia ingekuwa ni nchi ingine legelege. Pia asilimia kubwa ya rasilimali wanozitaka hawa wa West zote zipo kwenye maeneo yote ambayo Russia ameyachukua.

Pia hii yaonyesha kuwa Ukraine sasa matumizi yake yameisha na bara la Ulaya kwa kukosa rasilimali walozitaka imewalazimu kutumia neno tishio la Russia kusema wakata fedha za ndani na zile za misaada ya kimandeleo ili kupeleka fedha hizo kwenye bajeti ya ulinzi.

Hivyo tungoje kusikia maamuzi ya Security Summit ya leo pale London, mie nasubiria hapa Kibaigwa.

Kuna mengi ya kujifunza kwenye mgogoro huu.
 
Back
Top Bottom