Ngoja nikueleweshe Kidogo hapa.
Makampuni ya Kutengeneza Siraha nchini Marekani Kama Reython,Northgrop,Boeing na Mengine yanamilikiwa na watu binafsi Chini ya Sheria ya kudhibiti Siraha ya Marekani.
Kwahiyo,Biden anaposema Anatoa $ 600m kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine anamaanisha hivi;
Akipata Hizo pesa atanunua Siraha kutoka kwenye Makampuni ya Marekani,Siraha hizo ndizo hutumwa nchini Ukraine.
Usione Makampuni ya Siraha ya Marekani yanatumia Pesa Nyingi Sana kuwafadhili wagombea Urais na Ubunge nchini Marekani,Kwasababu wanatafuta Influence ya kuuza Siraha. Vita ni faida kwao. Pia,hawawezi kuuza Siraha Popote pale Duniani bila idhini ya Bunge.
Kwahiyo Usifikili Biden ana ghala la Siraha pale Marekani,laa hasha,yeye anatoa fedha za Serikali kununua Siraha kutoka kwenye Makampuni ya Marekani.