LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Embu twende pole pole.
Putin kosa lake liko wapi?
Kaenda kinyume na UN Charter kwa kufanya vamizi. UN Charter inasema sovereignity ya kila nchi iheshimiwe na ilindwe. Vamizi alofanya Putin ni kama lile alofanya Nyerere huku Zanzibar. Tofauti watu wa Ukraine wamepewa silaha kwa hiyo watalipinga vamizi. Zanzibar tulikuwa hatuna silaha kwa hiyo vamizi la Nyerere lilifanikiwa.
 
Kitendo Cha Raisi wa Ukraine kusambaza Siraha kwa Raia tayari hiyo nchi haitawaliki Tena. Hiyo ni Somalia Mpya kabisa,Marekani alikimbia Somalia baada ya Kuona nyomi ya Raia inakuja na AK-47. Kufanya Uchunguzi akagundua Kila Nyumba moja Mji wa Mogadishu ina RPG ya Kutungulia Ndege,hapo akaona hii Vita haiwezekani Tena.
Wenzetu wakimaliza shule kabla ya kuingia chuo ni LAZIMA wapitie jeshini, hivyo kwa mwananchi was kawaida kukabidhiwa silaha ni sawa tu coz wana mafunzo ya kutosha kabisa.

Inatokea nchi nyingi hasa kama kesho lina watu wachache.
 
Kaenda kinyume na UN Charter kwa kufanya vamizi. UN Charter inasema sovereignity ya kila nchi iheshimiwe na ilindwe. Vamizi alofanya Putin ni kama lile alofanya Nyerere huku Zanzibar. Tofauti watu wa Ukraine wamepewa silaha kwa hiyo watalipinga vamizi. Zanzibar tulikuwa hatuna silaha kwa hiyo vamizi la Nyerere lilifanikiwa.
Tatizo lililopo hapa media za West ndio zimedominate sana kwa hio mtu kama wewe ni ngumu sana kupata ukweli.

Ngoja nijaribu kukupa sababu ya hii vita kitu ambacho media ZA West hawakisemi

Sababu kubwa ni eneo la Donbas, ambalo lina mikoa kadhaa.

Marekani anataka ku dominate hiyo sehemu kupitia Ukraine.

Mwaka 2014 kulitokea vita kubwa tu, chanzo ikiwa hilo eneo. Waasi ambao wanajiita wanajeshi wa Ukraine, wamekuwa wakiua watu wa eneo hilo kwa miaka zaidi ya 5 sasa.

Sasa hivi karibuni waliambiwa waondoke, wasipoondoka wataondolewa kinguvu.

Baada ya kugoma ndo Russia kaanza kusambaratisha kambi zote za kijeshi za Ukraine.

Niendelee au unaona chenga chenga??

Hizi ni info.za ndani sio ZA CNN na BBC
 
Inatoka Korona inaingia Masase....

Tayari macron ameamua kumsaidia Ukraine silaha za viata. Marekani nayo tayari imeingia mzigoni baadaya ya kumdhoofisha kiuchumi. Jamaa walikuwa wanasubili wanamwangalia Putin ana silaha gani Sansa wamemsoma tayri hapa Ni patamu Sana.

Mmarikani alivyo mjanja kahakikisha ana coordinate nchi marafiki wote na putini amejikuta yupo mtu katib china ameshamruka tayari. Sasa hapo ndo patamu
Walikuwa na kampeni ya Asad out. Mrusi akatia timu wakachemsha, sasa unafikili wataweza Ukraine ambapo pale mrusi ni kama nyumbani kwake?
 
Mwisho wa hii movie ni Russia kufirisika kabisa kiuchumi na hatimaye ndio utakuwa mwisho wa urais wa Putin pia Russia atalazimishwa kulipa War Reparations kwa Ukraine.

Russia hana miujiza ya kuweza kumuokoa dhidi ya kuporomoka kwa uchumi wake kwa sababu kuanzia sasa hawezi kuuza chochote nje baada ya kuondolewa kwenye mfumo wa malipo wa SWIFT na pia hawaruhusiwi kutumia dola.
 
Back
Top Bottom