LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Yangu macho maana kwa jinsi upepo unavyo enda huwenda Putin akapakatwa.

Maana misaada inayo tolewa na yeye ana sua sua **** liza kazi ita mkost

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Screenshot_20220226-164034.png

Haya ndiyo yalikwa makubaliano kuwa leo mji mkuu wa Ukraine mapambano yasiendelee kwa ajili ya kufanya mazungumzo. Ukraine wamekataa. Operation inaanza muda huu kuanzia sasa.
 
Propaganda tu, vita bado haijapamba moto vifaru vingi namna hiyo waviteketeze?
 
India, Russia, the United States, China, the United Kingdom and France are the only countries that have operational ICBMs.
Nchi zinamiliki ICBM
 
Tsar bomb mnalijua nyie
Wewe jamaa umemeza kaneno kamoja TU. Nenda YouTube uangalie Siraha za Nyuklia alizokuwa Nazo Marekani wakati wa Vita baridi Kabla ya kuziharibu baada ya Mkataba wa Amani na USSR.

1.Atlas

2.Minuteman

3.Titan.

Hayo Makombora yalikuwa hatari Sana,japo inasemekana yaliharibiwa kwenye mkataba wa Amani,lakini nadhani huenda bado Marekani Anayo. Hayo Makombora ni LAND BASED SILOS MISSILE.
 
Kwa akili zako tu za kuzaliwa unadhani USA yuko tayari kuwekewa silaha nzito nzito na jeshi la kivita la URUSI kwenye nchi jirani kabisa na USA kama Canada na Mexico?

Ndivyo jinsi ilivyo kidunia kwa Urusi pia yuko sahihi kukataa na kujihami ni mojawapo ya kanuni bora sana za kiuongozi kwa nchi yoyote ile duniani.

Mfano USA kutengeneza silaha nzito za maangamizi kama hizo epersonics bombs ilihali anakataza mataifa mengine kutotengeneza hizo silaha, unadhani kwanini anakataza hayo mataifa mengine?

Jiulize na ujijibu mwenyewe.
Kama hadi makombora yawekwe karibu ndo waogope maana yake ile zana na majigambo ya kua na makombora ya masafa marefu inakua haina maana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Haijatumia hata 20% ya nguvu zake. Na huwezi nitajia operation ambayo Marekani iliwahi kutumia 20% ya nguvu zake. Hata WW2 wakati wengine wametumia nguvu zote na wamepitiliza Marekani alikuwa hana hata mapigano kwake. Hapa nafanya comparison kwa sababu umeanzia kwenye kulinganisha Iraq na Ukraine
Lakini mkuu nguvu iliyo tumika Iraq ni kubwa sana kwa sababu usiku wa kwanza wa uvamizi maelfu waliuwa.
 
Vita ilisimama tangu jana.. Putin aliamuru majeshi yake kutosonga mbele baada ya Zelensky kuomba mazungumzo na kusema yupo tayari Ukraine iwe neutral country isiyofungamana na upande wowote.. Putin akasema wakutane Minsk mji mkuu wa Belarus.. Zelensky kakataa anataka Warsaw Poland ambaye hasimu wa Russia.. Baadaye ghafla alipoona mashambulizi yamesita akasitisha mawasiliano.. Putin ameamuru mashambulizi yaendelee.
NA inasemekana huyo Rais ishaondoka Kiev yupo mji wa magharibi mpakani.. Picha anazotoa kuwa eti yupo Kiev inasemekana ni pre recorded... Yaani alizirekodi kabla.
Zinatumika kuhamasisha jeshi na watu wapigane Maana wakijua alishaondoka jeshi Lita surrender..
Inaonekana aliposema anataka mazungumzo Marekani imemzuia.. Maana walimwambia wameshamwandalia namna ya kumuokoa pamoja na hifadhi ili asiachie madaraka. Sasa ukweli utajulikana baadaye.. No one know exactly.
Screenshot_20220226-160748.jpg
 
Tuseme chanzo ni Marekani na washirika wake kutaka kuweka silaha zao za Nuke Ukraine kwa kupitia mgongo wa Ukraine kujiunga na NATO.

Mkataba wa Minsk uliosainiwa sijui miaka mingapi iliweka wazi kwamba NATO haitaendelea kujitanua kuelekea upande wa Urusi hivyo kitendo cha NATO kutaka kupokea Ukraine ni kuvunja mkataba huo.

Hii ndiyo maana Putin amezionya Finland na Sweden nao wakijifanya kutaka kujiunga na NATO watapigwa vibaya.

Sasa kwanini Putin azipangie nchi nyengine nini wafanye nini wasifanye? hii Dunia ni ya ajabu sana
 
Mwamba kweli hatabiriki, hata USA amekwisha ingiwa na baridi kutokana intelijensia zake alizopata kuhusu mwamba na mikakati yake.

Muda wowote atamchapa kiherehere yoyote na "Inter Continental Ballistic Missile" yenye "Nuclear War Head". Ndio wajue jamaa yupo serious.
Hii ikitokea wewe utapata faida gani..naona unaandika kwa bashasha..
 
Wamewaua Warusi 3500 dah
emoji28.png
Hakuna video. Hakuna picha ya kusapoti taarifa zao zinazoonyesha hayo yanayofanyika.

Mbona leo walivyowakamata wanajeshi wa Chechen 4 kuwatoa ndani ya gari na kuwapiga risasi na kuwaua wameonyesha video yao. Chechen walitoka jana jeshi la askari 1000. Leo 4 wameuuliwa tena muda huu. Iweje hizo za Urusi washindwe kuonyesha video hao askari waliyo waua kwa kiasi hicho wanachokisema?

Ukraine leo asubuhi wamesema Llyushin ndege ya Urusi yenye uwezo wa kubeba wanajeshi 200 wameilipua. Lakini mpaka sasa hivi hakuna picha, hakuna video.

Jana asubuhi ikatangazwa wamelipua ndege SU-27 ya Mrusi kumbe wametungua ndege ya kwao. Kucheki engine ni ndege ya kwao.

Ukraine walionyesha video wamewakamata askari wa jeshi la Urusi na kuonyesha wanawahoji hao mateka. Kuna kitu kinaitwa accent/lafudhi. Lafudhi yao si ya Warusi wana lafudhi ya Kiukraine. Ni maigizo wanafanya.

Zelensky sasa huko twitter anadai meli ya kivita ya Turkey imeizuia meli ya kivita ya Urusi kupita black sea. Lakini mamlaka ya Turkey kwa haraka imejibu muda huu yaani sasa hivi kuwa hiyo taarifa ni ya uongo.

Screenshot_20220226-170413.png


Ukraine kwa sasa hana airforce. Ukraine kwa sasa hana air defensive system. Ukraine hana drone. Ukraine hao hao wameua wanajeshi 3500 wa Urusi kwa siku 2. Amewaua kwa nini? Kwa vifaru?

Ukraine wanafanya propaganda nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii ila siwalaumu kwani ni jambo zuri hususani nyakati za vita. Unabusti morali ya raia na wapambanaji wako. Ni psychological warfare. Ni hizi habari Warusi wakizisoma zinawachanganya maandamano yanazidi Urusi na Putin anapata pressure ndani ya nchi kutoka kwa raia. Hapa wamempiga bao Putin.
 
Back
Top Bottom