Watayachimbaje ili hali vita inaendelea trump ni kichwa maji .. hivi ikitokea russia ameikata ukrain kwa 70% hayo madini usa atakuja kuchimba wapi kwa usalama upi
Huo mkataba wa madini ni namna moja kwa Marekani kujiondoa kwenye vita vya Ukreni - angalau ili isionekane kwa dunia kwamba US kashindwa na kutoka mikono mitupu.
Usisahau kwamba vita vya Ukreni, na hasa vikwazo alizowekewa Russia, vimegeuka kuwaathiri wao wenyewe kiuchumi. Hilo liko wazi kabisa.
Isitoshe, Trump alishawaambia kitambo Ukreni hata wafanyeje, hivyo vita hawawezi kushinda - na NATO wanalijua hilo.
Kinachofanyika ni kwamba ipo syndicate fulani inapenda hivyo vita viendelee bila kujali matokeo ya mwisho, ilimradi tu wao wanafaidika kwa namna moja au nyingine
Hapa mifano kadhaa ni majaribio na uuzaji wa silaha, biashara zingine chafu, rushwa, ufisadi na hata majaribio ya kibaiolojia maabara na biashara za viungo vya binadamu.
Hivi unadhani NATO inaipenda sana Ukreni kuliko matumbo yao wenyewe?
After all, wapo wanaowaona Waukreni kama Warusi walewale tu.
Yaani, Ukreni bila utajiri wao wanaoufaidi hao wapenda vita, inaonekana kama Russia tu.
Si ajabu Trump aliwakomalia kuwadai $500B za msaada waliopewa.