Kuhusu analysis ya uvamizi ilifanyika mapema, definitely! Hata intelligence za US na UK zilisema wazi kabisa kuhusu kuanza kwa uvamizi siku chache zilizopita.
Spirit ya Ukraine katika mapambano ni kubwa sana, so far. Nadhani dunia imeona, hivyo misaada ya kijeshi inayoongezeka si jambo la kushangaza. Silaha za kivita kama anti-tank missiles: British NLAW pamoja na Javelins kutoka Marekani zimesaidia kwa kiasi kikubwa sana kwa sasa dhidi ya vifaru vya Urusi pamoja na helicopters, kulingana na taarifa zilizopo.
Mizinga pamoja na stinger missiles kutoka Czech pamoja na Baltic states pia vimekuwa msaada mkubwa kwao, bila kusahau TB2 drones kutoka Uturuki. Kuna taarifa ya muda si mrefu kuwa nchi takribani 28 zimeridhia na zinapanga kupeleka misaada zaidi zikiwemo silaha.
Kuna taarifa pia kuwa Ukraine imeomba msaada kwa shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu kusaidia kuondoa maelfu ya miili ya wanajeshi wa Urusi kuirudisha nchini Moscow. Kama ni sahihi (kulingana na taarifa ya Naibu Waziri Mkuu), inaonesha resistance iliyofanyika ni kubwa sana.
Hata hivyo, bado ni mapema. Tusubiri tuone kile ambacho kitajiri hapo baadaye!