LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
"Russia ina uwezo mkubwa wa kuendana na hali yoyote ile nchini Ukraine, yenyewe kama yenyewe, na wala haihitaji msaada wowote wa kijeshi wa China", msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa China imezungumza.

"Russia ni taifa kubwa lenye uwezo na nguvu kubwa za kijeshi. Haihitaji msaada toka China wala nchi nyingine yoyote"

=====


Russia is capable of coping with the situation in Ukraine on its own and does not need China's military support, Chinese Foreign Ministry Spokesperson Hua Chunying announced on Thursday.

"Russia is a great power with might. It does not need the support of China or other countries," she said at a briefing, answering a corresponding question from a Western journalist.

The Chinese diplomat noted that Beijing’s position on this issue differs from the views of the American leadership. "We will not act as the United States acts, which supplies Ukraine with a large number of weapons," she stated.
 
Hakuna video. Hakuna picha ya kusapoti taarifa zao zinazoonyesha hayo yanayofanyika.

Mbona leo walivyowakamata wanajeshi wa Chechen 4 kuwatoa ndani ya gari na kuwapiga risasi na kuwaua wameonyesha video yao. Chechen walitoka jana jeshi la askari 1000. Leo 4 wameuuliwa tena muda huu. Iweje hizo za Urusi washindwe kuonyesha video hao askari waliyo waua kwa kiasi hicho wanachokisema?

Ukraine leo asubuhi wamesema Llyushin ndege ya Urusi yenye uwezo wa kubeba wanajeshi 200. Lakini mpaka sasa hivi hakuna picha, hakuna video.

Jana asubuhi ikatangazwa wamelipua ndege SU-27 ya Mrusi kumbe wametungua ndege ya kwao. Kucheki engine ni ndege ya kwao.

Zelensky sasa huko twitter anadai meli ya kivita ya Turkey imeizuia meli ya kivita ya Urusi kupita black sea. Lakini mamlaka ya Turkey kwa haraka imejibu muda huu yaani sasa hivi kuwa hiyo taarifa ni ya uongo.

View attachment 2132037

Ukraine kwa sasa hana airforce. Ukraine kwa sasa hana air defensive system. Ukraine hana drone. Ukraine hao hao wameua wanajeshi 3500 wa Urusi kwa siku 2. Amewaua kwa nini? Kwa vifaru?

Ukraine wanafanya propaganda nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii ila siwalaumu kwani ni jambo zuri hususani nyakati za vita. Unabusti morali ya raia na wapambanaji. Ni psychological warfare. Ni hizi habari Warusi wakizisoma zinawachanganya maandamano yanazidi Urusi na anapata pressure ndani ya nchi kutoka kwa raia. Hapa wamempiga bao Putin.
Yule jamaa si alikuwaga comedian kama Kingwendu yule, na nyie mnamuamini[emoji28]
 
Kikao cha jana jioni cha NATO plus Finland na Norway kuna siri itakuwa pale imeamuliwa. Naanza kuona response ya kina Biden haikuwa mbaya sana kama nilivyoona mwanzo. Maybe ni tunakusubiri upige wee dunia ikuone, alafu tukija utakosa visingizio vya kwamba sisi ndio tulianza
Plan ya kushughulikia kwa yeyote atakaye ingilia demilitarization na denazification operation huko Ukraine ipo tayari!!! Sidhani kama Russia alikuwa anafanya utani katika hilo. Sidhani.
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine amesema Uturuki imekubali kufungia meli za Urusi kupita straits za Black sea. Ikitokea hivyo meli za Urusi hazitapita kwenda kushambulia Ukraine mpaka watumie bandari iliyopo Crimea
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ujue humu kuna wapumbavu sana. Eti URUSI imedanganywa na wameshaingia kwenye Mtago. Yaan mtu anayejua haya anaishi kwa MTOGOLE hana hata Jeans ya 50k mwilini. Amesoma shule ya kata na hata hajawahi kuiona hata Beaker ikiwa maabara. URUSI wana kitengo cha usalama KGB na wanauwezo wa kuhack hata uchaguzi wa USA afu useme wameingia vitani bila ANALYSIS this is JOKE.
😂😂😂 haya mkuu.
 
Binafsi naunga mkono maamuzi ya Putin, USA na wenzake wa NATO wanatishia usalama wa Russia.Linapo kuja suala la usalama wa nchi hakuna mjadala. Ikiwezekana Putin aandae ICBM zake ikitokea wameingilia atume hizo kitu kwa USA na washirika wake. USA hajaadhibiwa kwa muda sasa baada ya kufanya uhalifu mwingi wa kivita katika nchi zingine.
 
Plan ya kushughulikia kwa yeyote atakaye ingilia demilitarization na denazification operation huko Ukraine ipo tayari!!! Sidhani kama Russia alikuwa anafanya utani katika hilo. Sidhani.
Hawana haja ya kuingia Ukraine, wanatoa silaha tu na operation ya kiini macho ya denazification inakwama. Na anayeongoza kuiua ni Myahudi Zelensky ambaye mababu zake waliuwawa na hao Nazis
 
Tuseme chanzo ni Marekani na washirika wake kutaka kuweka silaha zao za Nuke Ukraine kwa kupitia mgongo wa Ukraine kujiunga na NATO.

Mkataba wa Minsk uliosainiwa sijui miaka mingapi iliweka wazi kwamba NATO haitaendelea kujitanua kuelekea upande wa Urusi hivyo kitendo cha NATO kutaka kupokea Ukraine ni kuvunja mkataba huo.

Hii ndiyo maana Putin amezionya Finland na Sweden nao wakijifanya kutaka kujiunga na NATO watapigwa vibaya.
Russia ilikuwa na sauti enzi za USSR sasa hivi hana lolote
 
Inakumbusha wakati JWTZ inasambaza kichapo kwa m23, wao wanaingia twitter wanaandika.. mwisho wa siku waliumbuka vizaya sana
 
Inasemekana ishapangwa kabisa vijana wa myahudi (jeshi la Ukraine) watafute kombora moja tu la Mrusi walivugumize Poland ili wanaume wa kazi wakiongozwa na baba yao USA waingie kazini kumalizia mission yao. Ikumbukwe kwamba Poland ni moja kati ya nchi wanachama wa NATO waliokaribu kabisa na ukanda huu wa vita. Na kwa vile sheria za NATO zinaruhusu mataifa hayo kuishambulia nchi yoyote inayomvamia mwanachama wao, basi hii ndio itakuwa njia rahisi ya wao kutimiza malengo yao walioyapanga muda mrefu. Ikumbukwe pia katika siku za hivi karibuni za mzozo huu Marekani na baadhi ya nchi wanachama wa Umoja huo wa NATO wamekuwa wakipeleka silaha nzito nzito na wanajeshi zaidi katika nchi ya Poland, Lithuania na baadhi ya nchi zingine wanachama zilizo katika ukanda huo, lengo ni kutaka kutengeneza mazingira ya kuivamia Urusi kupitia kila upande wa nchi hizo wanachama ambazo tayari kwa muda mrefu nchi hizo zina silaha na wanajeshi wa NATO karibu na mipaka ya Russia. Kitendo cha Mrusi kuivamia Ukraine ambayo bado haijawa mwanachama wa NATO wala umoja wa Ulaya huku akiziacha nchi ambazo tayari zishajiunga umoja huo muda mrefu na ni jirani zake, kimewashangaza wengi. Kama lengo ni kuzuia upanuzi wa NATO katika eneo hilo anaziachaje nchi jirani zake kama Latvia, Estonia na Lithuania ziendelee kutamba na silaha hizo za NATO badala yake anaenda kuivamia nchi ambayo bado haijafikiriwa hata kuwa mwanachama halisi wa umoja huo?

images (2).jpeg


images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom