Binaadamu hawezi kukaa kwa amani toa huo utandu wa fikira kichwani mwako , binaadamu in direct anazaliwa na ubinafsi pamoja na tamaa, Pindi anapokuwa na akili timamu anapo soma na kuelimika hujitahidi kushindana na ubinafsi pamoja na tamaa aliyonayo lakini kwa kuwa ni kitu ambacho huwa kipo ndani yake hujitahidi kukipunguza na sio kukimaliza kabisa , so binaadamu Ni kiumbe kinacho penda kutawala (Ni sehemu ya uchochezi wa tamaa) inapo tokea ukatawala of course hauwezi kutawala bila ya kuwa na power ,
so ukitawala utataka kujipanua Zaidi ili uweze kupata rasilimali zitakazo kufanya uendelee kuimarisha kingdom yako , ktika Hilo kuna watu watakao furahishwa na falsafa zako na Kuna watakao chukizwa n falsafa hizo , hao watakao chukizwa na falsafa hizo ndio watakuwa chem chem ya vugu vugu la Vita ,Hilo litatokea bila ya kujali utawala wako unauendesha kwa haki au kwa batili , Yakupasa utambue ubaya wa kitu au Jambo huwa inategemea na upande utao usimamia
mfano che Guevara alikuwa Ni mkombozi na mpigania haki za wanyonge , Naomba nikuulize swali kama alikuwa ni mpigania haki kwa Nini USA iliamua kumuua ..? Jibu Ni kwamba alikuwa anakwenda kinyume na sera zao so waweza kuona hapo kwamba licha ya che Guevara kuwa mwana mapinduzi na mpigania haki lakini kwa kuwa upande aliosimamia haukuwa na manufaa kwa USA Wakaona ni Bora auwawe ,, hivyo ndio dunia ilivyo usije unadhani kwamba ipo siku dunia itatulia na kukosa Vita kabisa wakati hiyo ndio asili yake ,