LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hakuna kitu Marekani na Wamagharibi wenzie watafanya zaidi ya vikwazo vya kiuchumi na propaganda tu.
Umeangalia na angle ya wauza silaha na test ya silaha mpya? Maana vita zina wafaidika wake.
 
Ujinga tu. Putin na Biden na wadau wote wanaohatarisha usalama wa dunia ni WAJINGA. Wanajeshi watakufa, raia watakufa ili wao wasifiwe na watu aina yako.
Wewe ndio mjinga, jiulize kwanza kwanini hao wanajeshi unaowatetea kuu wawa kwanin wanakubali kuuwawa. Kifupi nataka nikwambie mpka hapa tulipofika kwa kila jambo kuna watu waliuwawa/walimwaga damu

Hata sisi inabidi tumwage dam zetu kwaajilia ya kizazi kesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu Wana kufa kila siku mjomba kwa sababu nyingine tofauti tofauti kifo ndio uhalisia wetu viumbe hai
Kifo kina utaratibu wake. Tunakufa kwa utaratibu maalum. Silaha za nyuklia zikitumika ipasavyo hata wewe hutakuwepo hapa kusema watu wanakufa kila siku mjomba.
 
Naona simba na yanga imeanza
Halafu unaweza kuta hii ni sinema tunachezewa huku. Nyuma ya pazia mijamaa inagonga stori na kupanga mambo yao.

Biden: Mzee ile kipande umeicheza zaidi ya holywood

Putin: Si nilikwambia niko vizuri? Hizi mambo nimezianza kitambo sana, we huniwezi

Zelensky: Hebu acheni ukuda, tuongeleeni mambo ya mpunga. Zimeshaingia kiasi gani?

Biden: Halafu na wewe mhuni yale mafaili ya Burisma ulishayafuta? Maana huku kuna wananchi wakuda sana. Kelele kibao

Zelensky: Mgao kwanza ndio kitu kinafutwa. Braza Putin keshaingia so kilichobaki ni kulipua masjala then tunasema ilikuwa ni matokeo ya vita

Biden: Dogo una akili sana. Ndio maana nilikupendekeza uwe rais

Putin: Hahahaaa, ila dogo acha kelele sana. Utakuja kufa. Nina misoja inalenga hatari
.....
 
Hakuna ujiniasi ni ujinga tu na ubabe wa Kikondoo umemjaa. Wanaokuja kuteseka ni raia wa kawaida maana yeye na familia yake wanalishwa hata kwa senti ya mwisho ya serikali. Kuivamia Ukraine bila sababu ya msingi eti kuonesha wewe ni mbabe ni ujinga. Yeye kajiunga na China na Irani nani kamzuia, mwenzie kusema anajiunga na NATO ni dhambi? Uhuru wa Ukraine anao yeye Urusi?
Masilahi ya Urusi ni NATO kuwa naye mbali.

Raia wengi watateseka na kuumia zaidi Ukraine akijiunga na NATO.

Ni genius kwa namna alivyoingia na anavyotetea masilahi yake, akili kubwa imetumika.

Otherwise hauelewi maana ya genius.
 
Alikuwepo Hitler,sasa yupo wapi?Wala sio genious. Ni vile watu wanaojielewa hawataki vita. Putin ni mgonjwa wa akili ana paranoia huyu.
Umekuwa brainwashed na propaganda za Wamagharibi.

Adolf Hitler alikuwa mzalendo namba moja wa Ujerumani. Ni vile tu washindi ndio huandika historia, otherwise the man loved his country truly.

Putin siyo genious, ni genius. Kama unamuona ana matatizo ya akili ni mtazamo wako, na sote tunauheshimu.

Reality stands; Putin is a genius and a true patriot of Russia.
 
Nakukumbusha tu kuwa ndio walioiangusha USSR.

Sio rahisi kupelekea mapambano ya vita lakini ktk eneo la hujuma, US yupo vizuri.
Ilikuwa zamani. Sasa hivi hakuna kitu.

Crimea ilienda kwa style hiihii, walifanyaje?

Hong Kong imeenda na China hivihivi, walifanyaje?

Afghanistan tu penyewe wameshindwa vibaya baada ya kupambana kwa takribani miongo miwili.

Hakuna lolote, at least enzi za Trump walijitahidi, ila hii Marekani ya Democrats ni toothless.
 
Sisi ni binadamu tunaweza sana kukaa kwa amani. Kuna watu wanaabudu legacy ndo huwa wanapenda vita. Ni tatizo la kisaikolojia.

Sasa akishakuwa raisi wa mataifa makubwa kama hao wa urusi na marekani ndo watu wanakufa kama kuku kulinda legacy zao.
Binaadamu hawezi kukaa kwa amani toa huo utandu wa fikira kichwani mwako , binaadamu in direct anazaliwa na ubinafsi pamoja na tamaa, Pindi anapokuwa na akili timamu anapo soma na kuelimika hujitahidi kushindana na ubinafsi pamoja na tamaa aliyonayo lakini kwa kuwa ni kitu ambacho huwa kipo ndani yake hujitahidi kukipunguza na sio kukimaliza kabisa , so binaadamu Ni kiumbe kinacho penda kutawala (Ni sehemu ya uchochezi wa tamaa) inapo tokea ukatawala of course hauwezi kutawala bila ya kuwa na power ,

so ukitawala utataka kujipanua Zaidi ili uweze kupata rasilimali zitakazo kufanya uendelee kuimarisha kingdom yako , ktika Hilo kuna watu watakao furahishwa na falsafa zako na Kuna watakao chukizwa n falsafa hizo , hao watakao chukizwa na falsafa hizo ndio watakuwa chem chem ya vugu vugu la Vita ,Hilo litatokea bila ya kujali utawala wako unauendesha kwa haki au kwa batili , Yakupasa utambue ubaya wa kitu au Jambo huwa inategemea na upande utao usimamia

mfano che Guevara alikuwa Ni mkombozi na mpigania haki za wanyonge , Naomba nikuulize swali kama alikuwa ni mpigania haki kwa Nini USA iliamua kumuua ..? Jibu Ni kwamba alikuwa anakwenda kinyume na sera zao so waweza kuona hapo kwamba licha ya che Guevara kuwa mwana mapinduzi na mpigania haki lakini kwa kuwa upande aliosimamia haukuwa na manufaa kwa USA Wakaona ni Bora auwawe ,, hivyo ndio dunia ilivyo usije unadhani kwamba ipo siku dunia itatulia na kukosa Vita kabisa wakati hiyo ndio asili yake ,
 
Hii UNSC wakati mwingine ni 'upuuzi mtupu'. Kama mataifa yanavamiana kijeshi, huku chombo cha kushughulikia usalama wa kimataifa kipo, basi hakuna maana yeyote ile kuendelea kuwa na baraza hilo. Tofauti na hapo, baraza hilo linahitaji marekebisho makubwa (overhaul).
ndio mnatambua leo eeh poleni na mkae kwakutulia kabisa
 
Back
Top Bottom