LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Ukraine akishinda hii vita huyu Rais atapendwa sana
 
Bradha nondo zako ni muhimu sana kwetu hebu achana nae anakupotezea muda. Pale tu anapoitaja tu un naacha kumuelewa.ni lini un ilifanya haki.
 
Chukulia mambo mengine kwa wepesi tu.Utapata shambulio la moyo bure.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
umekosea kaka hivyo utakuwa umepoteza maana halisi ya great thinker, kuna watubwanauliza kwa lengo la kutaka kuelewa

sasa wewe ukiwalisha matango pori itakuwa sio poa maana wengi umu hatujui chanzo cha vita yao

tunaweza tukaulizwa uku mtaani tukajibu kupitia jibu lako kumbe tofauti na uhalisia
 
Ukitaka story za kuchekesha kama hizi unakuja kusoma hapa😀
 
Ashasema MTU yoyote aingilie mambo yake atakiona.ndo maana wote wameogopa kuingilia
Dunia ina principle zake zinazoheshimiwa na mataifa makubwa na si uoga kama unavyosema.
Russia ni taifa kubwa lenye nguvu, NATO ina nchi zenye nguvu, kusipokuwa na principle kila maisha yasingekuwa kama tuyaonavyo sasa.
 
Nilisema wa nje nje wa ndani ndani, wandani watarejea ndani ya masanduku.View attachment 2131913
Uzushi wa magharibi. Subiri mwisho wake.

Tatizo hauelewi propaganda za vyombo vya habari vya ndani na nje. Huwa unasikiliza BBC swahili kila siku ukiambiwa Africa ni maskini na wewe unaamini katika umaskini kichwani mwako na unakuwa maskini kweli kweli.

Wanachotaka ni kukuaminisha wanachotaka wao uamini ili wafanye yao. Hiyo taarifa imewalenga waUkrain wapate hamasa ya kupambana.

Lakini mwisho wa Vita tutajua nani kapata nini cha msingi vita imalizile kuokoa roho za watu na uchumi wa dunia.
 
Warusi wastaarabu Sana. Tofauti na wale wa upande ule.
Tungekuwa tumeshashudia madaraja,vituo vya umeme, hospitali,vituo vya televishini na majumba ya raia yameshateketezwa wakisingizia kuwa zinatumia as a human shield.
Mi pia nimependa ustaarabu wa URUSI, hawana shida na makazi ya watu. Sijui tungezungumza nini muda huu.
 
Halafu sikujibu mimi.Rudia upya ujiridhishe.Ingawa,nasisitiza,uonapo majibu ya utani tulia.Wengine watakufafanulia utakacho.
 
Hivi Ukraine si ni nchi huru?
Sasa mbona kama Russia anawapangia wenzie? Kwani ye hofu yake nini km NATO wakiweka hizo silaha huko Ukraine? Ye si anasifiwa ana nguvu za kivita,na jeshi nk!

Basi km ni hivyo anawaogopa NATO
Hata marekani pamoja na maguvu yake yote hawezi kukubali Russia au China waweke makombora yao ya nuklia Cuba, Haiti, Mexico, au Canada, japo ni nchi huru. Hiyo ni issue ya msingi sana kiusalama usiichukulie kirahisi hivyo.
 
Aisee hizi siasa za vita ni ngoma sana. Afu kuna watu mnaishabikia US kama vile ni dini yenu
Idadi kubwa ya vyombo vya habari vinavyoripoti kile kinachoendelea katika mapambano ni kutoka Ulaya (ikiwemo Ukraine), pamoja na Marekani.

Vipo kadhaa ambavyo vinaeleza vizuri matukio na mwenendo wa mapigano pande zote. Vyombo vya habari hasa vya Urusi vimekuwa vikiripoti zaidi kuhusu progress ya hiyo "operation" yao.

Mpaka sasa sijaona chombo cha habari cha Urusi kikizungumzia kwa undani madhara yaliyopatikana kwa upande wao kitu ambacho ni tofauti sana na media zingine tunazozifahamu.
 
Halafu hawa USA na UK ndio walitakiwa kukaa kimya kabisa sababu hata wao USA hawakuruhusu kabisa CUBA kuwa kitua cha Russia wakaweka vikwazo mia kidogo na kujaribu kumuua Castro lakini kilichowasaidia wa CUBA ku survive ni USSR wakati ule na ukija hawa Uk wameuwa watu wangapi Nothern Ireland kwanini wasingeiacha tu wajiamulie wenyewe lakini wanajuwa N.Ireland ni buffer zone yao hakuna msafi
 
Natoa tu angalizo kufuatia hii vita ya Russia na Ukraine ni lazima bei ya Nishati katika soko la dunia itapanda.

Tujiandae kisaikolojia kununua petrol buku 3 na ushee kwa lita jijini Dar es salaam

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…