LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Tatizo lililopo hapa media za West ndio zimedominate sana kwa hio mtu kama wewe ni ngumu sana kupata ukweli.

Ngoja nijaribu kukupa sababu ya hii vita kitu ambacho media ZA West hawakisemi

Sababu kubwa ni eneo la Donbas, ambalo lina mikoa kadhaa.

Marekani anataka ku dominate hiyo sehemu kupitia Ukraine.

Mwaka 2014 kulitokea vita kubwa tu, chanzo ikiwa hilo eneo. Waasi ambao wanajiita wanajeshi wa Ukraine, wamekuwa wakiua watu wa eneo hilo kwa miaka zaidi ya 5 sasa.

Sasa hivi karibuni waliambiwa waondoke, wasipoondoka wataondolewa kinguvu.

Baada ya kugoma ndo Russia kaanza kusambaratisha kambi zote za kijeshi za Ukraine.

Niendelee au unaona chenga chenga??

Hizi ni info.za ndani sio ZA CNN na BBC
Aisee UN Charter mbona iko wazi sana? Kuvamia nchi ni kosa. Kwa mfano Marekani ilipovamia Iraq ilifanya kosa, Iraq ilipovamia Kuwait ilifanya kosa, Iraq ilipovamia Iran ilifanya kosa, n.k. Putin alipovamia Ukraine amekiuka UN Charter. Kama kuna matatizo au migogoro baina ya nchi yanatakiwa yapelekwe UN yajadiliwe na yasuluhishwe. Ndiyo sababu ya UN kuundwa.
 
Moja ya viapo wanachokula wanajeshi ni kuwa tayari kupoteza maisha kwa kuilinda na kuitetea nchi yako.
 
Walimshindwa Syria ndo watamuweza Ukraine uwanja wa nyumbani.
 
Kutoka Marekani Hadi Iraq ni 6800Km. Ilichukua siku 17 Marekani Kupeleka Majeshi yake laki moja na Nusu nchini Kuwait. Vita vilianza siku ya 20 ambapo ndani ya siku 7 Saddam alikuwa kashakimbia. Pia,Sadam Hussein alikuwa na Siraha Nyingi na Jeshi kubwa Kuliko Ukraine.

Kwa upande Mwingine,Russia hata kwa Mguu unaingia nchini Ukraine. Lakini Leo siku ya 3 bado ngoma mbichi. Pia,Jeshi la Ukraine limeshitukizwa make Putin na Lavron walisema ni Propaganda za Marekani wao hawatavamia Ukraine kamwe,badala yake wakavamia.

Yaani,Nchi kubwa Kama Russia inaishitukiza nchi ndogo Kama Ukraine? Hii ni Aibu kubwa Sana.
Ndugu yangu mimi nadhani huna data kabisa za vita vya Iraq, kwanza kukusahihisha tu vita vilianzia kutoka Kuwait na Kuwait na Iraq ni kama Tanga na Mombasa hilo moja, pili Saddam hakuwa kama alivyokuwa akisema ila waarabu wanajulikana ni wapiganaji. Kukusahihisha ila vita first desert storm nchi zote unazizijuwa wewe super power mpaka wasindikizaji walijikusanya Kuwait ndio vita ilianzia pale na vilichukuwa siku 43 kuiweka chini Baghdad wanaume walipigana, USA na washirika wake wote walijumuika nchi zote. Nenda Libya siku ngapi ziliwachukuwa kuichukuwa Libya? wewe unashangaa siku mbili watu wako city centre Samora evenue huku dunia nzima ikiwa upande wako? kasome history
 
Mwisho wa hii movie ni Russia kufirisika kabisa kiuchumi na hatimaye ndio utakuwa mwisho wa urais wa Putin pia Russia atalazimishwa kulipa War Reparations kwa Ukraine.
Mwisho wa Putin ni Mwisho wa Russia ? Jiulize Sentiments za Average Russian kuhusu Other European Countries na America
Russia hana miujiza ya kuweza kumuokoa dhidi ya kuporomoka kwa uchumi wake kwa sababu kuanzia sasa hawezi kuuza chochote nje baada ya kuondolewa kwenye mfumo wa malipo wa SWIFT na
Unadhani wote wanafurahia kudeal na kina Europe na America; Anaweza kutokea China; Nchi za Kiarabu pamoja na wasiofungamana na upande wowote
pia hawaruhusiwi kutumia dola.
Kwanini hata watu wanatumia dollar..., China, Brazil na Russia na wengine wakiamua kuanza kutumia na ku-deal na currency nyingine unadhani ni nani wa kupoteza zaidi ya America ?

Ni vigumu ku-predict ila sio rahisi ku-squueze Russia kama ilivyo kwa Iran au nchi nyingine; vilevile wa-Russia wengi washazoea maisha ya ku-hassle sio kama hizo other countries kidogo tu watu wanaandamana na kuleta shinikizo kwa serikali zao...
 
Ataibeba kwenye meli mpaka ulaya?
Vita ya pili ya dunia Uingereza ilibanwa ikawa haina supplies. Marekani ilitengeneza meli ndogo ndogo nyingi zinaitwa Liberty, meli inabeba tani 10,600. Tangu 1941 hadi 1945 meli 2,700+ ziliundwa kwa kutumia shipyards 18 za Marekani. Wastani wa meli moja kuundwa kwa siku tatu. Na kipindi kile hakuna kompyuta, welding ndio imegundulika haijazoeleka. Leo kuna hadi robotics na 3D printing na vyanzo vya gesi sehemu kibao. Si unajaza silaha Mediterranean sea unabeba gesi kutoka Qatar kwa tankers.

Marekani ilikuwa inatoa supplies na vyakula kwa Uingereza na Ufaransa, inapigana na Ujerumani, inatoa msaada kwa Soviet Union na wakati huo huo inapigana na Japan.

Kabla ya Nord Stream 1 Ulaya ilikuwa inapataje gesi? Wanachukua 60% ya Russian gas kwa kuwa ni more economic and reliable, wasipoinunua Urusi watapata hasara waongeze gharama za uzalishaji na wapate shida kwenye kufikia capacity wanayopokea. Lakini wakati huohuo wao watakuwa na option ya kununua gesi kwingine, ila Urusi atakuwa hana option ya kuuza gesi kwingine. Nadhani uashajua nani atakula jeuri yake
 
Uzalendo uliotukuka na atakumbukwa kupata maumivu sababu ya nchi yake, watu wengine ni wazalendo wa vyama tawala na sio nchi zao, hata wakiona upuuzi wanakaa kimya tu
Hao ni wazalendo wa teuzi
 
Ndugu yangu mimi nadhani huna data kabisa za vita vya Iraq, kwanza kukusahihisha tu vita vilianzia kutoka Kuwait na Kuwait na Iraq ni kama Tanga na Mombasa hilo moja, pili Saddam hakuwa kama alivyokuwa akisema ila waarabu wanajulikana ni wapiganaji. Kukusahihisha ila vita first desert storm nchi zote unazizijuwa wewe super power mpaka wasindikizaji walijikusanya Kuwait ndio vita ilianzia pale na vilichukuwa siku 43 kuiweka chini Baghdad wanaume walipigana, USA na washirika wake wote walijumuika nchi zote. Nenda Libya siku ngapi ziliwachukuwa kuichukuwa Libya? wewe unashangaa siku mbili watu wako city centre Samora evenue huku dunia nzima ikiwa upande wako? kasome history
Kwanini Urusi imeshitukiza Uvamizi? Walisema hawatavamia lakini wakavamia,huoni waliogopa Jeshi la Ukraine kujipanga na ndio maana wakateka maeneo mengi faster. Lakini Leo ni siku ya 3 bado Kievu imeshindikana kutekwa. Baadhi ya Kambi za Jeshi za Ukraine Zimekombolewa.

Pia kumbuka Saddam Hussein alikuwa na Wanajeshi Active Milioni Moja + Plus reserve Million 4 + Wapiganaji wa Kiislamu kutoka pande zote Middle East hasa Syria na Egypt. Ukraine ina Active Millitary Personnel 160,000 TU.

Kiufupi,Ukraine hakujua Kama Urusi itavamia ndio maana ndege za Urusi zilifanikiwa kuharibu Mifumo ya Ulinzi wa Anga ya Ukraine Aina ya Pantsir na S-200 haraka Sana. Ukraine hakujipanga na Vita siku ya Tarehe 24 make Lavrov alitoka kuongea na wandishi wa Habari kwamba hawana Mpango wa Kuvamia Ukraine.
 
Discipline kama hizi zilikua katika jeshi la Roman Empire, wengine waliokua na uzalendo huu ni wakina Fidel Castro na Che Guavara.
 
Back
Top Bottom