LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Sasa hivi jukwaa hili ni Pro Russia TU ndio wanatamba.
Wale wazee wa maelezo meeeengi wametoweka kuelekea kusikojulikana.

waliwalisha watu wengi sana matango pori Kwa vile wanaojua Kila aina ya silaha.
Kuna watu waliaminishwa kua Urusi ni masikini,dhaifu ,jeshi dhaifu,silaha Duni,wanajeshi wa Russia hawana nidhamu,Urusi nchi masikini,Haina high tech,hawawezi kupigana muda mrefu,Urusi ni supa pawa wa mchongo na Kila aina ya blabla.lkn watu wana msemo,usemao kua, "muda ni mwalimu mzuri",hatimae muda umesema.
Wako shamba wanapalilia mpunga
 
Uchambuzi mdogo.

Kwa mara ingine tena raisi wa Russia Vladmir Putin amecheza karata yake tofauti na matarajio ya nchi za NATO na raisi wa Ukraine Zelensky lakini kwa mbaali kaeleweka kwa raisi Donald Trump.

Kila chombo cha habari kilikuwa kikiongelea kuwa mpira umetupwa kwenye ngome ya Putin na kwamba ni yeye mwenye kusema akubaliana na kusitisha vita au la.

Alokifanya raisi Putin na kupokea mpira huo ulotoka kwa raisi Donald Trump na kuangalia kilichoandikwa juu yake kuhusu kusitisha vita na pia akamsubiri mwakilishi wa Donald Trump Steven Witkoff ongee nae kidogo.

Raisi Putin ambae alikuwa na ugeni wa rafiki yake Lukashenko raisi wa Belarus baada ya kuusoma mpira huo akafuta maandishi hayo na kuandika maandishi kuhusu masharti yake yeye anoyataka yatekelezwe ili kusitisha vita, kuiondolea uwezo wa kijeshi Ukraine na pia nchi hiyo kutojiunga na NATO, kutokuwepo kwa vikosi vya NATO kwenye ardhi ya Ukraine na kutambuliwa kwa majimbo ya Crimea, Sevastopol, Kherson, Zaporizhzhia, Luhansk na Donetski.

Pia akaongeza masharti mengine mapya kwamba hata kama kutakuwa na kusitisha vita (ceasefire) basi hakuna NATO kuendelea kupeleka silaha Ukraine ambayo hadi sasa imeshindwa vita hivyo. Madai mengine ya Russia aliyasema Putin kwa Witkoff hayajasemwa wazi.

Baada ya kuandika hayo, raisi Putin kautupa mpira huo kuurejesha kwa Donald Trump, Zelenskyy na NATO. Kilibakia ni NATO leo kufanya mkutano mwingine wa kimtandao wa video (teleconferencing) ili kujadili mchezo wa Chess anocheza mzee Putin.

.Kutengeneza upya sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Donald Trump kwampatia nafasi nzuri zaidi raisi Putin ambae nae alazimika kupita Katikati ya kamba iloning'nia huku Russia ikishinda vita ya Ukraine na huku Putin akitaka kutoharibu uhusiano na raisi Trump.

Kwa mara ingine yaonyesha wazi kuwa uzoefu Katika diplomasia za kimataifa ni jambo la muhimu sana.

Ukizingatia uzoefu wa raisi Putin katika maeneo yote ya ujasusi, siasa za kidunia, michezo ya kidiplomasia na kuchanganya na umwamba kidogo vimemsaidia sana kufanya hichi kitendo alikifanya ambacho twaweza kukiita kwa kiingereza "diplomatic manvoureing" yaani kuondoa tatizo kutoka kwako na kulirudisha kwa alieleta kwa kutumia neno "Yes" likimaanisha "No" na "No" likimaanisha "Yes".

Hivyo hakuna mbuzi aliechinjwa kama alivyodai mwenzetu Kipanya44, bali kuna Putin mcheza mchezo wa Chess ambae atambua wapi kwa kutupa kete mahali gani na muda upi.
 
Ukraine ameshapata medali zake muhimu alizokuwa anafukuzia kwa udi na uvumba

1.resume flowing of military aid

2.intelligence sharing from USA

3.Access to satellite images

Kwa Ukraine hata akipigana miaka 10 hii si tatizo kwake, sanasana urusi atazidi kupoteza ushawishi kama alivofurushwa huko syria
Naona umekuwa depressed baada ya kipigo Cha Kursk, hadi huna Cha kujibu umebakiwa na ukasuku wa hizo statements tatu, labda na ile ya tutazidi kuwachinja
 
Urusi hauwezi mziki wa west. ,nikumbushe pamoja na back up ya north Korea.., Belarus., Iran.,china na wengineo,bado ameshindwa kukatiisha kanchi kadogo tu Tena jirani yake
Naona Mzee wa The Kiev independent unazidi kujizima data. Huoni collective west wanavyohangaika kuanzia vikwazo, military aids, mercenaries, military trainers na advisors, intelligence support n.k. lakini bado hawajaweza kuikokoa Ukraine kutoka katika mkono wa The Super Bear of Siberia.
 
kp kipanya44 kama msemaji wa Kiev anasemaje kuhusu hili la kuzingirwa kwa majeshi ya Ukraine huko Kursk?
Anazidi kuweweseka, tazama majibu yake hapa chini👇👇
 

Attachments

  • Screenshot_20250315-104446.jpg
    Screenshot_20250315-104446.jpg
    345 KB · Views: 1
⚡Putin made Trump's envoy Witkoff wait 8 hours while he held a meeting with Lukashenko in Moscow.
 

Attachments

  • 19141428_gmbtmydxaaakpmr_jpeg_jpegecd58dd74c18daa34dc0966b4f3c4a4e.jpg
    19141428_gmbtmydxaaakpmr_jpeg_jpegecd58dd74c18daa34dc0966b4f3c4a4e.jpg
    15.3 KB · Views: 1
Washington is “cautiously optimistic” about the possibility of ending the war in Ukraine, U.S. national security adviser Mike Waltz told Fox News after President Donald Trump’s special envoy to the Middle East, Steven Witkoff, met with Russian dictator Vladimir Putin in Moscow.
 
⚡️🇪🇺 The EU has no plans to halt arms supplies to Ukraine even if a 30-day ceasefire is agreed, DW reports, citing diplomats.
 
Back
Top Bottom