LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mkuu dinia ya sasa sio ya Maguvu Bali ni akili. Huu no mtego kwa Mrusi na (japo Ukraine anaumia zaidi) Mataifa ya Magharibi na Marekani ni wajanja sana.
Hapa Putin anajengewa chuki duniani kuwa yeye ni katili, Ukraine atasaidiwa kimikakati na KUPEWA silaha ili amdhoofishe Russia, Economics sanctions zitawekwa za kila namna na mwisho kabisa option ya kumchapa kijeshi itaangaliwa.

Kwa sasa kuna watu wanaona kama Mmarekani kaufyata na sasa Russia ndio kidume, ila jiulize Mmarekani anapoteza nini ata akiamua Kukaa kimya?

Kuna watu wanashindwa kujiuliza hili swali. Nato haijawai kumeguka wa kutetereka kiuchumi sasa Je? Nguvu yao ipo wapi kipindi hiki?
Jibu: Yote yanayoendelea ni kwa sasa ni mipango yao (calculated) ndio maana huoni panic yeyote wa hofu kwao.

Stay tune na utajua kuwa Super power wa Dunia sio kumiliki michuma michuma .
Yaan ww kilaza wa SHULE ZA KATA ujue MTEGO afu KGB WASIJUE??? [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kwani lengo la kuivamia Iraq lilikua ni kuua magaidi gani?

Huko Iraq si mlisema Sadam Hussein ana silaha za WMD? Mkavamia mkaua watu na kuiharibu nchi lakini mpaka leo hizo silaha za WMD hazikuwahi kuonekana huko!
 
Kwa vita hii ya Ukraine ameonesha ni dhaifu kupita kiasi,,suffurings alizopata ni kubwa na calcution zake hazijaenda kama alivyotarajia.

Binafsi nimemdharau maana amekula hasara kubwa Sana tofauti na nilivyotarajia mpaka anaomba msaada wa Nchi vibaraka..

Ukweli ni kwamba Ukraine angekuwa na silaha kama ilivyo Iran , Russia asingetia pua,amefaidika na timing tuu.
Hasara ipi mkuu, kuna miundombinu iliyoharibiwa URUSI?? Marekani walipoingia SYRIA walipata FAIDA??
 
Kuhusu analysis ya uvamizi ilifanyika mapema, definitely! Hata intelligence za US na UK zilisema wazi kabisa kuhusu kuanza kwa uvamizi siku chache zilizopita.

Spirit ya Ukraine katika mapambano ni kubwa sana, so far. Nadhani dunia imeona, hivyo misaada ya kijeshi inayoongezeka si jambo la kushangaza. Silaha za kivita kama anti-tank missiles: British NLAW pamoja na Javelins kutoka Marekani zimesaidia kwa kiasi kikubwa sana kwa sasa dhidi ya vifaru vya Urusi pamoja na helicopters, kulingana na taarifa zilizopo.

Mizinga pamoja na stinger missiles kutoka Czech pamoja na Baltic states pia vimekuwa msaada mkubwa kwao, bila kusahau TB2 drones kutoka Uturuki. Kuna taarifa ya muda si mrefu kuwa nchi takribani 28 zimeridhia na zinapanga kupeleka misaada zaidi zikiwemo silaha.

Kuna taarifa pia kuwa Ukraine imeomba msaada kwa shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu kusaidia kuondoa maelfu ya miili ya wanajeshi wa Urusi kuirudisha nchini Moscow. Kama ni sahihi (kulingana na taarifa ya Naibu Waziri Mkuu), inaonesha resistance iliyofanyika ni kubwa sana.

Hata hivyo, bado ni mapema. Tusubiri tuone kile ambacho kitajiri hapo baadaye!
Mwisho wa siku wataingia ulingoni liwalo na liwe.

Screenshot_20220226-150411_Twitter.jpg
 
Hata marekani pamoja na maguvu yake yote hawezi kukubali Russia au China waweke makombora yao ya nuklia Cuba, Haiti, Mexico, au Canada, japo ni nchi huru. Hiyo ni issue ya msingi sana kiusalama usiichukulie kirahisi hivyo.
Okay sawa!
Kwahiyo solution ni kwenda kumpiga na kuiharibu nchi ya mwenzie!? Duh
 
Lakini ukiona wanavyosifiwa hapa na wataalamu ya maswala ya Vita wa Jf utadhani basi tena Ukraine kwa sasa ndiyo basi tena[emoji23]
Mwenzangu wataalamu wa vita wa jf kiboko[emoji16][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Screenshot_20220226-153726_Instagram Lite.jpg


Baada ya kuona simu zake hazipokelewi na maraisi wote wa Ulaya, rais wa Ukraine 🇺🇦 ametoa wito kwa watu wote wenye mapenzi mema na nchi yake waende kumsaidia.

Hii ni nafasi kwa Watanzania mnaosema bora mzaliwe mbwa Ulaya kuliko binadamu bongo.

Nendeni mkabebe mtutu, hii vita ni fupi sana inaisha ndani ya siku tano tu
 
Mwisho wa hii movie ni Russia kufirisika kabisa kiuchumi na hatimaye ndio utakuwa mwisho wa urais wa Putin pia Russia atalazimishwa kulipa War Reparations kwa Ukraine.

Russia hana miujiza ya kuweza kumuokoa dhidi ya kuporomoka kwa uchumi wake kwa sababu kuanzia sasa hawezi kuuza chochote nje baada ya kuondolewa kwenye mfumo wa malipo wa SWIFT na pia hawaruhusiwi kutumia dola.
Norh korea bado wanadunda mpaka leo na vikwazo venu mbuzi
 
Kwa hiyo sasa hivi wana jeshi wa Urusi wanaiba chakula ?
je unakubalia na mm ya kwamba Urusi haijatumia nguvu kubwa sana na ndio maana vifo vya raia ni vichache tofauti na tulivyo tegemea?
Haijatumia hata 20% ya nguvu zake. Na huwezi nitajia operation ambayo Marekani iliwahi kutumia 20% ya nguvu zake. Hata WW2 wakati wengine wametumia nguvu zote na wamepitiliza Marekani alikuwa hana hata mapigano kwake. Hapa nafanya comparison kwa sababu umeanzia kwenye kulinganisha Iraq na Ukraine
 
NATO haiwezi mshambulia Puttin sababu ya Eukraine labda tu aiguse nchi mshirika wa NATO. Wasiwasi uliopo ni kuwa Puttin hatabiriki tena. Alisema hatoivamia Eukrain lakini akaivamia. Sasa NATO imeamua kujihami kwa kuhakikisha silaha hazipo mbali na Urusi ikiwa ataamua lolote.
Hapo hujanipinga umefanya summary ya nilichosema
 
View attachment 2131960

Baada ya kuona simu zake hazipokelewi na maraisi wote wa Ulaya, rais wa Ukraine [emoji1255] ametoa wito kwa watu wote wenye mapenzi mema na nchi yake waende kumsaidia.

Hii ni nafasi kwa Watanzania mnaosema bora mzaliwe mbwa Ulaya kuliko binadamu bongo.

Nendeni mkabebe mtutu, hii vita ni fupi sana inaisha ndani ya siku tano tu
Ila huyu raisi wa Ukraine nimemkubali ni mzalendo hasa,Kagoma kukimbia nchi yake baada ya kupewa ofa na Wamarekani,na alipoona uzushi unasambazwa kwamba eti kakimbia nchi akatoa video kwa kutumia simu akihutubia taifa akiwa mtaani nchini mwake.
 
View attachment 2131960

Baada ya kuona simu zake hazipokelewi na maraisi wote wa Ulaya, rais wa Ukraine 🇺🇦 ametoa wito kwa watu wote wenye mapenzi mema na nchi yake waende kumsaidia.

Hii ni nafasi kwa Watanzania mnaosema bora mzaliwe mbwa Ulaya kuliko binadamu bongo.

Nendeni mkabebe mtutu, hii vita ni fupi sana inaisha ndani ya siku tano tu
Kusema kuwa simu zake hazipokelewi ni "kuongeza chumvi". Simu zake zinapokelewa kama kawaida, na anatoa updates za mazungumzo yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom